Nini hatma ya Muungano wetu?

Nini hatma ya Muungano wetu?

twekeni kilindini

New Member
Joined
Apr 11, 2021
Posts
0
Reaction score
0
Habarini wana ndugu,

Binafsi ni mgeni katika uwanja huu awali ya yote ningependa kubisha hodi humu ndani. Mada yangu haswa ni kuhusu muungano wetu ambao tumekuwa nao kwa kitambo sasa.

Linapokuja suala la muungano tumekuwa tukisikia swala la kuwaenzi waasisi wetu ilhali kuna mengi waasisi walianzisha mathalani Azimio la Arusha na siasa za ujamaa na kujitegemea.

Pili, ni nani mnufaika wa muungano wetu mkubwa? Je, ni Zanzibar, Tanganyika, CCM au wote?

Tatu, kama ni Tanganyika na sababu ni za kiusalama kama inavyodaiwa ni kweli Tanganyika haipo salama bila Zanzibar au ndio fear of unknown kama vile kijiji ambacho wote wanasema kuhusu mzimu lakini hakuna aliyewahi kuuona?

Binafsi bado naupenda muungano ambao wenye maslahi kwa pande zote mbili.

Nakaribisha kuelimishwa zaidi.
 
Back
Top Bottom