Nini hatma ya ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo (China project) ikiwa bandari zote kachukua Mwarabu wa Dubai?

Nini hatma ya ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo (China project) ikiwa bandari zote kachukua Mwarabu wa Dubai?

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2013
Posts
11,550
Reaction score
40,697
Nimejaribu kuwaza kwa kina haya yanayoendelea hapa Tanzania kuhusiana na sekta ya bandari.

Sote tunajua tayari Serikali na bunge wamepitisha na kusaini mkataba wa uendelezaji na uendeshaji shughuli za bandari zote za Tanganyika kuwa chini ya umiliki na usimamizi wa milele wa muarabu wa Dubai (DP world). Kupitia mkataba huo, automatically bandari ya Bagamoyo nayo itakuwa mikononi mwa muarabu wa Dubai!

Kabla ya hayo kutokea, tayari serikali ilishapitisha mpango wa mkataba wa ujenzi na upanuzi wa Bandari ya Bagamoyo baina ya Tanzania na China, mkataba ambao ulikuwa unaelezwa (Rais Magufuli alilithibitisha hili) kuwa unazuia pia uendelezaji na upanuzi wa bandari zingine zote katika mwambao wa bahari ya Hindi ikiwemo bandari ya Dar na Mtwara. Mkataba huo ulipitishwa mwishoni mwa utawala wa Kikwete, ukazimwa kipindi cha utawala wa Magufuli na baadaye ukafufuliwa na utawala wa Mama Samia.

Nini hatma ya mpango wa ujenzi na upanuzi wa bandari ya Bagamoyo chini ya mchina katikati ya mazingira ya mkataba mpya wa bandari zote za Tanganyika kuwa chini umiliki na usimamizi wa muarabu wa Dubai?
 
Bandari wanajenga TPA kwa kivuli cha fedha za waarabu

Waarabu watamwaga pesa nyuma ya pazia
Ikikamilika wanakabidhiwa/wanajikabidhi
 
Bandari ya Bagamoyo ndio kama imekufa hivyo kwa maana DP sio rahisi kwekeza kwa kiasi tulichokuwa tumepanga kwani mkataba huu hauwafungi kufanya hivyo.
 
Inasikitisha sana! Bandari ya Bagamoyo ilikuwa mkombozi kwa watu wa Pwani.
 
Kulingana na mkataba aliosaini mama yako bandari ya bagamoyo na ardhi yake ni mali ya Dp world na kama mnaitaka hiyo bandari mkataba unasema muwambie Dp world wao ndio wataamua kama wataindeleza au lah au kupiga chini maana wao ndio wamiliki wa ardhi ya bagamoyo.
 
Huenda Chinise hawakufika offer wadau awamu ya sita, wakidhani goodwill ya awamu ya nne itawabeba, Mwarabu akaweka fungu mezani." Mchuzi hunywewa wa moto"...Waswahili
 

Attachments

  • Flag_of_Tanganyika_(1961–1964).svg.png
    Flag_of_Tanganyika_(1961–1964).svg.png
    1.2 KB · Views: 4
Back
Top Bottom