zagarinojo
JF-Expert Member
- Jul 26, 2020
- 2,622
- 2,846
Jamii Forums tena. Sidhani kama ukweli juu ya maisha yalivyo ulishawahi patikana.
Je, maisha ni magumu kama wengi wasemavyo au ni rahisi Kama wachache waliofanikiwa wasemavyo? Kuna utatanishi mkuu juu ya majibu ya maswali haya.
Nimejaribu kutafakari kwa kina kama furaha katika maisha hutafutwa au hutokea yenyewe tu bila jitihada. Wakati mwingine nashindwa kuelewa nini chanzo cha furaha maishani.
Je ni fedha ulizonazo, wazazi ulionao au elimu uliyonayo au vitu unavyomiliki. Tunaishi kwenye dunia ambayo furaha haipo tena.
Tafiti mbalimbali kutoka vyanzo tofauti zinaonesha asilimia 70%wafanyakazi duniani wanafanya kazi wasizozipenda.
Si hivyo tu hakuna furaha katika ndoa, hakuna haki katika mahakama, hakuna furaha katika nyumbani zetu. Kila mtu anafanya kitu ajione juu zaidi ya mwingine. Lawama zinaongezeka.
Narejea mada yangu. Je, nini kifanyike ili upendo na furaha vitawale maishani? Nini hutukosesha furaha maishani?