Nini hukupa/kitakupa furaha maishani lakini nini hupelekea kukosa furaha?

Nini hukupa/kitakupa furaha maishani lakini nini hupelekea kukosa furaha?

zagarinojo

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2020
Posts
2,622
Reaction score
2,846
Jamii Forums tena. Sidhani kama ukweli juu ya maisha yalivyo ulishawahi patikana.

Je, maisha ni magumu kama wengi wasemavyo au ni rahisi Kama wachache waliofanikiwa wasemavyo? Kuna utatanishi mkuu juu ya majibu ya maswali haya.

Nimejaribu kutafakari kwa kina kama furaha katika maisha hutafutwa au hutokea yenyewe tu bila jitihada. Wakati mwingine nashindwa kuelewa nini chanzo cha furaha maishani.

Je ni fedha ulizonazo, wazazi ulionao au elimu uliyonayo au vitu unavyomiliki. Tunaishi kwenye dunia ambayo furaha haipo tena.

Tafiti mbalimbali kutoka vyanzo tofauti zinaonesha asilimia 70%wafanyakazi duniani wanafanya kazi wasizozipenda.

Si hivyo tu hakuna furaha katika ndoa, hakuna haki katika mahakama, hakuna furaha katika nyumbani zetu. Kila mtu anafanya kitu ajione juu zaidi ya mwingine. Lawama zinaongezeka.

Narejea mada yangu. Je, nini kifanyike ili upendo na furaha vitawale maishani? Nini hutukosesha furaha maishani?
 
Furaha ni kile unachokipenda ukakipata lakini baada ya kukizoea unaona kawaida hakikupi tena ile furaha kama mwanzo.
 
Ushindi wa CCM ndio unaninyima furaha.[emoji20][emoji20][emoji20][emoji20][emoji20]
 
Kila nikitafuta jibu mshale unaangukia kwenye pesa. Ngoja nikizipata labda matokeo yatakuwa tofauti.
Nisije weka porojo hapa nikawa mnafki.
 
Amani ndio hunipa furaha, hasa amani ya moyo.
Yaani niamke niwe mzima, nipate mlo, habari mbaya zisinijie, nisikwaruzane na mtu(ikitokea ni msamehee). Hapo lazima niwe nafuraha.

Pia i don't take things seriously, minding my own bznez na zaidi sana siwi mtu wa kuwaza sana jambo

Vitu huninyima furaha
1.kukosa usingizi
2.kudownload game 16gb alaf kwenye ku install nikute ipo corrupted.
 
Back
Top Bottom