Nini hupelekea kuwa na idadi kubwa ya stock exchange?

Drone Camera

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2017
Posts
14,041
Reaction score
13,907
Wakuu,

Natumai mnaendelea vyema na mapambano dhidi ya kirusi huyu.Mungu atusaidie tulishinde hili jaribu.

Mimi ni mdau mzuri katika ufuatiliaji wa mambo ya uchumi.Napenda sana mambo ya uchumi. Japo sijasomea wala si mtaalamu huko.

Swali langu ni kuwa: Kwanini baadhi ya nchi zinakuwa na Stock Exchange zaidi ya moja? Mfano South Africa nafahamu tatu,na nchi kama Marekani wanazo nyingi nyingi hata nadhani nyingine zipo ndani ya mji mmoja..je,ni nini sababu nyuma ya hili? Au ni idadi kubwa ya makampuni?

Vipi Tz hatuwezi kuwa na Stock Exchange nyingine hata tukaiweka kwenye mji mwingine mkubwa? Halafu pia je,nchi zote duniani zina masoko ya hisa au kuna ambazo hazina?

Swali la mwisho,Naomba kujuzwa sababu zinazopelekea hisa za kampuni fulani kushuka au kupanda.

Karibuni wachumi.
 
Simply ni uchumi tu especially nchi ambayo ina export sana kuliko ku import (debit and credit ya export minus import) inaitwa BOP (balance of payment ) au sometimes balance of trade.

Assumption ni kwamba ukiwa unauza sana nje utajipatia fedha za kigeni nyingi (foreign reserve)

Pili ni issue ya demand and supply ya fedha ya nchi husika .kama mahitaji ya fedha yako ni makubwa inakua na value kubwa kwenye ku exchange
 
Shukrani boss vipi kwenye swala la hisa
 
Wachumi mje basi huku; Paula Paul RRONDO The Monk , Na wengine mliokuwako ule uzi wa mafuta...Mnaweza kuwa na idea.

Mkubwa kwanza nitake radhi, umeniweka kundi moja na wahadhiri wangu, siku ile nilipigwa desa.

Wakati wakufunzi wanaandaa nondo, hapo kwenye hisa za makampuni kupanda na kushuka naweza kupangusa vumbi kidogo kuandaa mazingira ya wakubwa zangu waje kushusha somo.

Kama ilivyo ada, bei za hisa za kampuni yeyote zinategemea mambo mengi ikiwepo uimara wa uongozi wa kampuni, utulivu wa hali ya kisiasa kwenye nchi ilipo kampuni husika, kujiendesha kwa faida n.k

Kampuni inapokua na hayo mazingira mazuri, watu wananunua hisa kwa wingi, uhitaji unspokua mkubwa inaziongezea thamani.
Hali kadhalika ikitokea kashfa au hitilafu kwa kampuni utaona watu wanakosa imani ma pesa zao wanaamua kuuza hisa kuepuka kupoteza zaidi.

Lakini pia hali ya uchumi wa nchi au vita, majanga yanayoathiri uchumi wa nchi moja kwa moja yakitokea nchi iliyopo kampuni hata kama wanahisa wako nchi zingine waanza kuuza hisa zao kwa wingi.

Ndio maana kwa wenzetu kashfa ndogo inaweza kuigharim sana kampuni kwa jinsi watu wanavyoichukulia.
 
Shukrani mkuu nimekuelewa vyema hicho kipengele...Mimi nakuona profesa kabisa mkuu😎
 
Nafikiri post inauliza wingi wa stock exchanges, kama vile USA kuna NASDAQ, NYSE, etc wakati kwetu kuna DSE pekee.
Au sijaelewa swali?
 
Wachumi njooni basi tunahitaji majibu mengi mengi.
 
Mimi sio mchumi, lakini ninavyojua Stock Exchange ni soko tu kama lilivyo Kariakoo au Kisutu, sema wao hawauzi nyanya wanauza financial products kama shares, bonds etc.

Kwa wenzetu, haya masoko ni private entities, kinachosababisha kuwa mengi au machache ni market forces. It's possible hata leo likaanzishwa jipya.
 
Back
Top Bottom