Nini husababisha gari kutoa moshi mwingi sana wakati wa kuwasha?

ighaghe

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2013
Posts
2,286
Reaction score
3,203
Wakuu,

Nini kinaweza sababisha gari kutoa moshi mwingi wakati unawasha gari? Hili tatizo limeanza karibuni, haikuwa na hiyo Tabia, moshi ni mwingi sana huwezi kupaki ukaja kuwasha mbele ya watu. Itakuaibisha maana utadhani inaungua. Ukianza kuendesha unaisha au unabaki kidogo. Moshi ni mweupe.

Gari ni ya petrol, v6 ingine.
 
Huenda valve seal mkuu zimeenda kwao waone wataalamu
 
Huenda valve seal mkuu zimeenda kwao waone wataalamu
Shukran sana. Nilitaka mwanga tu maana wataalam hawachelewi kukuambia agiza engine.
 
Inawezekana uwiano wa hewa na mafuta yasiwe sawa...

Au oil inachanganyikana na petrol au diesel.. Hapo seal zinaweza kuwa zimeharibika
 
Inawezekana uwiano wa hewa na mafuta yasiwe sawa...

Au oil inachanganyikana na petrol au diesel.. Hapo seal zinaweza kuwa zimeharibika
Asante kwa hint mkuu.
 
Oil itakuwa inaingia kwenye combustion chamber. Ama Piston rings zimeisha.
 
Oil itakuwa inaingia kwenye combustion chamber. Ama Piston rings zimeisha.
Shukran mkuu. Ninapanga kumpa fundi kesho ss nlitaka kupata hint ili nifananishe na atakachonieleza.
 
Yaa, nguvu ipo na haina miss
Mara nyingi inakuwa hivyo kama valve seal zimechoka unakuta gari inawaka inatoa moshi kama inatumia makaa ya mawe asbh na baada ya hapo hukata au na hata nyakati za mchana hutoa moshi mwembamba,na ikiwa ring zimechoka utaona moshi karibu muda wote gari ikiwa on na pia nguvu hupungua na hata oil kuiona nyuma ya bomba la moshi pia hupunguza level ya oil wacheki hizo seal kwanza kabla ya ring.
 
Yaani hii ndo tabia yake asubuhi. Asante sana.
 
Wazee slow down

Gari haina shida ni mvuke tu

Gari ilioua valve seal na Piston rings moshi mweusi mwingi unatoka time to time au full time kutokana na uchakavu wa izo valve seal na piston rings

Gari ilioua cylinder head gasket utaona moshi Mweupe.. kabisah mwingi na hauachi kutoka

Na hayo matatizo gari itakosa nguvu na itakuwa na miss na itakuwa unakula mafuta sanah kutokana na auna ya tatizo

Maelezo ya jamaa ni mvuke tu wa kawaida

Utaenda haribu gari bure kwa mafundi mtaani

Chill mzee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…