Nini husababisha hofu,wasiwasi na mashaka kwa mtu

Ba E's

Senior Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
145
Reaction score
52
Nimekuwa nikisumbuliwa sana na hili tatizo la hofu,mashaka,wasiwasi na uoga kiasi kwamba siwezi kabisa kusimama na kutoa maelezo au kuelezea kitu mbele ya watu hata wakiwa kumi tu lakini km ni stori naweza kuongea vizuri na mpaka kuchekesha wenzangu, naweza nikawa na points za kutosha tu kuelimisha juu ya jambo fulani tatizo sina confidence kabisa, kwa kweli najisikia vibaya sana siwezi wakati mwingine hata kuchangia niwapo kwenye group discussion presentation ndo kabisa mwili wote utatokwa jasho na harufu fulani ya uoga na kuongea kwa kutetemeka. Nahitaji sana michango yenu ya kiushauri ili nami niwe na furaha hapa chuoni, niko chuo cha SUA nasomea uhandisi wa kilimo(bachelor of science in agricultural engineering)
 
Naamini jf ni combination ya wataalam wa kila aina so ushauri wenu na uzoefu wenu ktk maisha utanisaidia, njia au taratibu zozote naweza kuzifuata ili tatizo hili litoweke, nina mpango wa kuwa politician sasa kwa hali hii si nitaanguka jukwaani kwa uoga!
 
Pole mkuu.
Fanya mazoezi ya viungo kila siku/au kwa wiki,hii itasaidia mzungoka wa damu mwilini na kiwango cha utulivu(calmness )kitaongezeka.
Pia soma vitabu vya saikolojia na vya Sanaa ya kuzungumza katika umma(the art of public speaking)vitasaidia pia.
Angalia pia mavazi yako tafuta nguo itakayokufanya upendeze itaongeza kujiamini(na hapa napendeka mavazi yale yanayoitwa ya kiofisi,)look smart kiasi upite kwa watu wakutizame(don't get me wrong hapa lakini itasaidia,tahadhari ukivaa watu wakakuangalia sana kuna mawili either umependeza sana au kinyume chake kuwa makini hapa,namna ya kuvaa accordingly utagoole na utaona na baadhi yamagazi wanaelezea haya mambo,mf mwananchi jpili).
Nimalizie hivi.
Kujiamini (confidence)kunaathiriwa kwa kiasi kikubwa sana na aibu,mtu mwenye haya,soni ni vigumu kujiamini,lakini pia kwa mtu mwenye kigugumizi,unapokuwa unazungumza jitahidi kutazamana na unaoongea nao(maintain eye to eye contac) ni ngumu lakini jilazimishe itakuwa rahisi kadri unavyoendelea,kama una kigugumizi jitahidi kuzungumza kwa upole bila haraka.
Hayo yote niliyosema hapo juu yanaweza kufupishwa kwa namna hii hapa chini:-

Kujiamini(confidence)= na self esteem (Hali ya kujiona wa thamani)+ self efficacy (hali ya kujiona unaweza,sababu unaweza)
All the best .
 
Ahsante sana kaka kwa ushauri nitaufanyia kazi Kuhusu hizo sababu mbili yaani kuwa na aibu au soni na kuwa na kigugumizi, kiukweli nina aibu sana kigugumizi sina ila huwa inanitokea wakati naongea mbele ya watu maneno huonekana km yanapandiliana i mean maneno mawili yanataka kutoka kwa wakati mmoja hii hali huwa inaninyima raha sana!
 
Pole sana! tatizo lako linajulikana kama inferiority complex, huu ni ugonjwa moyoni, inaonekana ni mtu unaejisema sana, unajichukia kwa ndani, hujikubali na ni mtu asiye na hakika na anachokifanya, hiyo siyo aibu, ni matokeo ya kujiona huwezi kufanya/kusema kitu watu wakakikubali, inawezekana wakati uko mdogo ulikuwa unakaripiwa sana wakati unaongea au kufanya jambo fulani! hivyo jione kuwa wewe ni mtu wa pekee sana na kwamba unaweza, na ujipende pia! hii ndio tiba ya tatizo lako.
 

Ahsante kwa ushauri, kiukweli mimi ni yatima wazazi wangu walifariki kwa nyakati tofauti mama na baba pia hawakuwa pamoja hvyo mama ckuwahi kuishi naye hata wiki moja ukiondoa maisha ya kunyonya kwa hiyo nimekulia kwny mikono ya watu wasio wazazi wangu, kimsingi watu ambao hawajakuzaa huwa hawana machungu na wakati mwingine huchukulia kuwa hutakuwa na mafanikio yoyote ukubwani hivyo utakuwa ktk mazingira ya uwoga huenda kweli na hilo limeniathiri nitajitahidi kufuata ushauri wako.
 
 
jaribu kusoma vitabu ving vinavyoeleza namna ya kuondokana na uoga , kutojiamin ,na ufanyie kazi ushauri unaotolewa . . Pia uwe na desturi ya kufanya mazoezi ya viungo . Hata hivyo anza kuchangia wakati wa discusion ,na ujitahidi kujibu maswali au kuuliza hata yale mafupi mafupi ili kujipa mazoezi ili uondokane na adha hiyo . Kiukweli unahitaji jitihada ya dhati kwani hakuna atakaye kuwezesha mia kwa mia bali ni wewe mwenyewe . .
 
wakati unapotaka kuongea mbele ya watu kwa darasa wakati wa presentation au debate vuta pumzi harafu uibane kwa sekunde kadhaa harafu uitoe taratibu taratibu fanya hivyn Kama mara tano hivi harafu uni-PM uniambie unajisikiaje! pia jitahidi kupata muda wa kukimbia mchakamchaka hasa nyakati za asubuhi.
 

Ahsante kaka wisest man uliuliza pia khs umri, kaka nina miaka mingi ni 28 yrs ndg lkn tatizo ndo hilo nashukuru sana kwa ushauri murua kabisa naamini utanisaidia huwa siamini sana kwenda kwa masangoma ila hili tatizo huwa linanifanya nifikiri hivyo. Kuhusu kuku PM natumia simu kwa hiyo sijui naomba unipe maelekezo kaka samahani kwa kukusumbua lakini.
 
Usijali mkuu! PM humaanisha private message hivyo ukitaka kuwasiliana na yeyote humu jukwaani kwa mambo binafsi una-click user name ya huyo mtu then utaona neno profile yake na chini yake utaona 'sending message' i-click hiyo sehemu then utaona neno 'private message' ambayo ndio PM yenyewe! hii unaweza kuitumia kutoa mawasiliano yako kama phone no.,email nk. nadhani umenielewa mkuu.
 
Ahsante wakuu wote kwa msaada naona mabadiliko kidogo yanakuja maana ilikuwa ukiwa discussion au debate akinyosha mkono hata mtu uliyenaye jirani tayari ninapanic kana kwamba zamu yangu ya kuongea ndo itakayofuata, kwa sasa siogopi kihivyo ndg wisest man nitaku pm kesho nitajiunga dk za kutosha ili 2ongee, usiku mwema wataalam wangu!
 

Nawe pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…