Nimekuwa nikisumbuliwa sana na hili tatizo la hofu,mashaka,wasiwasi na uoga kiasi kwamba siwezi kabisa kusimama na kutoa maelezo au kuelezea kitu mbele ya watu hata wakiwa kumi tu lakini km ni stori naweza kuongea vizuri na mpaka kuchekesha wenzangu, naweza nikawa na points za kutosha tu kuelimisha juu ya jambo fulani tatizo sina confidence kabisa, kwa kweli najisikia vibaya sana siwezi wakati mwingine hata kuchangia niwapo kwenye group discussion presentation ndo kabisa mwili wote utatokwa jasho na harufu fulani ya uoga na kuongea kwa kutetemeka. Nahitaji sana michango yenu ya kiushauri ili nami niwe na furaha hapa chuoni, niko chuo cha SUA nasomea uhandisi wa kilimo(bachelor of science in agricultural engineering)