Nini husababisha mtu kula meno usiku

Nini husababisha mtu kula meno usiku

LA7

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2019
Posts
655
Reaction score
2,369
Mwanangu wa miaka miwili usiku tukiwa tumelala akiwa usingizini huanza kusugua meno yanatoa sauti ya kukera sana.

Mchana akiwa amelala usingizi huwa hafanyi hivo.

Je, ni nini husababisha?
 
mwanangu wa miaka miwili usiku tukiwa tumelala akiwa usingizini huanza kusugua meno yanatoa sauti ya kukera sana

mchana akiwa amelala usingizi huwa hafanyi hivo

je ni nini husababisha.
Mapepo majini au mizimu mikali ya baba yake
 
Anatumika kichawi! Mpeleke kwenye maombi usipuzie kabisa mkuu!! Huwa sio yye mwili wake unatumika bila yeye kujua ndo maana hicho kitendo hufanyika usiku
 
Tatizo la kusugua meno, linalojulikana pia kama bruxism, linaweza kujumuisha:

  • Uharibifu wa Meno: Kusugua kupita kiasi kunaweza kusababisha meno kuvunjika, kupasuka, au kuharibika.
  • Maumivu ya Taya: Inaweza kusababisha maumivu na usumbufu katika misuli na viungo vya taya.
  • Maumivu ya Kichwa: Maumivu ya kichwa ya mara kwa mara, hasa kwenye paji la uso, yanaweza kuwa matokeo.
  • Ugonjwa wa Meno: Kusugua kunaweza kuchakaza enameli, na kusababisha meno kuwa na hisia kali kwa moto na baridi.
  • Usumbufu wa Usingizi: Inaweza kuvuruga usingizi wako pamoja na wa mwenzi wako.

Ni muhimu kushauriana na daktari wa meno ikiwa unashuku una bruxism ili kuzuia uharibifu wa muda mrefu na kushughulikia sababu za msingi.
 
Anakuwa anamalizia chakula alichobakisha kwenye fizi
 
Anatumika kichawi! Mpeleke kwenye maombi usipuzie kabisa mkuu!! Huwa sio yye mwili wake unatumika bila yeye kujua ndo maana hicho kitendo hufanyika usiku
Acha ujinga.
MiAfrika ndivyo ilivyo kila kitu uchawi.
Pumbafffff.
 
mwanangu wa miaka miwili usiku tukiwa tumelala akiwa usingizini huanza kusugua meno yanatoa sauti ya kukera sana

mchana akiwa amelala usingizi huwa hafanyi hivo

je ni nini husababisha.
Mizimu anaisaidia kupiga misosi ya mifupa
 
Back
Top Bottom