Nini husababisha mwanamke kutoa damu nyingi wakati wa hedhi?

Nini husababisha mwanamke kutoa damu nyingi wakati wa hedhi?

Miss Natafuta

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2015
Posts
27,031
Reaction score
49,928
1623655902513.png
Naombeni kuuliza ,ni nini kinasababisha mwanamke wa umri wa makamo
34_37 ,hajawai pia kuzaa,kutoa damu nyiingi nyingi sana wakati wa hedhi? Yaani ni nyingi kiasi cha kuvaa pedi kila baada ya lisaa.
===
UFAFANUZI WA KINA WA TATIZO LA KUTOKWA NA DAMU NYINGI WAKATI WA HEDHI
Zababu zinazosababisha kutokwa damu nyingi ya hedhi.

Zifuatazo ni baadhi ya sababu kuu ambazo husababisha tatizo la kutokwa damu nyingi kuliko kawaida wakati wa hedhi.

Mabadiliko ya homoni
Kwa baadhi ya wanawake ambao hupata tatizo hili bila kuathirika kwa mpangilio wa mzunguko wao basi hii ni moja ya sababu kubwa. Mabadiliko haya yanaweza kusababishwa na msongo wa mawazo (stress), matumizi ya dawa, uzito mkubwa na mazoezi mazito.

Wanawake wengi wenye tatizo hili wameonekana kuwa na kiwango kikubwa cha homoni ya oestrogen ambayo hupelekea kuzalishwa kwa prostaglandins kwa wingi.

Prostaglandins ni kemikali ambazo husababisha mishipa yad amu kutanuka vilevile kupunguza uzito wa damu.

Jambo hili hupelekea damu kutoka kwa urahisi na kwa wingi.

Uvimbe katika mfuko wa uzazi
Uvimbe wa kawaida ambao sio wa saratani katika mfuko wa uzazi ni moja ya sababu za kutokwa damu nyingi wakati wa hedhi.

mara nyingi uvimbe huu hutokea katika misuli iliyounda kuta za mfuko huu, na huwaathiri zaidi wanawake wenye umri wa zaidi ya miaka 30.

Uvimbe huu unaweza kuonekana kwa kipimo cha mwangwi wa sauti (ultrasound). Na unaweza kuonyesha dalili au usionyeshe.

Ikiwa utaonyesha dalili basi zifuatao ni dalili muhimu ambazo huashiria uwepo wa uvimbe katika mfuko wa uzazi.

Kukojoa mara kwa mara
Maumivu chini ya kitovu.
Tumbo kujaa mithiri ya mjamzito.
Kuhisi mkandamizo chini ya kitovu.
Mimba kuharibika mara kwa mara.
Ukuaji wa seli za mfuko wa uzazi usio wa kawaida.
Kuna wakati seli zinazounda ukuta wa mfuko wa uzazi huweza kukua bila uthibiti na kusababisha uvimbe mgumu.

Uvimbe huu unaweza ukakua na kugeuka kuwa seli za saratani.

Ukuaji wa seli za mfuko wa uzazi sehemu isiyo sahihi.
Hii hujitokeza ikiwa seli za kawaida za ukuta wa mfuko wa uzazi zinakuwa mahali ambapo si sahihi.

Seli hii huendelea kuthibitiwa na homoni za uzazi na kipindi cha hedhi nazo hutolewa nje kama damu hivyo kiwango cha damu kuongezeka.

Ukuaji wa seli wa namna hii unaweza kutokea sehemu nyinezo za mfumo wa uzazi kama vile ovari, milija ya falopia, kibofu na shingo ya kizazi.

Mbali na tatizo hili kusababisha damu nyingi kutoka vilevile huambatana na maumivu makali; Kuharibu mpangilio wa hedhi na wakati mwingine husababisha ugumba.

Maradhi ya uvimbe katika via vya uzazi (PID)
Haya ni maradhi ambayo husababishwa na maambukizi ya bakteria ambao husambaa kwa njia ya kujamiana au njia nyinginezo.

Kwa wanawake hawa damu nyingi wakati wa hedhi huambatana na

Kutokuwapo kwa mpangilio wa mzunguko wa hedhi.

Homa kali
Mwili kuchoka kupita kawaida.
Uchafu au ute wenye harufu kali ikiwa PID imesababishwa na gonorrhoea.
Matumizi njia za vitanzi katika kupanga uzazi.
Kwa sasa ni wanawake wachache sana amabao hutumia njia za asili za kupanga uzazi.

Pengine ni kutokana na woga na wasiwasi wa ufanisi wa njia hizi za asili.

Kwa sasa wimbi kubwa la wanawake hutumia njia za kisasa za kupanga uzazi kama vile sindano, vidonge, vijiti na vitanzi.

Mbali na faida za kutumia njia hizi lakini njia hizi pia ni moja ya vyanzo vikuu vya matatizo mbalimbali ya mzunguko wa hedhi.

Njia ya kitanzi ni moja ya sababu kuu za kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi kwa sababu ya mabadiliko makubwa ya homoni yanayotokea.

Hali huwa mbaya zaidi katika hatua za mwanzo za kutumia njia hii na wakati mwingine madhara makubwa huweza kutokea ikiwa kitanzi kimekaa vibaya.

Upungufu wa lishe
Upungufu wa lishe mwilini ni chanzo mojawapo cha kutoka damu nyingi kupita kawaida.

Kupungua kwa madini joto ya chuma husababisha ugonjwa wa kutokwa damu.

Ikiwa mwanamke atakuwa na upungufu wa madini haya basi inaweza kuwa ni hatari zaidi kwa afya yake.

Magonjwa mbalimbali
Magonjwa kama anemia (damu kushindwa kuganda), von Willebrand (upungufu wa kemikali ya factor x ambayo husaidia damu kuganda.

Yote haya ni magonjwa hatari kwa vile husababisha damu kutoka bila kuganda kwa muda mrefu.

Vilevile maradhi katika ini yanaweza kuwa chanzo cha kupata hedhi yenye damu nyingi kupita kawaida.

Hii ni kutokana na umuhimu w aini katika kutengeneza kemikali zinazosaidia damu kuganda.

Hivyo kuathirika kwa ini na uzalishaji wa kemikali hizi huathirika pia kuharibika kwa mimba. Wakati mwingine mwanamke hupata hedhi yenye damu nyingi ikiwa mimba imeharibika ama kwa kukusudia au bila kukusudia.

USHAURI ULIOTOLEWA NA MDAU WA JF

Kwa kawaida mzunguko wa hedhi huchukua siku 21 mpaka 35, na mwanamke huingia kwenye hedhi kwa muda wa siku 3 mpaka 7. Mwanamke anapata hedhi ndefu au kwa muda mrefu zaidi kama akiingia kwenye hedhi kwa zaidi ya siku 7. Hali hii huitwa menorrhagiakwa kitaalamu. Hali hii inaweza kuambatana na kupata damu nyingi ya hedhi.

Sababu

Sababu zifuatazo zinasababisha hedhi kuwa ndefu zaidi ya kawaida;

Mabadiliko ya homoni hasa istrojeni na projestoni.Sindano za kuzuia mimbaMimba kutokaVitanzi vya kuzuia mimba (Intrauterine Contraceptive Devices)Endometrial hyperplasiaMaambukizi ya Via vya uzazi vya ndani (Pelvic Inflammatory Disease – PID)Vivimbe kwenye ukuta wa mji wa uzazi (endometrial polyps)Mabonge kwenye mji wa mimba (uterine fibroids)Saratani ya mji wa uzazi

Madhara
Kupata hedhi kwa muda mrefu kunaleta madhara ya kiafya na kijamii kwa mwanamke. Kijamii anaweza akashindwa kufanya shughuli zake vizuri na hata kuleta mgogoro katika mahusiano.

Kiafya anaweza kupata upungufu wa damu kutokana na kupoteza damu nyingi. Anaweza kupata dalili za kichwa kuuma, mwili kuchoka, mapigo ya moyo kwenda mbio.

Matibabu
Onana na daktari wako mara unapoona unapata shida hii. Matibabu hutegemea na sababu ya ugonjwa na yanaweza kujumisha njia zifuatazo;

Dawa za kupunguza maumivuVidonge vya homoniKitanzi chenye homoniKusafisha mji wa uzazi (Dilatation and Curretage)Kuundoa kizazi hasa kama kuna saratani au mabonge ya kizazi.
 
Naombeni kuuliza ,ni nini kinasababisha mwanamke wa umri wa makamo
34_37 ,hajawai pia kuzaa,kutoa damu nyiingi nyingi sana wakati wa hedhi ? Yaani ni nyingi kiasi cha kuvaa pedi kila baada ya lisaa

Kwa kawaida mzunguko wa hedhi huchukua siku 21 mpaka 35, na mwanamke huingia kwenye hedhi kwa muda wa siku 3 mpaka 7. Mwanamke anapata hedhi ndefu au kwa muda mrefu zaidi kama akiingia kwenye hedhi kwa zaidi ya siku 7. Hali hii huitwa menorrhagiakwa kitaalamu. Hali hii inaweza kuambatana na kupata damu nyingi ya hedhi...
Asante kwa ufafanuzi.ila swala sio kupata hedhi kwa muda mrefu Mkuu.

Muda ni siku tano ila damu nyiiingi sana
 
Asante kwa ufafanuzi.ila swala sio kupata hedhi kwa muda mrefu Mkuu
Muda ni siku tano ila damu nyiiingi sana
Mkuu, tatizo hilo linaitwa menorrhagia.
Nivizuri mwenye tatizo hilo amuone Daktari, kwasababu hiyo ni dalili mbaya
 
Naombeni kuuliza ,ni nini kinasababisha mwanamke wa umri wa makamo
34_37 ,hajawai pia kuzaa,kutoa damu nyiingi nyingi sana wakati wa hedhi ? Yaani ni nyingi kiasi cha kuvaa pedi kila baada ya lisaa
Miaka 37 hujazaa utazaa lini madam?
 
Naombeni kuuliza ,ni nini kinasababisha mwanamke wa umri wa makamo
34_37 ,hajawai pia kuzaa,kutoa damu nyiingi nyingi sana wakati wa hedhi ? Yaani ni nyingi kiasi cha kuvaa pedi kila baada ya lisaa
Habari.

Swali lako limelenga hasa kujua sababu za mtu kutokwa na damu kwa wingi wakati wa siku zake (Hedhi).

Jibu ni Kama ifuatavyo; zipo sababu nyingi sana zinazopeleka tatizo la Mwanamke kutokwa na damu kwa wingi wakati wa hedhi (tatizo ambalo kitaalamu linajulikana kama Menorrhagia), sababu hizo ni pamoja na;

1.Hormone Imbalance... inapotokea uzalishwaji wa vichocheo/hormone aina ya Estrogen na Progesterone hauko kwenye uwiano sawia basi tatizo la kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi huweza kutokea.

2. Matumizi ya njia za uzazi wa mpango kama VITANZI.

3.Saratani hasa ya Kizazi.

4.Ovary hambazo hazifanyi kazi (Kwenye swali pia umeeleza pia kuwa huyo mgonjwa hajabahatika kupata mtoto, yawezekana kabisa Ovary zake zikawa zina matatizo na ndio maana anatokwa na damu nyingi na pia hajafanikiwa kuwa na mtoto bado)

Asante na Karibu. #AfyaKliniki
 
Back
Top Bottom