Nini husababisha wanawake kuwa wabinafsi kwenye mali

Kuna mambo mengi ndugu mdau,
1. Bado kuna mume kufariki ghafla, na ukute hajaacha wosia ndugu zake wakang'ang'ana mali za marehemu. Japo kuna sheria za mirathi, imagine mwanamke huna pakuangukia yeye na vifaranga vyake

2. Kuna suala zima la mume kutapanya mali kwa michepuko, watoto wa nje na wahuni huko nje. Mume hashauriki kwanini mwanamke asijiongeze kuinusuru kesho yake yeye na watoto. Wacha tu afiche

Hizi ni baadhi tu ya sababu
 
Asikwambie mtu mkuu, dunia imebadilika sana, mwanamke akiwa na kitu zama hizi hiyo ndoa ina 80% ya kuvunjika, itokee neema ya Mungu tu. Ubinafsi, tamaa, ujeuri, ujuaji vyote hivi havikosekani ndani ya ndoa ambayo mwanamke pia ana kipato.
 
Mkuu unajua hii yote inatokana na zana kwamba ego ya mwanaume ni uchumi alionao, ndio maana anauliza kama kwanza unakwanja maana kwao ni rahisi kuheshimu ukiwa na pesa.. Na Sio lazima kupenda, sasa wao wakiwa na huo uchumi wanaona Ile ego inayokupa haki ya kumtawala ndio iko kwao .. Wewe ndio jukumu lako uheshimu... Ingawa si wanawake wote hufanya hivi ila wengi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…