Hili swali huwa linanishangaza sana! Muhindi ana zaidi hata ya miaka 30 au amezaliwa na kuzeekea hapa ila kuongea kiswahili kwa ufasaha ni shida kubwa.
Ila wazungu wanaokuja kwenye miradi au shughuli zingine kwa miaka mitano tu eneo analofanyia kazi ataijua lugha hiyo kwa muda mfupi, hata kama hapo zinatumiwa lugha zaidi ya moja zote atazijua na kuongea vizuri. Ila wahindi wengi wako mjini tena wana maduka makubwa yaani tunaingiliana sana kupitia biashara lakini kiswahili kwao ni shida.
Je, wewe unaona nini hupelekea hili?
Mkuu lazima uelewe wahindi so kama hawajuwi kiswahili vzr.
Ile ni lafidhi yao sababu ya kupenda kutojichanganya na watu makabila mengine.
Muhindi atasoma shule ya wahindi,,
Akirudi atakwenda dukani kukaa na family yake nayo itaongea kiswahili cha lafidhi ile,.
Akienda misikiti yao ni kiswahili hicho hicho,,
.atawezaje kujuwa kiswahili fasaha?
Nenda kakutane na wahindi wa mburahati,,au manzese..daresalam.
Huwezijuwa kama ni muhindi,,
Kiswahili kimenyooka kabisa.
Chukulia mfano mtu wa kabila fulan,,
Mfano tanga,
unaweza ukakutana nae yupo mji mwingine ,,
lakini lafidhi ya kiswahili chake kinaweza kisibadilike kama ataendelea kuwa na watanga wenzie..
Au hata warangi,nk
Kuna watu wapo ulaya au wana miaka zaidi ya 20 hawajarudi Tanzania,,
Lakini ukisikia kiswahili chake hukwepi,,kujuwa kama huyu ni tanga line.
Sababu ya kuendelea na kuishi na wenzio wale wale,
Lafidhi haibadiliki hata kidogo.
Wazungu wanajichanganya uswahilini.