Oil hiyo inavuja kutoka kwenye cylinder head ndiyo maana ifunika cylnder head yote. Ni vigumu kukupa diagnosis kamili bila kuikagua injini wakati inaunguruma. Hata hivyo hizo injini za VVT-i zina oil control valves ama moja au mbili juu ya cylinder head, moja ikiwa kulia na nyingine kushoto. Wasiwasi wangu ni kuwa o-rings za hizo oil control valves hizo zimekauka hivyo hazibani sawasawa na kuasababisha oil ivuje juu ya cylinder. Ama sivyo valve zenyewe ndizo zimekufa zinarudisha oil nyuma na kuivujisha kwenye cylnder head.
Kagua hizo valves ikiwezekana ubadilishe valve nzima siyo o-rings tu. Picha ulizoweka hazionyeshi sawasawa kwe vile zimechukuliwa upande mmoja tu wa injini ambapo sijui kama ni kulia au kushoto. Ingekuwa vizuri kama ningeona kutokea pande zote mbili: kulia na kushoto. Sasa hivi shughulika na hizo oil control valves tu, tena upate genuine kwani ukipata aftermarket zinaweza zisilingane sawasawa na tundu la kwenye injini na kusababisha uvujaji uendelee.