Nini kifanyike ili tren ya SGR isife!??

Hivi hakuna watanzania wanaoweza kusomeshwa na serikali wakafanya hiyo kazi badala ya kila kitu kufanywa na mwekezaji? Anachokifanya huyo mwekezaji kifanywe na watendaji wa serikali, kama waliopo wana mapungufu ya kitaaluma basi wapelekwe wakasome
Issue si watendaji issue ni mifumo.
 
Kwanza ufanyike upigaji, ili kutengeneza sababu za ubinafsishaji.
 
kama ilivyokua kwa mwendokasi basi SGR pia jambo ni lile lile- NAULI NI NDOGO SANA
 
Umeme na SGR ni uti wa mgongo kwa walalahoi,mabasi yameua sana maskini Ile basi ya Ally's iliyogonga treni iliua mwanetu aliekuwa Bugando doctorate na wala hata mtoto hakuwanae,nikiwa sehemu nikiiona Ile bus inatia uchungu sana.hebu tumikieni miradi hii miwili idumu,Barabara ni nyembamba,na hazina double lane.
 
Kama SGR inaenda tupu huku tickets zikiwa zimeisha ni red flags kwambwa CARTEL wapo kazini.
 
Kati ya mwaka 1994 na 1997 serikali ya China ilinunua treni chache sana kutoka Ufaransa, Ujerumani na Japan. Ikazifanyia reverse engineering na baada ya miaka 10 ikawa inategeneza treni zake yenyewe. Leo hii China ndiyo inayoongoza kwa wingi wa treni za mwendo kasi duniani. Treni zote za China zinaendeshwa na mashirika ya kiserikali, hakuna kinachoitwa mwekezaji labda subcontractors wa hayo mashirika. Hivi watanzania sisi tumerogwa wapi kudhani kuwa matatizo yetu yatatuliwa na wawekezaji? Neno wawekezaji nimelisikia sasa mwaka wa 29 tangu utawala wa Mkapa na matatizo hayajaisha lakini bado tunataka tutafute mwekezaji mwingine.

Kinachotakiwa ni usimamizi wenye adhabu kali kwa wanaopewa kuendesha mashirika hayo. China ukivurunda mali ya umma unahyongwa!
 
Prof assad ni fisadi na mla rushwa mzuri tu ni vile hujafanya naye kazi,inshu hapa waingie wawekezaji tu serikali ikae pembeni vinginevyo ya mwendokasi yanatufuata siku sio nyingi.
 
Shida yetu majizi na mafisadi ya ccm yanalindana sana na hayawezi kuwajibishana we huoni tu hata kwenye teuzi na tenguzi akivurunda sehemu a anahamishiwa sehemu b,kimsingi katiba hii na serikali ya ccm hii kila mradi wa umma lazima utafeli tu.
 
Mkono mtupu haulambwi
Halafu walishazoea
Nchi ya kitu kidogo
 
Wewe ndiyo umeongea point
Inatakiwa adhabu kali ukiharibu mali ya umma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…