Nini kifanyike kuboresha mtaala wa elimu

HALANGA

New Member
Joined
Jan 21, 2021
Posts
2
Reaction score
2
Wadau bado kuna ufahamu mdogo nini kifanyike kuboresha mtaala wa elimu.

1. Kuandaa vijana wetu kwenye mtaala ili washiriki uchumi wa viwanda lazima Sera ya Elimu lazima ibainishe kuwa Shule ni kituo cha kukuza ubunifu.

2. Ili kutekeleza hilo, mtaala utabainisha ufundishaji unakuza na kujenga ujuzi kwa mwanafunzi. Lazima tuelewe kuwa ufundishaji unaokuza na kujenga ujuzi ni zaidi ya kufanya practical mfano kwenye masomo ya Sayansi. Nashangaa kwa nini hili suala halieleweki. HATA ukiwa na vifaa vya kutosha kwenye maabara na kufanya practical bado hatujafikia utatuzi wa tatizo tulilonaloi.

Ufundishaji unaojenga ujuzi unafanyika kukiwa na "both minds on and hands on activities". Baada ya kupata maarifa kutoka kwa Mwalimu kwenye kipindi cha dk 40 au 80. Hadi sasa hakuna ufundishaji unaozingatia kukuza na kujenga ujuzi kwa wanafunzi. Ufundishaji huo ndiyo tunaoutaka kwenye mtaala ambapo kwa watu tuliofanya tafiti za kutosha inaeleweka.

Ni vile sisi wengine tunakosa forum ya kuelezea kwa kina suala hili. Mfano, hata wanafunzi wakifanya practical ukamilishaji wa kukuza na kujenga ujuzi wa kilichosoma kwenye hiyo practical hakija kamilika.

Hii ni lazima tutengeneze pedagogical framework pamoja na assessment framework ambayo kwenye mtaala haipo. Wenzetu wanatumia hiyo pedagogy utaona kuwa Innovation nyingi zinafanywa na watoto kuanzia miaka 14 hadi 25.
 
Sisi hatuwezi tumeshindwa labda kukakopi kwa waliofanikiwa mfano Korea kusini,China,Norway,Canada nk
Au watafutwe wataalamu ( wasitoke au kuwa karibu na chama cha mapinduzi) watoke ngo's ,diasporas, na mataifa yaliyoendelea kama nilivyotaja hapo juuu!!! Asiruhusiwe MTU yeyote mwenye mafungano na CCM mfano Benson Bana ,Bashiru nk
 
Wadau bado kuna ufahamu mdogo nini kifanyike kuboresha mtaala wa elimu.

1. Kuandaa vijana wetu kwenye mtaala ili washiriki uchumi wa viwanda lazima Sera ya Elimu lazima ibainishe kuwa Shule ni kituo cha kukuza ubunifu.

2. Ili kutekeleza hilo, mtaala utabainisha ufundishaji unakuza na kujenga ujuzi kwa mwanafunzi. Lazima tuelewe kuwa ufundishaji unaokuza na kujenga ujuzi ni zaidi ya kufanya practical mfano kwenye masomo ya Sayansi. Nashangaa kwa nini hili suala halieleweki. HATA ukiwa na vifaa vya kutosha kwenye maabara na kufanya practical bado hatujafikia utatuzi wa tatizo tulilonaloi.

Ufundishaji unaojenga ujuzi unafanyika kukiwa na "both minds on and hands on activities". Baada ya kupata maarifa kutoka kwa Mwalimu kwenye kipindi cha dk 40 au 80. Hadi sasa hakuna ufundishaji unaozingatia kukuza na kujenga ujuzi kwa wanafunzi. Ufundishaji huo ndiyo tunaoutaka kwenye mtaala ambapo kwa watu tuliofanya tafiti za kutosha inaeleweka.

Ni vile sisi wengine tunakosa forum ya kuelezea kwa kina suala hili. Mfano, hata wanafunzi wakifanya practical ukamilishaji wa kukuza na kujenga ujuzi wa kilichosoma kwenye hiyo practical hakija kamilika.

Hii ni lazima tutengeneze pedagogical framework pamoja na assessment framework ambayo kwenye mtaala haipo. Wenzetu wanatumia hiyo pedagogy utaona kuwa Innovation nyingi zinafanywa na watoto kuanzia miaka 14 hadi 25.

Safi sana Halanga, nilifikiri Hangai.

Juzi kati nimeona wamepumbaza watu kwa kuwaambia wanakusanya maoni ya mtaala, ila binafsi nilijua ni siasa za maji taka kama walivyofanya kuonjesha watu mambo ya katiba. Sisi watu tuna mzaha sana.

Nini kifanyike inaanzia kwenye mtaala, kwa maana ya Curriculum na Syllabus. Kwanini mtaala, kwasbb mpaka sasa ndio framework yenye mlengo huo.

Dhumuni/malengo;

-kujua kusoma, kuandika, kusikiliza, kuwasilisha, kutenda
-Kutafakari kwa kina na kuzingatia mazingira na historia na kuwa mbunifu
-kuwa dynamic (kunyumbuka kifikra na mtazamo), kutokuwa na akili mgando.
-uwezo wa kujisimamia na kusimamiwa.

Muhimu: mtaala lazima ujibu haya malengo na kutufikisha.

Curriculum;

Hutengenezwa kulingana na uwezo wa rika la wanafunzi.

Umri~darasa~mikakati

Umri

1. Umri wa kukua
(kupata lishe bora na kujikinga na magonjwa) , kupata nishati, kupewa misingi ya awali ya ya kijamii

2. Umri wa kubalehe
Umri kijana anatakiwa athibitiwe katika kazi za mikono, fikra na usimamizi muda. Ni umri, sahihi wa kujituma, wakiwa guided vyema wanauwezo wa kuthibitisha kuwa kijana ndio taifa la kesho.

3. ....

Darasa.

5-6~awali. (Darasa kwa mwaka)
-Kuchangamana na wenzao, kucheza, kufahamiana,
-kujua tabia mbaya na nzuri,
-kumsoma tabia na kuanza kuikuza au kuikemea. n.k

7-10~msingi (darasa kwa mwaka)
-hisabati na historia
-sayansi na mazingira
-biashara (vyanzo vya malighafi, masoko, uhasibu, ukarani)
-kilimo na ufugaji i.e njiwa, panya, maua, ... Mafunzo mafupi.
-sanaa na michezo (ubunifu; kuchora, kuimba, kucheza, kuogelea, kusuka, kushona, KUUNDA, KUTOA kichwani kuweka kionekane.

Hayo yote ya juu yawe kwa kiswahili

11 msingi hitimisho (ujuzi)
mzazi na jamii washirikiane kutimiza kwa matendo mwanafunzi aliyojifunza. Kama ajira ila kujitolea eneo mtoto anapoishi, na kazi ibadilike kila miezi m3

12-13~sekondary msingi (darasa nus mwaka)
Usahili ufanyike kila baada ya miezi 6
Madarasa haya 4 yatakuwa ni kumfundisha basic za kujisimamia na kusimamiwa.

Social
-lishe, virutubisho na kinga mwili
-kujitambua (biology, geography, civics)
-uwasilishaji
-uchambuzi wa mada
-ushirikiano

Financial
-usimamizi fedha (vyanzo vya fedha, njia za uwekezaji, kutunza mali...)
-usimamizi miradi (project management)
-usimamizi watu (hrm)
-ushirikiano (partnerships; misingi yake, usimamizi wa sheria, faida zake, mgawanyo wa majukumu)

Innovative
-ubunifu

14-16~sekondary juu (ubobezi)
-kilimo
-afya
-uchumi
- it
-sheria
- ........

17-.... (Vyuo vya specialisation)
Vyuo vya awali vipewe vipaumbele kwani ndio gurudumu la kujiajiri kwani ajira ni chache na waajiriwa ni wengi.

Kwa kiswahili

Kisha sera za uwezeshaji.
-practical training (paid, lazima(sera yake mahususi/sheria kabisa)
-mikopo (na sera zake kama zote.)

Makala nimeona imekuwa ndefu. Nimejaribu kugusia sehemu ya kwanza. Yapili ikiwa ni uwezeshaji wa wanafunzi wawe kwenye ajira, ya tatu itasimamiwa na sekta ya ajira kwa kusudi la kuweka ajira iwepo na iongezeke.

Kipengele cha mikakati nacho nimeona nikikiweka hapa ntawachosha wasomaji, na hatujazoea kusoma. Labda makala ijayo.

Nashukuru.
 
Ni vyema kila mtoto awe na faili lake na ahame nalo kwaajili ya ufuatiliaji.
Kama ilivyo mahospitalini na daftari la mgonjwa, kanisani na kadi ya michango, n.k
 
Tuchukue ule wa mkoloni ndio sahihi.Huu unawafanya wahitimu kupoteza mda darasani na kuwa masikini
 
Ndio huu wa sasa, umeboreshwa kidogo kukidhi wingi wa watu
Huu ni takataka,unamaliza chuo unakuwa machinga au bodaboda au mama lishe kwann usimalize la saba uingie direct kwenye umachinga au bodaboda kuliko kupoteza mda darasani
 
Wale walikuwa wachache, hivyo ilikuwa rahisi kuwa na uwafadhali.

Hivi sasa kama ukoloni, imegeuka kuwa kama sheria lazma kufika chuo. Io ndio dhamira, kufika chuo. Sio unaenda kufanya nn ila kufika chuo.
 
Mbona ndo unatumika Ulaya hadi sasa
 
Mbona ndo unatumika Ulaya hadi sasa

Naweza sema si kweli.

Kwasababu mtaala wa ugerumani ni tofauti kabisa na wa uingereza. Ujerumani uko kinyuma cha uingereza.

Mfano; uingereza unapewa fomula ukokotoe.
Ujerumani unaanza kukokotoa, mnachanganua mpaka mwisho mnapata fomula.

Scandinavia uko nako mtaala wao tofauti, na utofauti wao unatokana na utamaduni wao wa kuheshimu kila mtu. Wao hawana mambo ya kujikweza kwamba mimi ni flani wewe sikitu.

Sasa labda wao uingereza kuna mambo mengine wanazingatia, ila wengi wao huwa hawajui kuandika. Hayo ni matokeo ya elimu tulioridhi. Tafuta mzungu yyt, kati ya 5 ukiweza kusoma zaidi ya 3 wewe ni fundi. Maana wanaandika kama bata.
 
Back
Top Bottom