Mh. Mwanamichakato, sijui nikuite ni mzalendo, ama umekuwa na mawazo ya kizalendo.
Ni kweli tukiwa na petroleum refinery industry yetu, hakika tutapunguza sehumu kubwa sana ya gharama za uagizaji wa petroli, dizeli, oil pamoja na bidhaa mbali mbali zitokanazo na usafishaji wa crude oil petroleum.
Hebu tujiulize hasa sisi wa gen. wa miaka ya 50s, 60s, ni kwa nini TIPER iliuliwa?
Wengine wanasema ati ni sababu TIPER wakati inajengwa, idadi ya WaTanzania ilikuwa na ndogo, wengine wakasema ati technology ilishapitwa na wakati.
Hizo zote zilikuwa ni sababu za kuhalalisha upigaji tu.
Tunapo waambia nchi hii, TANZANIA upigaji ulianza zamani na sasa imekuwa kansa sugu, huwa hamuelewi.
Ni jambo jema sasa kuianzisha TIPER mpya sasa tukilenga na usafishaji wa mafuta (crude oil petroleum toka Uganda kwa Bomba linalojengwa sasa, ni kweli tutapunguza ama tutashusha bei za bidhaa za petroleum.
Je, viongozi wetu waliona hili? Wanayo mawazo haya ya kizalendo? Je, nao wanamawazo hayo hayo ya kipigaji?
Ndugu Mwanamichakato, nakuomba fanya re-search kidogo tu juu ya mampuni yenye kibali cha kuagiza bidhaa za petroleum toka nje, je, hakuna mikono mingi ya viongozi wetu wengi kwenye makampuni hayo?
Mwl. Nyerere (RIP) alisema, mtu akila nyama ya mtu hawezi kuacha. Je, na hawa viongozi wetu walishakula nyama ya mtu, ni kweli watakumbuka wazo hili la kujenga TIPER nyingine?
Siku hizi wao wanaita kulamba ASALI, je wataacha? Siku hizi kuna wazo la kusema tunawakaribisha wawekezaji, (wakoloni mamboleo) , je, hata hilo wazo wanalo?
Huenda tutapata ukinzani mkubwa toka nje, hasa wale watuuziao bidhaa za petroleum, hivi ni kweli?
Kama sivyo, ama ndivyo, tutawasaidiaje hawa viongozi wetu?