MIXOLOGIST
JF-Expert Member
- Mar 1, 2016
- 14,311
- 36,056
ishushwe daraja
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Timu yetu ina tatizo kwenye uongozi zaidi kuliko kikosi, kwani kikosi bado kinatengeneza nafasi nyingi na shida ni wa kuzifanya magoli tu.Leo wana lunyasi tujadiliane namna ya kunusuru timu yetu baada ya kuona sasa tunapokwenda sio kabisa,kulingana na mustakabali wa team yetu.
Simba ni team ambayo ilijizolea umaarufu mkubwa sana hapa barani Afrika na ulimwenguni pia,club ya simba ilishaanza kuwa tishio midomoni, masikioni mwa mataifa mengi balani Afrika na imefikia hatua hata club itakayopangiwa na simba basi walikuwa na kimuhemuhe.
Simba hii ilishaanza kujijengea heshima mpaka CAF huko na kupewa offer mbali mbali kuanzia AFL na mengine,hapo hatujagusia masuala ya dili za hapa na pale.
Naamini kama tutapeana elimu na nini chakufanya basi kaunzia sisi mashabiki tunaweza kuiweka Simba mahali salama kabisa,tuache ule msemo wa kijinga kwamba"SIMBA NA YANGA" haiwezi kuwa za moto zote kwa pamoja hivyo lazima kuna kipindi mmoja atashuka"huu ni msemo kwa watu wasio na maono".
Tuanze kwa mashabiki nini tufanye,tuje kwa wanachama wenye kadi nini waanye,tumalizie na viongozi kipi wafanye.
Ni vyema hata wa upande wa pili ukatoa hoja za busara kuliko kushambuliana,tunapotaka kutatua tatizo kama hili lina milolongo yake hivyo lazima tufate procedure zoote za kufanikisha jambo hili.
NINI KIFANYIKE KUINUSURU SIMBA HII
Mo tunamkumbusha kwa bakora ili amrudishe babraS
asa umchape mo halaf Babraham arudi kweli jombaa bila mo ungemjua Babraham wewe?
Hiyo itasaidia mashabiki wana.mchango mkubwa Sana.Tuwasusie tu timu na uwanjani tusiende
Ndugu yangu umetuchoka!!!Simba arudishwe tuu mbugani akale Hata nyasi kama mjini hapawezi
Watu walienda kutafuta rizki.Mechi ya juzi Simba na Mashujaa, tulikuwa watazamaji almost 50 kipindi cha kwanza kilivyoisha tu watu wakaondoka. Kipindi cha pili tuliangalia watu kama 20 tu wengne hawajarudi tena. Hii timu ina shida kubwa sana nahisi kuna ishu chini ya kapeti.
B… hii ilifaa iwe thread kamili, umeongea mengi yaliyoniacha nikitafakari mengi.Timu yetu ina tatizo kwenye uongozi zaidi kuliko kikosi, kwani kikosi bado kinatengeneza nafasi nyingi na shida ni wa kuzifanya magoli tu.
Kwa sasa ndani ya timu yetu kuna shida kubwa ya uongozi, tayari Mwenyekiti wa Bodi na mwekezaji hawaongei lugha moja kama awali.
Hadi sasa baadhi ya posho za ushindi wa mechi zimekatwa na kufutwa, hii inashusha sana ari za wachezaji wetu na watendaji.
Kitendo cha watu wote wa mwekezaji kuondolewa na baadhi kupelekwa timu B kunazidi kukoleza mahusiano mabovu ya Bodi na mwekezaji.
Kwa sasa imefikia kuwa mwekezaji ahudumii timu ipasavyo, na kufanya mambo mengi yawe mabegani mwa Mwenyekiti wa Bodi.
Kwa jinsi mwekezaji alivyohamishia makazi yake nchi nyingine, nje ya Tanzania, ndiyo anazidi kuwa mbali na timu.
Hivyo, labda tuanze sasa mchakato upya wa uwekezaji kwenye timu yetu, ili tuwe na sheria na masharti mapya au mwekezaji mpya.
Ova