Nini kifanyike kuinusuru hii Simba?

sasa nyie wengine mnataka ushauri hlf muupeleke wapi wakati timu ni ya muhindi?
 
Timu yetu ina tatizo kwenye uongozi zaidi kuliko kikosi, kwani kikosi bado kinatengeneza nafasi nyingi na shida ni wa kuzifanya magoli tu.

Kwa sasa ndani ya timu yetu kuna shida kubwa ya uongozi, tayari Mwenyekiti wa Bodi na mwekezaji hawaongei lugha moja kama awali.

Hadi sasa baadhi ya posho za ushindi wa mechi zimekatwa na kufutwa, hii inashusha sana ari za wachezaji wetu na watendaji.

Kitendo cha watu wote wa mwekezaji kuondolewa na baadhi kupelekwa timu B kunazidi kukoleza mahusiano mabovu ya Bodi na mwekezaji.

Kwa sasa imefikia kuwa mwekezaji ahudumii timu ipasavyo, na kufanya mambo mengi yawe mabegani mwa Mwenyekiti wa Bodi.

Kwa jinsi mwekezaji alivyohamishia makazi yake nchi nyingine, nje ya Tanzania, ndiyo anazidi kuwa mbali na timu.

Hivyo, labda tuanze sasa mchakato upya wa uwekezaji kwenye timu yetu, ili tuwe na sheria na masharti mapya au mwekezaji mpya.

Ova
 
Ikila mkono mwingine hiyo tarehe 20 April, solution itapatikana tu.
 
Hata Yanga walipotia wakati mgumu (kuchangisha bakuli) lakini walijipanga na sasa wanafanya vizuri.

Simba pia wajipange, timu inatakiwa kusajili wachezaji wenye ushindani wa kutosha hasa kwenye kufunga magoli.
 
Mechi ya juzi Simba na Mashujaa, tulikuwa watazamaji almost 50 kipindi cha kwanza kilivyoisha tu watu wakaondoka. Kipindi cha pili tuliangalia watu kama 20 tu wengne hawajarudi tena. Hii timu ina shida kubwa sana nahisi kuna ishu chini ya kapeti.
Watu walienda kutafuta rizki.
 
B… hii ilifaa iwe thread kamili, umeongea mengi yaliyoniacha nikitafakari mengi.

Wajua nimekuwa nasikia mengi zikiwemo lawama kuelekezwa kwa mwekezaji ila niliona kama chokochoko hadi uliposema hivi ndio nimeamini.
 
Ukweli mchungu lakini ndio ufumbuzi wa kila kitu kabla ya yote Simba ianze na usajili wa viongozi. Simba iwaondoe Try Again and Mangungu haraka sana kabla ligi haijaisha. Kwenye uongozi Simba iwasajili haraka sana watu wenye kujua fitina za mpira Magori na Dalali pale juu hata kama ni kwa kipindi cha mpito kuelekea kupata viongozi wengine. Try Again na Mangungu wameshathibitsha kuwa hawaujui mpira na hata fitina za mpira hawazijui.

Ifike mahali sasa Simba iwasamehe Kaburu, Tuli na Aveva warudi kwenye uongozi pamoja na kuwa wana tuhuma za upigaji pesa kwani baniani mbaya kiatu chake dawa. Hao wakina Kaburu, Tuli na wengineo ndio watu wanaoweza kupambana na na wakina Hersi + Arafat. Vinginevyo wanasimba wakiendelea kukomaa na kuwazuia wakina Kaburu wasirudi basi wajue kabisa Yanga atatawala soka la bongo kwa muda mrefu. Na mbaya zaidi Azam wameanza kujitambua kwa maana hiyo Simba wasipochukua hatua sasa hivi kabla ligi haijaisha basi hata nafasi ya pili itakuwa historia.

Ni mtizamo tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…