Nini kifanyike kumsaidia Nikki Mbishi?

Aimbe na atumie tungo kama za NAY
Nini maana ya Sanaa sasa kama atashindwa kuwa yeye kama yeye, inawezekana umeanza kumsikiliza juzi ama ndio umemfahamu kupitia thread hii, Ningekushauri tu jaribu kununua kazi zake utakutana na hiyo message unayoitaka, album yake ya mwisho nimeinunua ni Katiba Mpya Ina nyimbo kama Watanganyika wadanganyika, Bara zuri, Nani aliyeturoga na Katiba mpya, zote hizo zina aina ya maudhui unayoyataka
 
Tangu lini sinza akatoka mtu timamu?
Kule ni wapakwa mafuta tu na wazembe.
 
Yaeza kua nkajua kazi zake zaidi yako, na mara nyingi msanii lazima awe na uwezo wa kucheza na mahitaji ya fans, lifestyle ya wasikilizaji wa nyimbo zake hubadlika kila day, msanii lazima awe flexible ndo maana akina Fid, Dully, nk wapo mzigoni jana na leo, walioamua kuuishi uzamani wanapotea kila kukicha.
 
Presentation skills inaweza fanya mzigo usiende kwa walengwa
 
Atafute menejimenti. Akipata menejimenti nzuri, kipawa chake kikubwa kitamnufaisha yeye na kizazi chake. Pia, menejimenti itamsaidia kujidhibiti. Uhuru alionao unautumia vibaya. Inatakiwa akaunti zake ziwe chini ya menejimenti na zitumike kufanya mambo ya tija yatakayomsaidia kuongeza kipato na kujitanua kisanaa.

Atakufa masikini pamoja na kuwa ndiye MCEE bora wa muda wote hapa Bongo.
 
Ndio maana na yeye ana mashabiki/wasikilizaji wake, wasingekuwepo sidhani kama angeendelea kutoa album. Hao unao waita flexible wana fan base yao pia vile vile kuna watu hata hawawafahamu kabisa
 
sio yeye tu,wasanii wengi wa rap wamekata ringi, wanachorap hakina soko wala mashiko so watapataje pesa? ila wengi wao ni masela m*vi tu na wanazidi kuuendekeza.
 
Amefanya kitu gani cha kumtia aibu?Umesimanga kuliko kueleza kafanya nini.
 
sio yeye tu,wasanii wengi wa rap wamekata ringi, wanachorap hakina soko wala mashiko so watapataje pesa? ila wengi wao ni masela m*vi tu na wanazidi kuuendekeza.
Eti wanasema wanakomboa mitaa ilihali wao njaa kali ndio wanapaswa kukombolewa 😂
 
Msanii inabidi sanaa yako ieleze mawazo yako, ukiona hadi unatumia mitandao kufikisha mawazo yako, maana yake sanaa yako ni mfu.
 
Kama boss anapakwa mafutwa chawa kama huyu yeye inafanywaje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…