moodykabwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2015
- 625
- 602
TFF ivunjwe. Kama alivyofanya JK kumpata Maximo, tuende nchi za ulaya mf. Ufaransa tukaombe wazee wastaafu waliopata kuongoza soka nchini mwao. Waje waongoze TFF huku wakituwekea misingi mizuri. Wachawi wa soka laTz si TFF bali ni vilabu vitatu, Yanga na Simba vyenye dhambi ya kuweka mawakala wao hapo TFF badala ya viongozi, na Azam inayotumia nguvu ya pesa ku-influence maamuzi mbalimbali.Naomba tujadili wataalam wa mpira ni kwann mpira wetu Tanzania umegubikwa na maneno maneno sana??
Nini kifanyike tutoke hapa Tulipo??
Nawasilisha kwenu wazalendo wa TANZANIA
Taarifa: wachezaji wanaolipwa hiyo mil 3-5 wapo japo wengi ni wakigeni.MALIPO
Baadhi ya wachezaji ligi daraja la nne na la pili wanacheza kwa kujitolea tu hawalipwi na wakilipwa wanapewa shs 10,000 mpk 15,000 kwa mechi wakiumia hakuna huduma za matibabu wanakwenda kutibiwa na familia zao.
Baadhi ya timu ligi kuu wachezaji wanalipwa 300,000 chini ya laki5 na bado wanacheleweshwa kulipwa..mchezaji yupo uwanjani anakuwa na stress kibao, familia itakula nn, kodi atalipa vp, ada ya shule kwa mtoto, ataweka akiba vp ajenge nyumba nk
Ifikie hatua michezo ipewe thamani na mpira uwe unalipa angalau na sisi tusikie mchezaji kanunuliwa japo milioni 100 kwenye club angalau watu wapate hamasa waongeze juhudi mpira unalipa.
Ifikie hatua mchezaji ligi kuu alipwe japo milioni 30 kwa mwezi na standards kiwango cha chini alipwe japo milion 3-5 after tax
Nikimkumbuka Imani Madega naanza kuuona ukweli ktk hoja yako.Nimejaribu kufwatili katiba za vilabu mblai mbali za ligi kuu Tanzania kiukweli hakuna katiba ilioko kwa ajili ya mpira
Hizi Timu zote zipo kwa ajili ya kisiasa tu Watu waje watengeneze majina yao uchaguzi ukifika utasikia wanagombea ubunge au udiwani
Pia bwana RageNikimkumbuka Imani Madega naanza kuuona ukweli ktk hoja yako.