MALIPO
Baadhi ya wachezaji ligi daraja la nne na la pili wanacheza kwa kujitolea tu hawalipwi na wakilipwa wanapewa shs 10,000 mpk 15,000 kwa mechi wakiumia hakuna huduma za matibabu wanakwenda kutibiwa na familia zao.
Baadhi ya timu ligi kuu wachezaji wanalipwa 300,000 chini ya laki5 na bado wanacheleweshwa kulipwa..mchezaji yupo uwanjani anakuwa na stress kibao, familia itakula nn, kodi atalipa vp, ada ya shule kwa mtoto, ataweka akiba vp ajenge nyumba nk
Ifikie hatua michezo ipewe thamani na mpira uwe unalipa angalau na sisi tusikie mchezaji kanunuliwa japo milioni 100 kwenye club angalau watu wapate hamasa waongeze juhudi mpira unalipa.
Ifikie hatua mchezaji ligi kuu alipwe japo milioni 30 kwa mwezi na standards kiwango cha chini alipwe japo milion 3-5 after tax