Nini kifanyike kuongeza ufaulu wa somo la Hesabu

muhinda-moja

Senior Member
Joined
Sep 22, 2014
Posts
117
Reaction score
9
Wadau nakaribisha mawazo nn kifanyike ili kuongeza ufaulu wa mathematics kwa o'level kwani hata shule zenye wali napo ufaulu unasuasua kama zile shule ambazo hazina waalimu.
 
Kuwe na njia nyepesi za kufikia jibu. Kwa mfano katika topic inayohusiana na mambo ya simultaneous equation, kuna njia nyepesi sana kufikia jibu, lakini haitumiki.
 
Kuwe na njia nyepesi za kufikia jibu. Kwa mfano katika topic inayohusiana na mambo ya simultaneous equation, kuna njia nyepesi sana kufikia jibu, lakini haitumiki.

njia gani hiyo mkuu,kwani kuna elimination method,na subsititution method,hiyo nyingine ni ipi broo.
 
Somo la Hisabati kama linavyofahamika ktk shule za msingi si somo gumu, lakini ni somo ambalo ili mwanafunzi alifauru ni lazima alipende. Kwa wanfunzi kupenda somo kunajengwa na sababu nyingi.

Nitazitaja chache tu
1. Mwl anayemfundisha mtoto katka madarasa ya awali(darasa la I, II na III). Awe mwenye competent teaching skills.

2. Mazingira ya kujifunzia (vitabu na mazoezi yanayosimamiwa kwa karibu...exercises with close supervision)

3. Walimu wenye ari na moyo wa kuwaelewesha wanafunzi katk madarasa yanayofuata nk.

Mtoto anaanza kupenda hesabu au kuzichukia akiwa katika madarasa ya 3 na 4, katka madarasa haya akiwa na walimu wazuri wenye ari na moyo wa kufundisha watazingatia hayo nilotaja hapo juu na mwanafunzi ataendelea kupenda somo la hesabu.

Lakini suala la kufikiri kuwa mwanafunzi atapenda hesabu akiwa secondari ni kujidanganya.

Madarasa ya 5 6 na 7 na hatimaye secondari ni matokeo ya msingi uliotengenezwa ktk shule ya msingi; ndio maana mtoto aliyekuwa anafanya vizur hesabu shule ya msingi ataendelea kupenda hesabu akifanikiwa kufundishwa na mwl mwenye ari na moyo wa kuelewesha ktk shule ya secondari na kuendelea!
 
kuwepo na competent teacher wa somo la hesabu wa kutosha kwasababu kuna waalimu wanafundisha hesabu lakini wenyewe hawajui hesabu vya kutosha hii itasaidia sana.

Kwa mfano mimi wakati ninasoma secondary mwalimu wangu wa hesabu alikuwa anajua kufundisha vizuri na pia alikuwa anatupatia njia ya kuprove majibu yetu baada ya kufanya calculation na kupata solution of course nilikuwa nainjoy sana kwani nilikuwa na uhakika na majibu yangu kitu ambacho kilinisaidia kufaulu vizuri somo la hesabu !!!!
 
Kuhakikisha wanapata walimu wengi, wazur, wenye uwezo, na teaching skills nzur ili wanafunzi waweze kulipenda somo wakiwa bado wachanga, na kutoa kasumba ya kusema hesabu ni ngumu.

hakuna cha ugumu kila somo ni gumu ndo maana nilipata F ya history ila yote ni BACKGROUND
 
Kwa Tz hii chini ya CCM labda mshusheni pass mark to 10 percent.
 

Pole mkuu!
 
njia gani hiyo mkuu,kwani kuna elimination method,na subsititution method,hiyo nyingine ni ipi broo.

Hiyo nyingine haipo kwenye vitabu vyote vya mathematics ulimwenguni, ila nipo nayo kichwani, labda siku moja unaweza kuiona na kuitumia.

Nipo bado katika kutafuta njia nyepesi hata katika topic zingine.
 
MHH hesabu balaa ingawa me o level nilikuwa kilaza wa history kuliko hesabu, nlivoenda advance BAM ikaanza kunikimbiza nkaifauru kwa msaada wa BRN
 

Well said Ila niongeze pia wazazi nao wanahusika katika kuwasaidia watoto kulipenda somo la hesabu.. encouragement inahitajika sana Sio mzazi anakuwa wa kwanza kusema "umefeli hesabu??

Huo ugonjwa wa taifa"
 
Hiyo nyingine haipo kwenye vitabu vyote vya mathematics ulimwenguni, ila nipo nayo kichwani, labda siku moja unaweza kuiona na kuitumia. Nipo bado katika kutafuta njia nyepesi hata katika topic zingine.

tanzania itajivunia kua na wewe!
 
Motisha kwa walimu wa hisabati iwepo., mishahara iboreshwe kwa kuwazuia walimu wa hisabati wasihame kada nyingine, madaraja ya walimu yapande kwa wakati, walimu walipwe malimbikizo yao ya likizo, miundo mbinu kama maji, umeme, barabara, ualime iwe kazi kama kazi zngine ili tuondokane na dhana kuwa ualimu sio kazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…