muhinda-moja
Senior Member
- Sep 22, 2014
- 117
- 9
Wadau nakaribisha mawazo nn kifanyike ili kuongeza ufaulu wa mathematics kwa o'level kwani hata shule zenye wali napo ufaulu unasuasua kama zile shule ambazo hazina waalimu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
hesabu zt zwe za kujumlisha
Kuwe na njia nyepesi za kufikia jibu. Kwa mfano katika topic inayohusiana na mambo ya simultaneous equation, kuna njia nyepesi sana kufikia jibu, lakini haitumiki.
Kuhakikisha wanapata walimu wengi, wazur, wenye uwezo, na teaching skills nzur ili wanafunzi waweze kulipenda somo wakiwa bado wachanga,na kutoa kasumba ya kusema hesabu ni ngumu.
hakuna cha ugumu kila somo ni gumu ndo maana nilipata F ya history ila yote ni BACKGROUND
Kwa Tz hii chini ya CCM labda mshusheni pass mark to 10 percent.
Tuangalie kipindi cha junia jumbo cha tbc kila jumamos saa 3 kamili.....
njia gani hiyo mkuu,kwani kuna elimination method,na subsititution method,hiyo nyingine ni ipi broo.
Somo la Hisabati kama linavyofahamika ktk shule za msingi si somo gumu, lakini ni somo ambalo ili mwanafunzi alifauru ni lazima alipende. Kwa wanfunzi kupenda somo kunajengwa na sababu nyingi. Nitazitaja chache tu
1. Mwl anayemfundisha mtoto katka madarasa ya awali(darasa la I, II na III). Awe mwenye competent teaching skills.
2. Mazingira ya kujifunzia (vitabu na mazoezi yanayosimamiwa kwa karibu...exercises with close supervision)
3. Walimu wenye ari na moyo wa kuwaelewesha wanafunzi katk madarasa yanayofuata nk.
Mtoto anaanza kupenda hesabu au kuzichukia akiwa katika madarasa ya 3 na 4, katka madarasa haya akiwa na walimu wazuri wenye ari na moyo wa kufundisha watazingatia hayo nilotaja hapo juu na mwanafunzi ataendelea kupenda somo la hesabu. Lakini suala la kufikiri kuwa mwanafunzi atapenda hesabu akiwa secondari ni kujidanganya. Madarasa ya 5 6 na 7 na hatimaye secondari ni matokeo ya msingi uliotengenezwa ktk shule ya msingi; ndio maana mtoto aliyekuwa anafanya vizur hesabu shule ya msingi ataendelea kupenda hesabu akifanikiwa kufundishwa na mwl mwenye ari na moyo wa kuelewesha ktk shule ya secondari na kuendelea!
Hiyo nyingine haipo kwenye vitabu vyote vya mathematics ulimwenguni, ila nipo nayo kichwani, labda siku moja unaweza kuiona na kuitumia. Nipo bado katika kutafuta njia nyepesi hata katika topic zingine.