Nini kifanyike kupunguza matokeo mabaya form four?

Nini kifanyike kupunguza matokeo mabaya form four?

mbaraka.m

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2011
Posts
209
Reaction score
37
Kwa upande wangu naona yafuatayo yafanyike:1-mitaala yenye kueleweka.2-mwisho kwenda ualimu grade A iwe div three.3-kuwe na pre-form 1 kwa one yr kuwaandaa wanafunz kuingia kidato cha 1.4-lifestyle za wazaz na wanafunz zibadilike i.e wazaz wajue wajibu wao na wanafunz wajue kwa nin wanasoma na kuachana na ubitoz na usharobaro.5-maslah kwa walimu.6-miundo mbinu mashulen iboreshwe eg maktaba.7-viboko shule ya msing zirudishwe ili kubust nidhamu.8-mtihan wa taifa form two urudishwe.9-kabla ya wanafunz kuanza pre-form 1 kuwe na wiki 2 za guiding and counselling. NB-elimu ya msing ndo dira ya yote,wadau ongezeeni mengine
 
Walimu warudishiwe morale madai yao yatekelezwe matokeo ya kmlazimisha mwal aingie darasani anaishia kutofundisha .

Walim wana mgomo baridi! haiwezekani kufeli kwa namana hii!
 
USIMAMIZI thabiti wa mfumo wa elimu! Inawezekanaje mwanafunzi apate ziro kidato cha nne kama mfumo wetu ungekuwa imara? Hivi hakuna kufeli kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne? Hawa asilimia 60 ama walipaswa kurudia au kuacha shule kabla ya kujiandikisha kufanya mtihani. LAKINI pia kama taifa tujitathmini huu mfumo wa kumpima mwanafunzi kwa kutegemea mtihani mmoja tu umepitwa na wakati. Huu ni mfumo wa kikoloni na hautusaidii watz. Tunawachokesha bure Watoto kukariri madudu ambayo hata hawatayafanyia kazi huko baadaye.
 
Vipi lile wazo la misosi shuleni???

ni kweli kaka.Shule za msing halmashaur ya chamwino zilikuwa ndani ya mpango wa chakula(WFP)na matokeo yalikuwa mazur kutokana na maudhurio
 
Nataman haya mawazo niya print then nimpelekee wazir husika
 
Ya kufanya ni mengi sana na pengine ni kuanza na watawala kwa kuwaambia wajiuzulu ili tuoverhauline kila kitu
 
Nadhani kikubwa ni motisha kwa walimu maana hata kama shule haina vitabu kama mwalimu yuko motivated atahangaika kutafuta material kwa udi na uvumba na atakuwa na uchungu akiona wanafunzi wake hawamwelewi kwa hiyo atatumia kila mbinu kuwafanya wamwelewe. Kwa hiyo mimi naona Mwalimu Kwanza
 
Wote mmeongea ila mtu wa mwisho wa kuimpart knowledge kwa mwanafunzi mmemsahau mpaka leo mshahara wake ni duni alafu mnategemea afanye kazi sawa na mfanyakazi wa TRA?
 
Back
Top Bottom