Nini kifanyike kurejesha eneo lililogeuzwa kuwa barabara?

kiredio Jr

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2024
Posts
989
Reaction score
1,843
Habari zenu wadau

Naomba Msaada wa ushauri au maoni kuhusu jambo hili.

Ikiwa umenunua kiwanja maeneo ya kando ya mji, ukajenga nyumba na eneo lingine likabaki, majirani walipoanza kuongezeka wakaomba kutumia eneo lile kama njia ya miguu, mwisho ikawa njia kuu ya wao na magari ya kuingia majumbani mwao.

Je, mmiliki ukitaka kurejesha eneo lako unapaswa kufuata taratibu za kisheria au unaamua tu kufunga hiyo njia? Na je majirani wanaweza kuzuia kitendo hicho au ipo sheria inayo walinda?

Naombeni maoni yenu juu ya hili, maamuzi yanahitajika.
 
Ramani halisi ya eneo ipo, na ilitolewa na kampuni iliyo uza kiwanja.
Basi kaza sura nunua nguzo zungushia eneo lako ni rahisi TU Kisha atakae pata bugudha ataenda serikali ya mtaa wakikuita waoneshe makaratasi
 
Habari zenu wadau

Naomba Msaada wa ushauri au maoni kuhusu jambo hili.

Ikiwa umenunua kiwanja maeneo ya kando ya mji, ukajenga nyumba na eneo lingine likabaki, majirani walipoanza kuongezeka wakaomba kutumia eneo lile kama njia ya miguu, mwisho ikawa njia kuu ya wao na magari ya kuingia majumbani mwao.

Je, mmiliki ukitaka kurejesha eneo lako unapaswa kufuata taratibu za kisheria au unaamua tu kufunga hiyo njia? Na je majirani wanaweza kuzuia kitendo hicho au ipo sheria inayo walinda?

Naombeni maoni yenu juu ya hili, maamuzi yanahitajika.
Kwanza kabisa, ufate taratibu za kukli[patia eneo lako hati kubwa ya wizara ya ardhi. Maana hiyo itajumuisha vipimo vyote vya halali.
 
Ikiwa ramani ya eneo ipo hata kama si rasimi na kila aliyenunua alionyesha njia ya kwenda kwake bado una haki ya kutumia eneo lako. Aliyepaswa kutoa barabara au njia ni muuzaji wa eneo na si wewe. Hakuna cha mtu wa juu Serikalini zaidi ya Rais ambaye ndo amekasimishwa madaraka ya kusimamia ardhi kwa niaba ya watanzania
 
Vipimo vya awali ninavyo lakini pia wizarani ni muhimu kwenda na kupata vielelezo kutoka kwao
 
Sio woga ila sipendi migogoro
Yah migogoro hasa ya ardhi sio mizuri ila kwa hapa huu wako sio mgogoro huku mitaani wengi tu tena watu wa kawaida kabisa wanafunga njia na watu wanafata njia ya mtaa bila bugdha
 
Ila mkuu mi napingana kidogo na waliokushauri huko juu. Mi nakushauri kwanini usiache tu iwe njia? Najua ni ardhi yako ila kama ni katikati ya kiwanja chako nakushauri i-divert tu njia ipite kwa pembeni Kisha zungushia uwa eneo linalobaki au kama ni njia imejianzisha pembeni ya kiwanja chako mega tu Hilo eneo acha iwe njia ya kudumu.

Hii haitakuwa unyonge au haitamaanisha umeshindwa vita ila kwanza utakuwa umesaidia jamii kwa kiasi kikubwa pili, utakuwa umeepusha migogoro endelevu na mwisho itaonesha ukomavu wa kifikra

Ni hayo tu mkuu
 
Ikiwa ramani ya eneo ipo hata kama si rasimi na kila aliyenunua alionyesha njia ya kwenda kwake bado una haki ya kutumia eneo lako. Aliyepaswa kutoa barabara au njia ni muuzaji wa eneo na si wewe. Hakuna cha mtu wa juu Serikalini zaidi ya Rais ambaye ndo amekasimishwa madaraka ya kusimamia ardhi kwa niaba ya watanzania
Sasa nimejua raamani ya eneo ndyo suluhisho, nimekuelewa vizuri kaka
 
Back
Top Bottom