Nini kifanyike kurejesha eneo lililogeuzwa kuwa barabara?

Naweza nikaacha iwe njia kwani ni muda mrefu inatumika hivyo, lakini kwa sasa nataka kuongeza ujenzi maalum kwaajili ya mifugo yangu.
 
Eneo lako si lina mipaka rasmi?

Kama ndio basi huna budi kuzungushia uzio kuonesha eneo lako linapoishia...
Mipaka rasmi ipo na majirani wa kwanza kuja walikuta hakuna njia kabisa na wakaomba watumie kwa kupitia wao na kupitisha vifaa vyao vya ujenzi
 
Eneo langu la kwanza(halikupimwa) nilichelewa majirani wote wakajenga kiwanja changu na jirani nyuma yangu ikawa main road. Kuiziba na njia rasmi iko mbali ingekuwa mgogoro, niliacha barabara ya kama 4m mwishoni mwa kiwanja.
Eneo lingine(limepimwa) nilipoona tu watu wanaacha barabara rasmi kisa inajaa maji na kugeuza eneo langu barabara nikasema sitarudia kosa. Jumapili moja nikapiga msingi wa fence kozi tano kuzunguka eneo lote ndio ikawa mwisho wa kutumiwa kama njia ya magari.
Hapo kama umechelewa watu wote washazoea kuepusha Shari mega mita chache tu acha njia.
 
Niliongea na jirani mmoja akasema alisikia mwingine akisema yeye ni mtu wa juu serikalini na hawezi kubali njia ifungwe
basi vielelezo sahihi huna
kuna mwamba aliziba njia, inayounga pale Victoria(pembezoni mwa benki ya NBC) na M/Nyamala kwa kopa,
njia ina upana wa zaidi ya mita 15, alinunua miaka ya 90 huko
alipiga ukuta mmoja matata sana, wakapiga kelele wee, sa hivi kimya
 
Wajirani wakiomba njia unatakiwa uwaambie piteni juu .......ulifanya kosa sana kuwapa njia hao
 
Niliongea na jirani mmoja akasema alisikia mwingine akisema yeye ni mtu wa juu serikalini na hawezi kubali njia ifungwe
Sasa hao wanaojitia watu wa juu ndio wa kuwanyoosha kwa vyovyote nakwambia tena anza nae huyo alafu nikupe tu mara nyingi hiyo inatumika kama defence mechanism tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…