Nini kifanyike kwenye hali hii ya tofauti ya majina?

Nini kifanyike kwenye hali hii ya tofauti ya majina?

UMUNYU

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2017
Posts
726
Reaction score
564
Naombeni ushauri wa nini kifanyike. Mdogo wangu amesoma hadi chuo kikuu. Jina la ubatizo alilolitumia shule ambalo liko kwenye vyeti vyake ni tofauti na jina alilopewa na wazazi kabla ya ubatizo.

Jina hilo la kabla ya ubatizo liko kwenye hati za mashamba aliyoachiwa na baba mkubwa, nauliza nini kifanyike ili jina hilo liingizwe hata kwenye cheti chake cha kuzaliwa?

Najua kwenye vyeti vyake vya shule haiwezekani
 
Hakuna kisichowezekana hapo! cha kufanya aende mahakamani huko atakula kiapo cha kubadili jina kisha atapewe hati ya utambuzi wa majina yake hayo .
 
Back
Top Bottom