Nini kifanyike ualimu uheshimike?

Nini kifanyike ualimu uheshimike?

M24 Headquarters-Kigali

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2012
Posts
8,199
Reaction score
8,186
Wakati nasoma chuo wale watu waliokuwa wanasoma Education walikuwa hawataki hata kujulikana wanasoma nini maana kwao ilikuwa ni aibu kuonekana unasoma Education. Mtu yupo tayri kukuazima kitabu cha Course yoyote ya Law ili mradi tu aonekane si mtu wa Education. Ndo najiuliza hapa kipi kifanyike ili Fani ya UALIMU iheshimike????
 
Fani ya ualimu ni muhimu sana katika maisha ya binadamu, na unae ona anaibeza huyo ni tahiraa asiejitambua na kuelewa kua hapo alipo ni walimu ndio wame mfikisha. Walimu ungamaneni, mshikamane kwa badiriko yenu.
 
Ni kitu rahisi sana.Ni kwa kuwalipa walimu mshahara na posho, marupurupu kama wabunge na viongozi wa juu wa serikali na kuwalipa wabunge na viongozi wa juu wa serikali sawa na mshahara na marupurupu wanayolipwa walimu. Hata kwa majaribio ya miezi sita tu itatosha kurudisha heshima ya walimu na fani ya ualimu.

Baada ya miezi sita ya majaribio, serikali na wabunge watatengeneza mazingira ya fani ya Ualimu iheshimike.
 
Mmmm! Japo umetia chumvi nyingi lakini pia serikali imekuwa ikichangia kwa kiasi kikubwa, mtu aliyepata karibu na div.0 eti huyo akienda kuomba vyuo vya ualimu anapokelewa kwa mikono miwili sasa kwa nini walimu wasidharaulike. Kupata ualimu iwe bahati kama kupata sheria hapo heshima itakuwepo pamoja na kuboreshewa mazingira.
 
Fani ya ualimu ni muhimu sana katika maisha ya binadamu, na unae ona anaibeza huyo ni tahiraa asiejitambua na kuelewa kua hapo alipo ni walimu ndio wame mfikisha. Walimu ungamaneni, mshikamane kwa badiriko yenu.

like,respect to you
 
Hivi 'maporofesa' na 'malechara' nao ni "walimu"? Kama ndio, nao wanadharaulika?
 
Back
Top Bottom