Salamu,
Dunia inaenda kasi sana! Tulipokuwa wadogo tukifuatilia na kufundishwa harakati za ukombozi Afrika na dunia, tulijifunza (lau kidogo) uhuru na haki ya Wapelestina. Tulisoma kuhusu Yassir Arrafat na Palestine Liberation Army (PLO). Wakati huo, kama ilivyokuwa kwa POLISARIO cha Sahara Magharibi, Tanzania ilikuwa inaunga mkono PLO dhidi ya Israel.
Kumbuka wakati huo tulikuwa hatufungamani na upande wowote! Leo hii, siasa zetu kuelekea mzozo wa Mashariki ya Kati hazieleweki! Nafikiri sasa ndio hatufungamani na upande wowote! Kulitokea nini, au ulikuwa ni msimamo wa Mwalimu Nyerere? Hivi vuguvugu la POLISARIO lilishaje?
Leo hii nipo mtu mzima, lakini nipo nyuma kwa siasa za dunia kuliko nilipokuwa shule ya msingi! Sijui nini kimenikumba! Na nini kimelikumba taifa!