JOHNGERVAS
JF-Expert Member
- Mar 22, 2016
- 1,011
- 1,681
Wakuu zamani vijana wengi wa kikatoliki moja kati ya ndoto zetu ilikuwa ni kuwa Mapadre.
Mimi binafsi nilijichanganya sana Huko Rombo, parokia ya Mkuu wakati huo nilikuwa napenda sana Shirika la mtakataifu Aloyce, kutumikia altareni huku ndoto zetu ikiwa ni baadae kwenda seminari hadi Upadrisho
Asee wakati huo nilikuwa najitoa sana nilikuwa sipendi mademu wala pombe yaani nilikuwa nikisikia mtu anakkunywa pombe namuona kama ibilisi, shetani kabisa.
Nilipofika kidato cha tatu mwamba nikaanza kujichanganya na wadau,Pombe kwa sana mademu full yaani unalewa hadi walevi wanakuita mlevi. Malaya kuwazidi hata wale uliowakuta kwenye tasnia ya zinaa
Nikaanza kupotezea masuala ya kutumikia na mawazo ya upadre yakakata kabisa, Nilikuwa na washkaji wengi sana wakati Huo wanaitwa Gilliadi, Imma,Isdovic, Ireneusi, Fredias, Hillary n. katika ile timu ni Hillary na Evaristi tu ndio mapadre kwa sasa.
Wale vijana wengine ndio tumekuwa na tabia mbaya kuliko watu wengine mtaani.
Binafsi ndoto yangu ilikatika kwa sababu ya Ulevi na zinaa.
Vipi wewe nini kilikufanya usifikie, na maisha yako hapo kitaa kwa sasa yanaendeleaje?