Nini kilimfanya Benjamin Mkapa ashindwe kuchapa Taazia ya muasisi wa TANU Abdul Sykes katika magazeti ya chama?

Ninakubali mkuu lakini nikisoma Historia na ya kutafuta mwenyewe ni kwamba wakuja hao waliweza tu kuchungulia fursa maana toka Sykes alipoletwa Dar toka Pangani na Effendi Plantan walijiunga kwenye kundi la Wakuja ambalo lilikuwa linajikomba kwa Wahindi.

Tofauti na wenzao kama Kilwa Association au lile kundi la Wasukuma na Wanyamwezi ambao walikuwa wanataka haki ya weusi.
 
Wapi na lini Askari Mamluki ageuke Mzalendo na Mpigania Uhuru na akumbukwe kwenye historia ya nchi?
Si unajua upole wetu hatujaanza leo ndio maana Mgeni anaweza kuja Tanzania na akatamba sana akatufanya anavyojua. Wazulu na Wanubi walikuwa wanajiona wao ndio wao hapo Kariakoo wanajiweka kundi moja na Waarabu na Wahindi na timu yao Sunderland
 
Mwalimu wangu Sheikh Mohammed Said nimekusoma mahali ukieleza kutaka kuweka tazia ya MwanaMapinduzi na katibu mkuu wa Kwanza wa Afro Shiraz Sheikh Thabit Kombo.

Tafadhali naomba uiweke hapa kwa faida ya baraza.
 
Red...
Ikiwa unafikiri hivyo ni sawa.

Muhimu kwangu ni kuwa nimewapa watu nafasi ya kusoma historia ambayo wengi hawakuwa wanajua kuwa ipo.

Naamini wewe umejifunza mengi hapa jamvini.
Umelisha watu tangu pori kuwa nyerere alipokelewa na abdul.. ndio kutuamini hayo mengine.. wewe ungejikita kuandika kuhusu wazee wako na sio menginenyo.
 
Akishikwa urongo huanza kujitapa mara cambridge mara harvard nakutokujibu hoja husika
 
Mwalimu wangu Sheikh Mohammed Said nimekusoma mahali ukieleza kutaka kuweka tazia ya MwanaMapinduzi na katibu mkuu wa Kwanza wa Afro Shiraz Sheikh Thabit Kombo.

Tafadhali naomba uiweke hapa kwa faida ya baraza.
Thomas...
Ile taazia haifai kuwekwa hapa kwa kuwa muandishi Mlamali Adam alikuwa mkali kwake.
 
Akishikwa urongo huanza kujitapa mara cambridge mara harvard nakutokujibu hoja husika
Inside10,
Hawa Harvard na Cambridge ndivyo vyuo ambavyo ikiwa patatokea elimu mpya wao huitaka kujua kuna kipi kipya.

Kwa kuwa nilikuja na elimu mpya ndiyo wakanifikia si kuwa mimi nimejitapa hapana ni kile kitabu cha Abdul Sykes ndicho kilichowavutia lakini ni miaka mingi imepita.
 
Si unajua upole wetu hatujaanza leo ndio maana Mgeni anaweza kuja Tanzania na akatamba sana akatufanya anavyojua. Wazulu na Wanubi walikuwa wanajiona wao ndio wao hapo Kariakoo wanajiweka kundi moja na Waarabu na Wahindi na timu yao Sunderland
Mtochoro,
Babu yangu Salum Abdallah ni kizazi cha kwanza cha Mmanyema aliyeingia Tanganyika kama mamluki kutoka Belgian Congo.

Babu yangu ameshiriki kuongoza migomo mitatu dhidi ya Waingereza 1947, 1949 na 1960 pia kashiriki katika kuunda Tanganyika Railways African Union (TRAU)1955.

Kuwa yeye baba yake alitokea Congo hakukumzuia kupigania uhuru wa Tanganyika.
 
Hakika ww ni bingwa wa kusamabaratisha harakati za tandamti na aggrey
 
Hakika ww ni bingwa wa kusamabaratisha harakati za tandamti na aggrey
Inside,
Ikiwa umepima mjadala huu na umeona mimi nimesambaratishwa ni vizuri hapana neno ila ningependa kukufahamisha kuwa kuna vipindi 9 vitarushwa In Shaa Allah kwa njia ya video kuhusu historia hii.

Kipindi # 1 hicho kipo mtandaoni na kimevutia watazamaji wengi kuliko tulivyotazamia.
 
Nguruvi3 angekubali kuonekana ni vyema mngefanya mnakasha wa laivu.. hakika ungepat aaibu KUU
 
Nguruvi3 angekubali kuonekana ni vyema mngefanya mnakasha wa laivu.. hakika ungepat aaibu KUU
Inside,
Sasa mimi nifanye mjadala na yeyote kwa kutafuta kitu gani?

Kama kitabu ndicho hicho tunakwenda toleo la 4.

Wasomaji wamekipenda kitabu.
 
Wanajamvi,
Abdul Sykes hakuwahi kufanya mkutano wa hadhara popote pale nje ya Tandamti na kidongo chekundu
Na huo ndio ukweli mchungu kuwa...
  • Hakuna ushahidi wowote kwamba Abdulwahid Sykes aliwahi kuchaguliwa kuiongoza TANU tangu kuasisiwa kwake hadi uhuru unapatikana.
  • Hakuna ushahidi wowote kwamba Abdulwahid Sykes, aliwahi kusimama jukwaani akiinadi TANU tangu kuasisiwa kwake hadi uhuru unapopatikana.
  • Hakuna ushahidi wowote kwamba Abdulwahid Sykes aliwahi kuwa kiongozi wa juu wa TANU katika ngazi ya taifa, Jimbo, Wilaya hadi Kata (pamoja na mtaa wa Gerezani)
Ila ziko kumbukumbu ya Abdulwahid Sykes katika mambo matatu...
  • Kujitwalia madaraka kimabavu baada ya kuvamia ofisi za TAA mwaka 1948 na kuwatimua wazee wake kwa ngumi na mateke.
  • Kama mtoto wa mjini kuwania uongozi wa TANU mwaka 1953 akipimana nguvu na wakuja na kugalagazwa vibaya na Mwl. Nyerere.
  • Kumlisha mpwa wake hizi porojo za kuwataka Watanganyika kuwaenzi hawa walowezi kwamba ndio waliopigania uhuru wa taifa lao.
Inasikitisha kuwaona baadhi ya Watanzania wanameza hizi ngano za Mohamed Said akiitumia dini kama kinga kuficha ukweli wa historia ya Wazalendo waliojitoa mhanga kutetea maslahi ya Watanganyika dhidi ya Wakoloni.

Wengi anaowatajataja Mohamed Said kuwa walipigania uhuru wa Tanganyika hawakuwa wazawa nyakati hizo na ama walikuwa ni walowezi au askari wa Wakoloni waliokodiwa kutoka sehemu mbali mbali barani Afrika.

Mohamed Said anafanya hivyo akiamini kuwa uongo ukirudiwarudiwa siku nenda rudi kuna siku (over our dead bodies) unaweza kugeuka ukawa ukweli na miongoni mwa wazee wake wazawa wa iliyokuwa Tangayika ni wachache sana.

Mohamed Said hataki katakata kumpa heshima stahiki mwanzilishi, kiongozi na Rais muasisi wa AA mwaka 1929, msomi Mwl Cecil Matola, Mtanganyika, Mkristo na Myao moja ya makabila mahiri ya kusini mwa Tanzania.

Mohamed Said hamtaji kabisa, msaidizi wa Rais wa AA aliyepokea kijiti baada kifo cha ghafla cha Mwl Cecil Mtola na huyo si mwingine bali ni Ramadhani Ali , Mfanyabiashara, Muislaam na Mtanganyika kutoka kabila la Wazaramo.

Badala yake Mohamed Said kwa hila na makusudi na akijua fika anaeneza uongo, anadai muasisi wa AA alikuwa baba yake Abdulwahid Sykes, Kleist Sykes askari wa Wakoloni kutoka Afrika Kusini wa kabila ya Wazulu.

Hivyo hivyo Mohamed Said hampi umuhimu wowote mwanzilishi na Rais muasisi wa TAA mwaka 1948, msomi Dr Vedasto Kyaruzi, Mtanganyika, Mhaya ambaye ilibidi apewe uhamisho kutoka jijini Dar ili atengwe na wenziye.

Badala yake Mohamed Said anatutaka tumpe hashima zote mjomba na mtoto wa Kleist Sykes, Abdulwahid Sykes, Mzulu na askari wa KAR kama muasisi wa TAA, kisa? Kuwatimua wazee wake ofisini kwa ngumi na mateke.

Hivyo hivyo Mohamed Said hataki kumpa heshima stahiki Mtanganyika na msomi Dr. Julius Nyerere, Rais muasisi wa TANU na Baba wa Taifa aliyetuunganisha Watanganyika kwa umoja na mshikamano hadi tukapata uhuru mwaka 1961.

Badala yake Mohamed Said anataka tumuenzi mlowezi kutoka Afrika Kusini kwamba bila yeye TANU haingeasisiwa na madai ya uhuru yasingefanikiwa...shame, shame, shame kwa Mohamed Said na wote wanaomeza hizi porojo zake.

Hata hivyo nampongeza Mohamed Said kwani katengeneza sana hela na hizi porojo zake na kawateka wengi kweli kweli. Sasa naomba aeleze bayana ni kwa nini baada ya vita hawa Wazulu wakaamua kulowea Tanganyika.
 
Mag...
Raha niipatayo ninaposoma huu uchambuzi ni huu.

Kwa miaka mingi mlikuwa mkisomeshwa historia siyo na mkawa kimya pengine ukimya wenu ni kutokana na kutoijua historia ya kweli.

Nimeandika kitabu nimeisahihisha historia yote.
Baada ya kusoma kitabu changu mnanishambulia.

Ilikuwaje miaka yote mkawa kimya?
Juu ya hayo yote mimi sina tatizo na fikra zenu.
 
Mohamed Said, wewe umesimuliwa na sana sana umesimuliwa na mjomba kibarazani. Sisi wengine mengi ya haya tumeyashuhudia, hatukusimuliwa kama wewe. Sasa nakuambia, mengi ni uongo. Uongo umekupa kula yako, endelea kuwadanganya lakini kaa chonjo usije ukatia mkate wako mchanga, umri unakwenda.
 
Poise,
Maiti hazitaabiki kwa kufanyiwa tabaruku.

Somo la historia ni somo linalovutia sana.

Nimepongezwa na watu wengi sana kwa video hiyo.

Bahati mbaya sana wewe inakutaabisha.
Una matusi ya rejareja na dharau kubwa sana we Mzee Mzushi

Nimekuelewa ulivyocomment hapa kwenye maandishi ya Poise na nimegundua umemtusi vibaya sana Poise labda yeye hajatafakari maneno hayo
 
Come on! Mo '' two wrongs don't make a right''
Kitabu chako ni sehemu tu ya vitabu hakifanyi ulichoandika kuwa sahihi.

Tumekuonyesha matundu, na moja ni hili la Abdul Kumpokea Nyerere Dar es Salaa, bahti mbaya Profesa Shivji na Pro Saida walighafilikiwa na sasa unawatumia kufanya ''justification'' bila kujua walinukuu hoja zako.

Kwahiyo maisha ya vitabu viwili, chako na cha Prof Shivji ni ''symbiotically''

Kwamba, Prof na wenzake walipokea hoja ya Nyerere kutoka kwako, na wewe unawatumia kama Maprofesa kuthibitisha hoja. Tatizo ni umri wa kitabu na utetezi.

Pili, Mag3 kaweka hoja, sasa wewe uliyesoma makabrasha zitetee hoja zako.

Uwepo wa kitabu kingine chochote hauwezi kutetea hoja za kitabu chako.
Kwani kuna tatizo gani ukisimama katika kitabu chako na kukitetea kwa hoja?

Tatu, wapi Abdul Sykes alisimama na kuhutubia mkutano nje ya Tandamti, Kipata na Agrey ?

Jambo la muhimu sana kwa Watanzania si ukombozi wa Wazulu.

Wazulu wanatakiwa WAOMBE radhi kwa kuwa mamluki dhidi ya Wazalendo , halafu waombe radhi Waislam kwa unyama waliowatendea. Hakuna mahali Kleist au Abdul Sykes wameomba radhi

Kwavile wamepewa nishani ya Uhuru, nishani hiyo pia inakuja na kuwajibika.

Ni wito sasa kwa Familia ya Sykes ijitokeze na kuomba Watanzania radhi , kisha Waislam kwa unyama walioutenda.

Familia ya Sykes iombe radhi kwa unyama uliofanywa na wazazi wao kwa Watanganyika na Waislam.
 
Nguruvi...
Kama ninavyokueleza kila siku kuwa mimi sina tatizo na sihangaiki.

Kitabu kipo sokoni sasa mwaka wa 22 na tunakwenda toleo la 4.
Wiki hii umeniona niko hewani kufanya series za historia hii vipindi 10.

Unahitaji ushahidi gani zaidi ya huu kukithibitishia kuwa historia hii imewavutia wasomaji wengi?

Kitabu changu hakijapata kuwa sehemu ya kitabu chochote.
Hiki ni kitabu cha pekee sana.

Sasa tumetoka katika kitabu tumehamia kwenye documentary.
Namshukuru Mungu.

Maktaba yangu ni kati ya maktaba tatu bora zilizohifadhi historia ya Julius Nyerere.
Hili sikusema mimi wamesema walioandika Wasifu wa Julius Nyerere.

Mimi wakati naandika kitabu cha Abdul Sykes sikuwaza hata kwa mbali kama kitanifikisha hapa.

Hivi unajua publishers wangapi wananitafuta?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…