Nini kilimfanya Benjamin Mkapa ashindwe kuchapa Taazia ya muasisi wa TANU Abdul Sykes katika magazeti ya chama?

Nini kilimfanya Benjamin Mkapa ashindwe kuchapa Taazia ya muasisi wa TANU Abdul Sykes katika magazeti ya chama?

Wewe ni mjukuu na zao halisi la Mwalimu, Mohamed Said ni mjukuu na zao halisi la Abdul Sykes. Mjukuu wa Mwalimu unaupiga nwingi, unaitetea legasi yake vizuri sana, huwapi nafasi wajukuu wa Sykes kuidogosha historia na mchango wake mkuu sana kulisimamisha taifa hili lilivyo leo.
Mohamed ana sifa moja kubwa miongoni mwa nyingi.
Ni mtu anayejua kuipeleka hadhra aliyoikusudia kule anakotaka.
Katika kufanisha mipango yake iwe kwa uzuri au ubaya kutegemea hoja, Mohamed hurudi jambo hata mara 1000. Mzee Said anafahamu, kurudia rudia uongo mara nyingi hugeuka kuwa ukweli.
Soma hapa chini
Kwa mtu anayesoma vitu juu juu, au asiye na ufahamu wa kina na mada au mwenye upungufu tu wa kibinadamu wa kuelewa, hoja ya Mohamed inasomeka tofauti lakini kwa mtazamo wa kusudio lake.

Msomaji ataamini kuwa Nyerere alitoka Butiama na kufikia kwa Abdul Sykes.
Na kwamba ujio wa Nyerere ilikuwa zao la juhudi za Abdul Sykes.
Hapo Mohamed atakuwa tayari amempa 'mbwa jina baya ili amuue''

Hapa ieleweke suala si uhusiano wa Nyerere na Abdul unaopingwa.
Nyerere alifika Dar es Salaam kwa mara ya kwanza katika mkutano mwaka 1948 akitokea Tabora.

Baadaye Nyerere alikuja Dar kufundisha kama Mwalimu kule Pugu.

Alipoacha kazi ya Ualimu ndipo alipokwenda kuishi na Abdul

Mohamed hawezi kukueleza mahusiano ya kufahamiana japo kwa juu juu kati ya Nyerere na Abdul

Atakachokueleza ni Nyerere kuishi kwa Abdul na atarudia mara 1000 na inageuka kuwa ''ukweli ''

Tumemueleza Mohamed, haiwezekani Chama kikawa na makao makuu Dar es Salaam chini ya Abdul Kleist Syke Mbuwane, na mwenyekiti huyo asitambue uwepo wa tawi kubwa sana la Tabora likiongozwa na katibu Nyerere.

Haiwezekani kwamba Nyerere alizuka mwaka 1948 kuja katika mkutano ambao watu hawamjui na wala hawakutaka kumjua baada ya hapo.

Ikiwa ni hivyo huyu Abdul atakuwa kiongozi Mpumbavu sana.
Abdul hakuwa mpumbavu! wa kutambua wasomi wachache sana enzi hizo Nyerere akiwa miongoni!

Na ikiwa ilitokea haitakuwa ajabu, Abdul alikuwa Askari na aliwahi kuwafurumusha kwa makonde baba zake katika mapinduzi ya chama, seuse kumtambua Nyerere!

Sina tatizo na mtazamo wa Mohamed wala historia yake.

Nina tatizo na jinsi anavyotumia kalamu yake kuudurusu uongo mara 100 hata kuufanya uwe ukweli kwa sababu rahisi tu '' ukitaka kumuu mbwa mpe jina baya'' na hapa Nyerere hakwepi jina.

Masalaam, narudi viungani kuokota kumbaa !

JokaKuu Pascal Mayalla Mag3
 
Wewe ni mjukuu na zao halisi la Mwalimu, Mohamed Said ni mjukuu na zao halisi la Abdul Sykes. Mjukuu wa Mwalimu unaupiga nwingi, unaitetea legasi yake vizuri sana, huwapi nafasi wajukuu wa Sykes kuidogosha historia na mchango wake mkuu sana kulisimamisha taifa hili lilivyo leo.
Yoda,
Mimi ni mtoto kwa Abdul Sykes kwani yeye na baba yangu Said Salum ni rika moja.

Kleist Sykes ni babu yangu alikuwa rafiki na jirani wa babu yangu Salum Abdallah Mtaa wa Kipata katika miaka ya 1920.

Legasi ya Mwalimu itasimamishwa kwa matendo yake mwenyewe wala si kwa kutetewa na mtu.

Hii ndiyo ilikuwa hoja ya Prof. Haroub Othman alipomwambia Mwalimu kuwa kitabu cha Sheikh Ali Muhsin Barwan, ''Conflict and Harmony in Zanzibar,'' (1997) na kitabu cha Mohamed Said, ''The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism,'' (1998) vimeathiri legasi yake pakubwa.

Sijamdogosha yeyote katika kuandika historia ya wazee wangu si kwa maneno halisi au kwa mafumbo.

Nimeiandika historia ya TANU kama ilivyokuwa.

Kubwa linalowakera wengi ni mchango wa wazee wangu hawa katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Historia yao hii ilifutwa mimi nimeiandika na leo tunayo pamoja na sisi na inasomwa sasa mwaka wa 24.

1648497518818.png
 
Mkapa kama mwandishi bila shaka alijua uzito wa stori iliyokuwa mbele yake na pengine kwa kufahamu uhusiano wa Abdul na Nyerere alimtaka Nyerere mwenyewe amwandikie rafiki yake taazia kwa mkono wake au amhoji (exclusive interview).
Hapa unaonyesha huna uhakika Sana.
Yawezekana kuwa Mkapa aliyataka yote haya kwa Mwalimu na yeye akakataa?

Hapa ndipo panapoumiza kichwa.

Kuamini kuwa Mkapa kwa kutaka kwake tu aliamua kupuuza kifo cha Abdul Sykes huu ni muhali mkubwa sana.
Nini kilisukuma kuwaza haya kuhusu Marehemu Mkapa ?

Kwani ilikuwa ni lazima kwa Mkapa kuandika kuhusu Abdul Sykes ilihali waandishi wengine walishaandika wasifu wa Abdul Sykes na kuchapwa kwenye magazeti ?
 
Hapa unaonyesha huna uhakika Sana.

Nini kilisukuma kuwaza haya kuhusu Marehemu Mkapa ?

Kwani ilikuwa ni lazima kwa Mkapa kuandika kuhusu Abdul Sykes ilihali waandishi wengine walishaandika wasifu wa Abdul Sykes na kuchapwa kwenye magazeti ?
Proved,
Nyinyi hamkuwapo wala hamkuwajua watu hawa.

Sisi ni wazee wetu tunawajua vizuri na tunaijua Dar es Salaam ilivyokuwa miaka ile angalau tulikuwa wadogo.

Watu wa Dar es Salaam wamemjua Nyerere kwa mara ya kwanza wakimuona yuko na Abdul Sykes.

Harakati za kuunda TANU kudai uhuru zinapamba moto watu wanamuona Nyerere na Abdul Sykes nyumbani kwake au ofisini kwa Market Master, Kariakoo.

Hapo jiulize mwenyewe katika miaka hiyo nani aliyekuwa anampa umaarufu mwezake?

Abdul ndiye anayemfanya Nyerere apate umaarufu ajulikane Dar es Salaam au Nyerere ndiye anaempa Abdul umaarufu?

Haiwezekani kuwa Nyerere alikuwa haijui nguvu hii iliyokuwa imemzunguka mjini Dar es Salaam na ndani ya chama cha TANU.

Inawezekana vipi Abdul afariki na magazeti ya TANU The Ntionalist na Uhuru yampuuze yasiandike taazia yake?

Unadhani nani alistahili kuandika taazia ile?
Joseph Kasela Bantu aliyempeleka Nyerere nyumbani kwa Abdul Sykes?

Brendon Grimsshaw Mhariri wa Tanganyika Standard ndiye aliandika taazia ya Abdul Sykes.

Magazeti ya TANU hayakuandika chochote ila taarifa kuwa Julius Nyerere amehudhuria maziko ya Abdul Sykes.

Hapakuwa na cha zaidi.
Mwaka wa 1968 magazeti yalikuwa hayo ya TANU na Tanganyika Standard la Waingereza.

Aisha ''Daisy'' Sykes alikuwa bint mdogo mwanafunzi wa University of East Africa, Dar es Salaam na kauona udugu uliokuwapo baina ya baba yake na Nyerere.

Daisy akaamua kuandika kitabu lakini mwalimu wake wa historia John Iliffe akamkataza akamwambia asubiri kwanza suala hilo linahitaji kupewa muda.

Daisy hakupata tena kuandika kitabu hicho.

1648499988135.png

Daisy akiwa ameshika kitabu cha Abdul Sykes
 
Hapo jiuize mwenyewe katika miaka hiyo nani aliyekuwa anampa umaarufu mwezake?
Abdul ndiye anayemfanya Nyerere apate umaarufu au Nyerere ndiye anaempa Abdul umaarufu?


Kuna wadau wameandika humu kwamba Mwl alikuwa katibu wa TAA tawi la Tabora na aliwahi kufika Dar mwaka 1948 kwenye mkutano wa TAA.

Mpaka hapo si alikuwa maarufu miongoni mwa Viongozi wa TAA ikiwemo Abdul, kwanini ionekane kwamba Abdul ndio kampa umaarufu Nyerere ?

Mpaka Mwl anamshinda Abdul kwenye uchaguzi wa TAA baadae, ina maana bado hakuwa maarufu ?, Au alipendelewa tu na wajumbe ?


Watu wa Dar es Salaam wamemjua Nyerere kwa mara ya kwanza wakimuona yuko na Abdul Sykes.
Unazungumzia Viongozi wa TAA au raia wa kawaida ?
 
Kuna wadau wameandika humu kwamba Mwl alikuwa katibu wa TAA tawi la Tabora na aliwahi kufika Dar mwaka 1948 kwenye mkutano wa TAA.

Mpaka hapo si alikuwa maarufu miongoni mwa Viongozi wa TAA ikiwemo Abdul, kwanini ionekane kwamba Abdul ndio kampa umaarufu Nyerere ?

Mpaka Mwl anamshinda Abdul kwenye uchaguzi wa TAA baadae, ina maana bado hakuwa maarufu ?, Au alipendelewa tu na wajumbe ?



Unazungumzia Viongozi wa TAA au raia wa kawaida ?
Proved,
Unahitaji kuijua historia yote ya African Association kama ilivyokuwa Tabora ili upime mwenyewe:

''Tabora ilianza kushiriki katika siasa mwaka 1945 wakati African Association ilipoingizwa mjini Tabora kutoka Dodoma kutokana na juhudi za Edward Mwangosi.

Tabora kwenyewe msukumo wa katika kuanzisha chama cha Waafrika zilitoka kutoka Combine Dancing Club, kilabu kilichoanzishwa na vijana wa pale mjini kwa ajili ya kujifurahisha.

Wanachama mashuhuri wa kilabu hiyo walikuwa ndugu wawili Wamanyema - Maulid na Abdallah Kivuruga, Chamngíanda Usingizi, Ramadhani Nasibu, Rashid Mussa, Issa Kibira, Hamis Wabeba, Mwinyi Khatib Hemed, Swedi Juma, Issa Hamis Pama na Rajab Kanyama.

Wanachama wengi wa kilabu hii walikuwa Wamanyema, kizazi cha pili baba zao wakiwa wametokea ile iliyokuwa wakati huo Belgian Congo, wakafanya maskani Kigoma, Ujiji na Tabora mwishoni mwa karne ya kumi na tisa.

Wamanyema likiwa kabila la Waislam watupu ilikuwa rahisi kuungana kama kikundi cha kabila moja na kuanzisha chama cha siasa.

Kwa hiyo Combine Dancing Club kidogo kidogo ilijigeuza kutoka chama cha starehe na kuwa chama cha siasa.

Kumbukumbu za kikoloni zinaonyesha kwamba kamati ndogo ndani ya kilabu iliundwa katika mwaka 1945, Mwinyi Khatibu Hemed, Mzigua kutoka Bweni, Pangani, akiwa katibu.

Hemed aliandika barua makao makuu ya African Association mjini Dar es Salaam kuujulisha uongozi juu ya dhamira ya kufungua tawi mjini Tabora.

Tarehe 3 Machi, 1945 African Association mjini Tabora ilifungua ofisi yake ikiwa na na viongozi wafuatao: Hamisi Simbe (Rais), Ramadhani Nasibu (Makamu wa Rais), M. K. Hemed (katibu), Chamngíanda Usingizi (Mwenyekiti), Fimbo Mtwana (Mweka Hazina) na Rashidi Mussa (Mkaguzi wa Hesabu).

African Association, kama ilivyokuwa asili ya kilabu iliyotokana nayo, ilishikwa na Wamanyema.

Hivi ndivyo Wamanyema walivyokuja kuongoza siasa Tanganyika.

Julius Nyerere, wakati huo akifundisha St. Maryís School, alishuhudia sherehe za uzinduzi wa African Association.

Nyerere hakutambua hata kidogo wakati huo kuwa alikuwa akishuhudia sehemu ya historia kazi yake mwenyewe ikijifungua mbele ya macho yake.

Mwaka 1946 wasomi wa Makerere walianza kujishughulisha na African Association pale Hamza Mwapachu na Julius Nyerere walipochaguliwa Katibu na Katibu Msaidizi na nafasi nyingine za uongozi zikishikwa na Wamanyema.

Baada ya uhamisho wa Mwapachu kutoka Tabora, Nyerere akashika nafasi yake na kuwa katibu wa chama. Mwaka huo huo Nyerere alisafiri kwenda Dar es Salaam kama mjumbe wa Tabora kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa African Association.

Katika mkutano huu ndiyo kwa mara ya kwanza Dossa Aziz alimtia Nyerere machoni.

Lakini urafiki baina ya Dossa na Nyerere haukushamiri hadi mwaka 1952, Nyerere alipokuja Dar es Salaam na kuungana na wazalendo wengine.''

(Kutoka kitabu cha Abdul Sykes)

Katibu wa AA alikuwa Hamza Mwapachu, Nyerere alikuwa Katibu Msaidizi.
Alipoondoka Mwapachu Tabora ndipo Nyerere akashika nafasi hiyo.

Kuhusu Nyerere kushinda uchaguzi wa 1953 dhidi ya Abdul Sykes nimeeleza kuwa Hamza Mwapachu, Abdul Sykes na Ali Mwinyi Tambwe walifanya mkutano nyumbani kwa Mwapachu Nansio, Ukerewe kuhusu kumtia Nyerere katika uongozi wa TAA na 1954 TANU iundwe.

Tatizo lilikuwa Nyerere vipi atamshinda Abdul Sykes Dar es Salaam?
Akina Sykes walikuwa na nguvu sana.

Nyerere alikuwa mgeni hakuna aliyekuwa anamjua.

Uamuzi ukawa Abdul amsaidie Nyerere apate kuchukua nafasi hiyo ili yeye akabidhiwe jukumu la kuongoza mapambano ya kudai uhuru.

Mwapachu hakutaka Abdul aongoze mapambano ya kudai uhuru kwa kuwa hakutaka ionekane TANU kama vuguvugu la Waislam dhidi ya Waingereza.

Hii ndiyo sababu Abdul alimtaka Chief David Kidaha Makwaia aje TAA wamchague Rais kisha waunde TANU mwaka unaofuatia na Chief Kidaha aongoze harakati za kudai uhuru.

Historia hii nieieleza kwa kirefu katika kitabu cha Abdul Sykes.

Muhimu hapa ni kuwa fikra ya kuunda TANU iko kati ya Hamza Mwapachu na Abdul Sykes miaka mingi nyuma.

Huulizwa maswali mengi sana katika haya.

Je, Nyerere alikuwa anajua historia hii au hakuwa anaijua na ndiyo maana amekuwa kimya kuhusu vipi alikuja kuongoza TANU?

Au hakuwa anajua ndiyo sababu hakupata kumwadhimisha Hamza Mwapachu au Abdul Sykes?

1648503921362.png

Chief David Kidaha Makwaia
 
Thanks God, Mkuu Maalim Mohammed Said ni mtu mwerevu anayejua vyema kusoma nyakati, anamjua vizuri JPM, naamini anazijua vyema sababu zilizopelekea "wale jamaa" waendelee kuhifadhiwa kule 'mahali salama', hivyo tangu baada ya kumtolea angalizo lile, sasa yuko makini kwa kupunguza kuipush ile agenda yake ambayo ndio the motive behind most of his writings, na by the time 'jamaa' anamaliza, "if at all atamaliza", the time left will be too little too late to keep pushing his agenda forward!.

Paskali
Nje kidogo ya mada, Paskali ! hayo maneno uliandika July 31, 2020. Najiuliza sana uliona kitu gani tofauti na wengi wetu? soma ''if at all atamaliza'' .
 
Nje kidogo ya mada, Paskali ! hayo maneno uliandika July 31, 2020. Najiuliza sana uliona kitu gani tofauti na wengi wetu? soma ''if at all atamaliza'' .

Huyu jamaa wakati mwingine ana maneno ya kinabii.
 
Back
Top Bottom