Nini kilimfanya Benjamin Mkapa ashindwe kuchapa Taazia ya muasisi wa TANU Abdul Sykes katika magazeti ya chama?

Wewe ni mjukuu na zao halisi la Mwalimu, Mohamed Said ni mjukuu na zao halisi la Abdul Sykes. Mjukuu wa Mwalimu unaupiga nwingi, unaitetea legasi yake vizuri sana, huwapi nafasi wajukuu wa Sykes kuidogosha historia na mchango wake mkuu sana kulisimamisha taifa hili lilivyo leo.
 
Yoda,
Mimi ni mtoto kwa Abdul Sykes kwani yeye na baba yangu Said Salum ni rika moja.

Kleist Sykes ni babu yangu alikuwa rafiki na jirani wa babu yangu Salum Abdallah Mtaa wa Kipata katika miaka ya 1920.

Legasi ya Mwalimu itasimamishwa kwa matendo yake mwenyewe wala si kwa kutetewa na mtu.

Hii ndiyo ilikuwa hoja ya Prof. Haroub Othman alipomwambia Mwalimu kuwa kitabu cha Sheikh Ali Muhsin Barwan, ''Conflict and Harmony in Zanzibar,'' (1997) na kitabu cha Mohamed Said, ''The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism,'' (1998) vimeathiri legasi yake pakubwa.

Sijamdogosha yeyote katika kuandika historia ya wazee wangu si kwa maneno halisi au kwa mafumbo.

Nimeiandika historia ya TANU kama ilivyokuwa.

Kubwa linalowakera wengi ni mchango wa wazee wangu hawa katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Historia yao hii ilifutwa mimi nimeiandika na leo tunayo pamoja na sisi na inasomwa sasa mwaka wa 24.

 
Mkapa kama mwandishi bila shaka alijua uzito wa stori iliyokuwa mbele yake na pengine kwa kufahamu uhusiano wa Abdul na Nyerere alimtaka Nyerere mwenyewe amwandikie rafiki yake taazia kwa mkono wake au amhoji (exclusive interview).
Hapa unaonyesha huna uhakika Sana.
Yawezekana kuwa Mkapa aliyataka yote haya kwa Mwalimu na yeye akakataa?

Hapa ndipo panapoumiza kichwa.

Kuamini kuwa Mkapa kwa kutaka kwake tu aliamua kupuuza kifo cha Abdul Sykes huu ni muhali mkubwa sana.
Nini kilisukuma kuwaza haya kuhusu Marehemu Mkapa ?

Kwani ilikuwa ni lazima kwa Mkapa kuandika kuhusu Abdul Sykes ilihali waandishi wengine walishaandika wasifu wa Abdul Sykes na kuchapwa kwenye magazeti ?
 
Hapa unaonyesha huna uhakika Sana.

Nini kilisukuma kuwaza haya kuhusu Marehemu Mkapa ?

Kwani ilikuwa ni lazima kwa Mkapa kuandika kuhusu Abdul Sykes ilihali waandishi wengine walishaandika wasifu wa Abdul Sykes na kuchapwa kwenye magazeti ?
Proved,
Nyinyi hamkuwapo wala hamkuwajua watu hawa.

Sisi ni wazee wetu tunawajua vizuri na tunaijua Dar es Salaam ilivyokuwa miaka ile angalau tulikuwa wadogo.

Watu wa Dar es Salaam wamemjua Nyerere kwa mara ya kwanza wakimuona yuko na Abdul Sykes.

Harakati za kuunda TANU kudai uhuru zinapamba moto watu wanamuona Nyerere na Abdul Sykes nyumbani kwake au ofisini kwa Market Master, Kariakoo.

Hapo jiulize mwenyewe katika miaka hiyo nani aliyekuwa anampa umaarufu mwezake?

Abdul ndiye anayemfanya Nyerere apate umaarufu ajulikane Dar es Salaam au Nyerere ndiye anaempa Abdul umaarufu?

Haiwezekani kuwa Nyerere alikuwa haijui nguvu hii iliyokuwa imemzunguka mjini Dar es Salaam na ndani ya chama cha TANU.

Inawezekana vipi Abdul afariki na magazeti ya TANU The Ntionalist na Uhuru yampuuze yasiandike taazia yake?

Unadhani nani alistahili kuandika taazia ile?
Joseph Kasela Bantu aliyempeleka Nyerere nyumbani kwa Abdul Sykes?

Brendon Grimsshaw Mhariri wa Tanganyika Standard ndiye aliandika taazia ya Abdul Sykes.

Magazeti ya TANU hayakuandika chochote ila taarifa kuwa Julius Nyerere amehudhuria maziko ya Abdul Sykes.

Hapakuwa na cha zaidi.
Mwaka wa 1968 magazeti yalikuwa hayo ya TANU na Tanganyika Standard la Waingereza.

Aisha ''Daisy'' Sykes alikuwa bint mdogo mwanafunzi wa University of East Africa, Dar es Salaam na kauona udugu uliokuwapo baina ya baba yake na Nyerere.

Daisy akaamua kuandika kitabu lakini mwalimu wake wa historia John Iliffe akamkataza akamwambia asubiri kwanza suala hilo linahitaji kupewa muda.

Daisy hakupata tena kuandika kitabu hicho.


Daisy akiwa ameshika kitabu cha Abdul Sykes
 
Hapo jiuize mwenyewe katika miaka hiyo nani aliyekuwa anampa umaarufu mwezake?
Abdul ndiye anayemfanya Nyerere apate umaarufu au Nyerere ndiye anaempa Abdul umaarufu?


Kuna wadau wameandika humu kwamba Mwl alikuwa katibu wa TAA tawi la Tabora na aliwahi kufika Dar mwaka 1948 kwenye mkutano wa TAA.

Mpaka hapo si alikuwa maarufu miongoni mwa Viongozi wa TAA ikiwemo Abdul, kwanini ionekane kwamba Abdul ndio kampa umaarufu Nyerere ?

Mpaka Mwl anamshinda Abdul kwenye uchaguzi wa TAA baadae, ina maana bado hakuwa maarufu ?, Au alipendelewa tu na wajumbe ?


Watu wa Dar es Salaam wamemjua Nyerere kwa mara ya kwanza wakimuona yuko na Abdul Sykes.
Unazungumzia Viongozi wa TAA au raia wa kawaida ?
 
Proved,
Unahitaji kuijua historia yote ya African Association kama ilivyokuwa Tabora ili upime mwenyewe:

''Tabora ilianza kushiriki katika siasa mwaka 1945 wakati African Association ilipoingizwa mjini Tabora kutoka Dodoma kutokana na juhudi za Edward Mwangosi.

Tabora kwenyewe msukumo wa katika kuanzisha chama cha Waafrika zilitoka kutoka Combine Dancing Club, kilabu kilichoanzishwa na vijana wa pale mjini kwa ajili ya kujifurahisha.

Wanachama mashuhuri wa kilabu hiyo walikuwa ndugu wawili Wamanyema - Maulid na Abdallah Kivuruga, Chamngíanda Usingizi, Ramadhani Nasibu, Rashid Mussa, Issa Kibira, Hamis Wabeba, Mwinyi Khatib Hemed, Swedi Juma, Issa Hamis Pama na Rajab Kanyama.

Wanachama wengi wa kilabu hii walikuwa Wamanyema, kizazi cha pili baba zao wakiwa wametokea ile iliyokuwa wakati huo Belgian Congo, wakafanya maskani Kigoma, Ujiji na Tabora mwishoni mwa karne ya kumi na tisa.

Wamanyema likiwa kabila la Waislam watupu ilikuwa rahisi kuungana kama kikundi cha kabila moja na kuanzisha chama cha siasa.

Kwa hiyo Combine Dancing Club kidogo kidogo ilijigeuza kutoka chama cha starehe na kuwa chama cha siasa.

Kumbukumbu za kikoloni zinaonyesha kwamba kamati ndogo ndani ya kilabu iliundwa katika mwaka 1945, Mwinyi Khatibu Hemed, Mzigua kutoka Bweni, Pangani, akiwa katibu.

Hemed aliandika barua makao makuu ya African Association mjini Dar es Salaam kuujulisha uongozi juu ya dhamira ya kufungua tawi mjini Tabora.

Tarehe 3 Machi, 1945 African Association mjini Tabora ilifungua ofisi yake ikiwa na na viongozi wafuatao: Hamisi Simbe (Rais), Ramadhani Nasibu (Makamu wa Rais), M. K. Hemed (katibu), Chamngíanda Usingizi (Mwenyekiti), Fimbo Mtwana (Mweka Hazina) na Rashidi Mussa (Mkaguzi wa Hesabu).

African Association, kama ilivyokuwa asili ya kilabu iliyotokana nayo, ilishikwa na Wamanyema.

Hivi ndivyo Wamanyema walivyokuja kuongoza siasa Tanganyika.

Julius Nyerere, wakati huo akifundisha St. Maryís School, alishuhudia sherehe za uzinduzi wa African Association.

Nyerere hakutambua hata kidogo wakati huo kuwa alikuwa akishuhudia sehemu ya historia kazi yake mwenyewe ikijifungua mbele ya macho yake.

Mwaka 1946 wasomi wa Makerere walianza kujishughulisha na African Association pale Hamza Mwapachu na Julius Nyerere walipochaguliwa Katibu na Katibu Msaidizi na nafasi nyingine za uongozi zikishikwa na Wamanyema.

Baada ya uhamisho wa Mwapachu kutoka Tabora, Nyerere akashika nafasi yake na kuwa katibu wa chama. Mwaka huo huo Nyerere alisafiri kwenda Dar es Salaam kama mjumbe wa Tabora kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa African Association.

Katika mkutano huu ndiyo kwa mara ya kwanza Dossa Aziz alimtia Nyerere machoni.

Lakini urafiki baina ya Dossa na Nyerere haukushamiri hadi mwaka 1952, Nyerere alipokuja Dar es Salaam na kuungana na wazalendo wengine.''

(Kutoka kitabu cha Abdul Sykes)

Katibu wa AA alikuwa Hamza Mwapachu, Nyerere alikuwa Katibu Msaidizi.
Alipoondoka Mwapachu Tabora ndipo Nyerere akashika nafasi hiyo.

Kuhusu Nyerere kushinda uchaguzi wa 1953 dhidi ya Abdul Sykes nimeeleza kuwa Hamza Mwapachu, Abdul Sykes na Ali Mwinyi Tambwe walifanya mkutano nyumbani kwa Mwapachu Nansio, Ukerewe kuhusu kumtia Nyerere katika uongozi wa TAA na 1954 TANU iundwe.

Tatizo lilikuwa Nyerere vipi atamshinda Abdul Sykes Dar es Salaam?
Akina Sykes walikuwa na nguvu sana.

Nyerere alikuwa mgeni hakuna aliyekuwa anamjua.

Uamuzi ukawa Abdul amsaidie Nyerere apate kuchukua nafasi hiyo ili yeye akabidhiwe jukumu la kuongoza mapambano ya kudai uhuru.

Mwapachu hakutaka Abdul aongoze mapambano ya kudai uhuru kwa kuwa hakutaka ionekane TANU kama vuguvugu la Waislam dhidi ya Waingereza.

Hii ndiyo sababu Abdul alimtaka Chief David Kidaha Makwaia aje TAA wamchague Rais kisha waunde TANU mwaka unaofuatia na Chief Kidaha aongoze harakati za kudai uhuru.

Historia hii nieieleza kwa kirefu katika kitabu cha Abdul Sykes.

Muhimu hapa ni kuwa fikra ya kuunda TANU iko kati ya Hamza Mwapachu na Abdul Sykes miaka mingi nyuma.

Huulizwa maswali mengi sana katika haya.

Je, Nyerere alikuwa anajua historia hii au hakuwa anaijua na ndiyo maana amekuwa kimya kuhusu vipi alikuja kuongoza TANU?

Au hakuwa anajua ndiyo sababu hakupata kumwadhimisha Hamza Mwapachu au Abdul Sykes?


Chief David Kidaha Makwaia
 
Nje kidogo ya mada, Paskali ! hayo maneno uliandika July 31, 2020. Najiuliza sana uliona kitu gani tofauti na wengi wetu? soma ''if at all atamaliza'' .
 
Nje kidogo ya mada, Paskali ! hayo maneno uliandika July 31, 2020. Najiuliza sana uliona kitu gani tofauti na wengi wetu? soma ''if at all atamaliza'' .

Huyu jamaa wakati mwingine ana maneno ya kinabii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…