Nini kilimnyima Kikwete heshima ya kuipatia Tanzania katiba bora?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,189
Reaction score
10,375
Kama katiba pendekezwa ya Jaji Joseph Warioba ingepitishwa, Rais Jakaya Mrisho Kikwete angeingia kwenye historia ya kuiletea Tanzania katiba ya kimageuzi!

Kama hiyo katiba ingepita, ingemweka Kikwete kwenye nafasi ya kukumbukwa na vizazi vingi kama "mwanamageuzi" nchini. Ilibaki kidogo tu aipate hiyo heshima!

Nini kiliingilia huo mchakato na kupelekea Kikwete kuponyokwa na hiyo heshima?
 
Kama katiba pendekezwa ya Jaji Joseph Warioba ingepitishwa, Rais Jakaya Mrisho Kikwete angeingia kwenye historia ya kuniletea Tanzania katiba ya kimageuzi!

Chama alichokuwepo
 
Masikitiko makubwa, huenda anajutia sana japo ni ngumu sana kwa mccm kujuta!🙁🙁🙁

Alisema watakaohusika wote majina yao yangeandikwa kwa wino wa dhahabu katika historia ya nchi, bahati mbaya akakutana na vibaka njiani na akawaelewa akasahau legacy aliyokua anaijenga (huenda walimuonea wivu japo aliidaka agenda hii toka upinzani)! Kwa hili hasemeheki kamwe kutoka kwa kila mtanzania mwenye akili sawasawa
 
Kama katiba pendekezwa ya Jaji Joseph Warioba ingepitishwa, Rais Jakaya Mrisho Kikwete angeingia kwenye historia ya kuniletea Tanzania katiba ya kimageuzi!

Kama hiyo katiba ingepita, ingemweka Kikwete kwenye nafasi ya kukumbukwa na vizazi vingi kama "mwanamageuzi" nchini. Ilibaki kidogo tu aipate hiyo heshima!

Nini kiliingilia huo mchakato na kupelekea Kikwete kuponyokwa na hiyo heshima?
Angekuwa amelisadia taifa sana. Maslahi binafsi na kutokuwa na nia ya dhati kusaidia nchi yalimpoteza.
 
Mazee ya ccm yanayonufaika na mfumo wa kifisadi ndio yalizuia katiba mpya

Kikwete alipewa maelekezo kuacha kuendelea na mchakato Hana kosa lolote yule mzee lasivyo wangekuwa washa murestisha in peace ndio maana akawaachia nchi yenu!!

Shida kubwa ninayoiona ni CCM kutokuwa chama Cha siasa na kujigeuza dola

Hii nchi haitakaa ipate maendeleo chini ya Hawa nzi wa kijani!!
 
Hii kali! Rais anatishwa na kuogopa?? Pathetic
 
Mkuu, mbona unashangaa? Anayekuweka madarakani ndiye anakulisha maneno ya kuyazungumza kwenye kadamnasi.

Kwani huwaoni akina Joe Biden na Kamala wake wakizurura na teleprompter na vijimemo na notisi wakati wote wanapoongea na umma?

Yaani, wanaweza kutaka kusema kitu, lakini kitu chenyewe hakikuandikwa; hapo wanalazimika kukimezea tu kana kwamba hawakioni wala hawakijui.
 
UKAWA, CCM na JK wataisikia tu mbingu kwa wengine. Ubinafsi wao umetuondolea wananchi nafasi adimu sana ya kuwa na Katiba bora kabisa ya Wananchi.
Mbona wewe hujisemei, mkuu? Ungekuwa si mbinafsi, basi ungetoka mitaani uongoze maandamano kutwa kuchwa hadi kieleweke, katiba ipatikane. Acha kuwasingizia hao wenyewe.

Kama yeye angeweza kufanya, alikuwa na nini zaidi yako? Na wewe kama unashindwa, una nini kinachokunakisi kwake?
 
Mimi nilitimiza wajibu wangu kwa kutoa maoni kwa jopo la viongozi wa tume ya katiba waliozunguka kote nchini kukusanya maoni. Unataka niandamane ili iweje?

Mimi nilihusika kwenye kuwachagua wajumbe wa lile bunge la katiba? Nilihusika kwenye mivutano yao ya serikali mbili, au tatu?
 
Mkuu, kwa hiyo baada ya hapo ukakunja mikono yako mgongoni na kubaki kuwakodolea tu macho ya uzodoaji?

Uwezo ndipo ulipoishia? Hakuna lingine zaidi la kufanya ili kulinusuru taifa, zaidi tu ya kujilalamisha kibodini?
 
UKAWA, CCM na JK wataisikia tu mbingu kwa wengine. Ubinafsi wao umetuondolea wananchi nafasi adimu sana ya kuwa na Katiba bora kabisa ya Wananchi.

..wanaopaswa kulaumiwa ni Ccm.

..Ukawa hawakuwa na akidi ya kutosha kuzuia mchakato wa katiba mpya.

..Zoezi la kuandika Katiba pendekezwa lilikamilishwa na wajumbe wa Ccm chini ya Samuel Sitta, Samia Suluhu, na Andrew Chenge.

..Raisi Kikwete alikabidhiwa Katiba pendekezwa ambayo ilipaswa kupigiwa KURA YA MAONI.

..Sasa tujiulize, nani aliwajibika kuandaa kura ya maoni lakini hakufanya hivyo?
 
Mkuu, mbona unashangaa? Anayekuweka madarakani ndiye anakulisha maneno ya kuyazungumza kwenye kadamnasi.

Kwani huwaoni akina Joe Biden na Kamala wake wakizurura na teleprompter na vijimemo na notisi wakati wote wanapoongea na umma?

Yaani, wanaweza kutaka kusema kitu, lakini kitu chenyewe hakikuandikwa; hapo wanalazimika kukimezea tu kana kwamba hawakioni wala hawakijui.
Nashangaa ndio kwa sababu najua kawekwa na wananchi na ukishakua rais unamuogopa nani tena? Angefanya tu kibingwa tubaki tunasema alishakuwepo rais bingwa na akabadilisha historia ya nchi, hamna hero anakuwa kiurahisi, unasimiamia unachoamini no matter what! Alipoteza opportunity na naamini anaijutia hata kama hasemi! Aende kwenye matamasha ya kina shilole tu sasa kujifariji
 
Kama katiba pendekezwa ya Jaji Joseph Warioba ingepitishwa, Rais Jakaya Mrisho Kikwete angeingia kwenye historia ya kuiletea Tanzania katiba ya kimageuzi!

Kama hiyo katiba ingepita, ingemweka Kikwete kwenye nafasi ya kukumbukwa na vizazi vingi kama "mwanamageuzi" nchini. Ilibaki kidogo tu aipate hiyo heshima!

Nini kiliingilia huo mchakato na kupelekea Kikwete kuponyokwa na hiyo heshima?
Kwa faida yako nitakuambia leo kwa nini Rasimu ya Katiba ya Warioba ilitupwa. Kulikuwa na kifungu cha Marais kuwajibika kwa makosa yao watakayokuwa wamefanya wakiwa madarakani. Sasa Jakaya aliruhusu na alipokea fedha za Escrow kutoka kwa Harbinder Singh/ Rugemalira.

Wakati huo huo Andrew Chenge naye akiwa ni mnufaika wa Escrow kutoka kwa Rugemalira. Ndipo akamtonya Jakaya kuwa kama Rasimu ya Warioba itapita basi hicho kifungu cha Marais kuwajibika kwa makosa waliyofanya, basi ajiandaye kushtakiwa na kufungwa.

Jiulize kwa nini Dr Mvungi aliuliwa utapata majibu ya kwa nini mchakato ulikwama.

Ndipo Jakaya Kikwete akaelewa na kuamua kuuvuruga mchakato wa Katiba kwa kuogopa kuja kushtakiwa
 
Wewe maneno hayo kakwambia nani Kikwete au Chenge?
 
Back
Top Bottom