Nini kilimnyima Kikwete heshima ya kuipatia Tanzania katiba bora?

Nini kilimnyima Kikwete heshima ya kuipatia Tanzania katiba bora?

Kwa faida yako nitakuambia leo kwa nini Rasimu ya Katiba ya Warioba ilitupwa. Kulikuwa na kifungu cha Marais kuwajibika kwa makosa yao watakayokuwa wamefanya wakiwa madarakani. Sasa Jakaya aliruhusu na alipokea fedha za Escrow kutoka kwa Harbinder Singh/ Rugemalira.

Wakati huo huo Andrew Chenge naye akiwa ni mnufaika wa Escrow kutoka kwa Rugemalira. Ndipo akamtonya Jakaya kuwa kama Rasimu ya Warioba itapita basi hicho kifungu cha Marais kuwajibika kwa makosa waliyofanya, basi ajiandaye kushtakiwa na kufungwa.

Jiulize kwa nini Dr Mvungi aliuliwa utapata majibu ya kwa nini mchakato ulikwama.

Ndipo Jakaya Kikwete akaelewa na kuamua kuuvuruga mchakato wa Katiba kwa kuogopa kuja kushtakiwa
Kipengele kilichokwamisha katiba mpya ni Cha serikali tatu

Hicho ulichokizungumza kilitakiwa kiwekwe kipengele za kuanzia 2015
 
Mazee ya ccm yanayonufaika na mfumo wa kifisadi ndio yalizuia katiba mpya

Kikwete alipewa maelekezo kuacha kuendelea na mchakato Hana kosa lolote yule mzee lasivyo wangekuwa washa murestisha in peace ndio maana akawaachia nchi yenu!!

Shida kubwa ninayoiona ni CCM kutokuwa chama Cha siasa na kujigeuza dola

Hii nchi haitakaa ipate maendeleo chini ya Hawa nzi wa kijani!!

Yaani amiri jeshi mkuu atishwe na waimba Iyena Iyena?
Basi alikuwa rais dhaifu.

Kiufupi alikuwa na rasimu yake ya mfukoni
 
Ndio democrasia,CHADEMA waligomea.
ila kwa sasa hawa goma goma tumeshawaona akili yao,hatutokubali kuwasikiliza
 
Mkuu, kwa hiyo baada ya hapo ukakunja mikono yako mgongoni na kubaki kuwakodolea tu macho ya uzodoaji?

Uwezo ndipo ulipoishia? Hakuna lingine zaidi la kufanya ili kulinusuru taifa, zaidi tu ya kujilalamisha kibodini?
Vijana ndiyo wanaotakiwa kuleta mabadiliko. Kwa bahati mbaya nimeshapita kwenye huo umri kitambo.
 
Kama katiba pendekezwa ya Jaji Joseph Warioba ingepitishwa, Rais Jakaya Mrisho Kikwete angeingia kwenye historia ya kuiletea Tanzania katiba ya kimageuzi!

Kama hiyo katiba ingepita, ingemweka Kikwete kwenye nafasi ya kukumbukwa na vizazi vingi kama "mwanamageuzi" nchini. Ilibaki kidogo tu aipate hiyo heshima!

Nini kiliingilia huo mchakato na kupelekea Kikwete kuponyokwa na hiyo heshima?
Aliendekeza ushkaji badala ya uzalendo
 
Kama katiba pendekezwa ya Jaji Joseph Warioba ingepitishwa, Rais Jakaya Mrisho Kikwete angeingia kwenye historia ya kuiletea Tanzania katiba ya kimageuzi!

Kama hiyo katiba ingepita, ingemweka Kikwete kwenye nafasi ya kukumbukwa na vizazi vingi kama "mwanamageuzi" nchini. Ilibaki kidogo tu aipate hiyo heshima!

Nini kiliingilia huo mchakato na kupelekea Kikwete kuponyokwa na hiyo heshima?
Rais ambaye angeweza kuipatia nchi katiba mpya na bora na ya haki ni JPM TU na sababu zipo wazi kwa wenye akili ...rais anaye fanya vizuri na kukubalika sana na watu ni.rahisi kwa huyo rais kuleta katiba mpya kuliko yule ambaye akubaliki kwa sababu asiye kubalika ana kuwa na hofu wa hiyo katiba inaweza kumwaribu
 
Angetoa katiba, maana yake alikkuwa anakubali CCM iondoke madarakani. Hata yeye asingeweza kuhimili maisha bila CCM.
 
Back
Top Bottom