bigmind
JF-Expert Member
- Oct 28, 2015
- 12,457
- 12,689
Kumekuwepo na drama nyingi kuhusiana na KOROSHO, binafsi nina swali langu moja tu napenda kujibiwa na serikali au mdau yeyote anayeza maana serikali wenda wasijbu kwa kukosa majibu au kudharau chanzo cha swali.
Binafsi kama raia na mtanzania nina haki ya msingi kuuliza swali hili na kudai majibu.
SWALI:
Nini kilipelekea kupanda ghafla kwa bei ya korosho mwaka jana, na labda serikali ilihusika kwa namna yeyote na kupanda bei???
Binafsi katika kufuatilia takwimu za uzalishaji wa korosho naona Tanzania hatupo ata katika nchi 10 za mwanzo zinazozalisha korosho kwa wingi duniani.
Nigeria
Ivory cost
Vietnam
Brazili
Philippine
India
China
..........
Na nyingine, kiufupi unaweza kujiuliza Tanzania nchi ambayo iliwapa mafunzo ya kuzalisha korosho Vietnam iweje leo wawe wazalishai wakubwa huku sisi tukibakia mkiani.
Ninachotaka kusema hapa ni kuwa kinachoendelea sasa hivi ni mabishano ya kijinga kati ya serikali na wadau wa korosho kati ya serikali, wakulima na wafanya biashara. Ila sijaona kama kuna ata mmoja wapo anayejaribu kujibu swali langu hapo juu. Hapa inamanisha ata hatujui bei ya sasa ya soko la korosho duniani ikoje, na hatujajua nini kilitokea mwaka jana bei ikaenda juu ghafla.
Binafsi nilionya mwaka jana, kuwa serikali haikutakiwa kufanya harusi ya kusherekea bei ya juu ya korosho isiyojulikana imepanda kwasababu ipi, ambapo pia wakulima walinunilia hadi mbuzi na kuku soda, Nijuavyo tangia uhuru mkulima wa korosho na mazao mengine kama kahawa sijawahi kuona wakulima wakijikwamua kutokana na umasikini kutokana na kilimo cha haya mazao hasa korosho, pamba, kahawa na mengine kama tumbaku zaidi kuzidi kudidimia katika umasikini.
Ni upuuzi kukalia kulumbana na vitu ambavyo majibu yake yapo wazi, wakulima watafarijika wakijua kuwa bei ya korosho kutokana na kukokotolewa kwa mnyororo wa thamani hawataona shida kuuza bei yeyote iwapo uhalisia utajulikana.
Mfano, kalipio na mkwara wa Mh. Waziri mkuu kwa wafanya biashara/wanunuzi wa korosho ni wa kisiasa sana unaotokana na mambo mawili.
Mosi ni Uonga wa boss wake, kufuatia matukio ya mwendelezo wa sakata hili na pili ni ikanda/kisiasa nikimanisha anatafuta kuwin matakwa ya wapiga kura wake wa mikaoa ya kusini mashariki. Ila ningependa kama angetoa taarifa ya hali ya soko kwenye masoko ya kimataifa ili tujue nani hasa mchawi.
Lakini nimesoma article moja, online inaonesha uzalishaji wa korosho kwa mwaka 2015, ulikuwa mkubwa mno kwenye mataifa yanayozalisha korosho ambapo yalipelekea mavuno ya 2016 kuekelea 2017 kuwa chini/mabaya. Na hii ndiyo inahisiwa kuwa sababu ya korosho kuwa juu mwaka jana (2017). Kwa uthibitisho wa hili chunguza phenomena ya uzalishaji wa korosho kwa Tanzania hasa kwa mikoa ya mtwara, pwani na Lindi, mwaka jana mavuno yalikuwa juu mwaka huu yameenda chini na ilitokea coincidence mavuno yakaongezeka kidogo na bei ikawa juu kitu ambacho ni nadra sana kutokea kwa sector ya kilimo nchini Tanzania.
Nimalize kwa kutoa ushauri wangu kwa serikali na wadau wa Korosho na mazao mengine, hasa mhusika mkuu wizara ya kilimo na waziri wake mpya.
Kilimo lazima kiwekewe mikakati ya muda mrefu na mifupi huku wizara ikitoa ushauri wa kitaalam na kimasoko kwa wakulima. Tafiti hasa za masoko kuhusu bei za masoko ya mazao ya kilimo na bidhaa za kilimo ndani na nje ya nchi hakuna. Cha kusikitisha ni urasimu wa umangi meza wa kuruhusu sekta binafsi katika kufanya tafiti za kilimo.
Ushuhuda;
Sheria ya takwimu inatumika vibaya sana, juzi kati tulikuwa tunafanya kikiutafiti juu ya wafugaji wadogo katika mikoa ya Arusha, Mbeya na mwanza sasa wacha uone urasimu kila tukienda kuomba vibali kwanza mlolongo ni mrefu sana. Unatakiwa uanzie wizara ya kilimo, uende tamisemi, uende NBS, uende kwa mkoani, uende wilayani uende katani jamani.
Kusema kweli tutafika tukiwa tumechelewa ama hatutafika kabisa..!
Jumapili njema.