Nini kilisababisha ukaacha kuvuta bangi?

Nini kilisababisha ukaacha kuvuta bangi?

dumbi

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2018
Posts
988
Reaction score
1,542
Wakuu poleni na korona, sina mengi nataka tupeane mastory kwa wale tulowahi kutumia mmea, ndumu,kuku moshi,ganja na majina kibao siwezi kuyamaliza ili tupoteze haya mawazo ya korona.

Mimi naanza na sababu zilonifanya nikaacha na nikaweza kukaa kwa muda mrefu miaka mingi tu japo siku hizi nastua mara moja moja maana nisingeacha mpaka leo ningekuwa sijaoa.

Okey twende
1)nikivuta bangi nilikuwa nawaza mambo mengi sana mfano naweza nikamuwaza ndugu fulani au rafiki yani mwanzo tangu tumejuana yani inakuja kama movie yote tulopitia mimi nayeye na makosa yote ambayo mimi nilikuwa nayafanya ambayo mimi nilikuwa naona ni kawaida hapa ndio naona makosa na kujilaumu kwa nini nilifanya vile ,hii ilisababisha kumuonea aibu muhusika.

2)nilikuwa napenda kukaa peke yangu,niktoka mskani natamani nisikutane na mtu yeyote mpaka nafika chumbani kwangu hii ilitokana na macho yangu nikitoka kula kitu yalikuwa yanakuwa mekundu sana halafu kama yamevimba kwaiyo watu huwa walonizoea wananiuliza mbona mcho yako mekundu sana? wenyewe tuliita jicho nyanya,ukiacha macho sikuwa napenda story na watu hata kama sijala kitu ila nikivta nazidisha mpaka kumkwepa mtu nikimuona mbele yangu tusikutane.

3)nilikuwa sipendi wanawake niliwahi kukaa mwaka mzima bila kula mzigo halafu nilikuwa napendwa sana na ma dem, pamoja na kuonesha hisia zote za kunitaka lakin mimi sikuwa tayar yani kama ningeamua ilikuwa demu simtongozi na namwambia njoo sehem fulani na akija lazima nimle lakin kutokana na ndumu niliwaaacha kma walivyo mpaka wenyewe wakawa wanakata tamaa na mimi sikujali kabisa na walikuwa visu balaa dah yani mpaka sasa najilaumu yani flani sijamla?

4)hii naona ni faida ilikuwa kila siku lazima nifanye mazoezi ya kukimbia na kubeba vyuma yani kila siku ya mungu tena asubuhi na jioni ila kutokana na lishe ya kwaida sikuwa mbavu na hii ilisabishwa na kukimbia kila siku asikwambie mtu hakuna zoezi zuri kwa ajili ya mwili kama kukimbia mengine mbwembe tu kama una kitambi we kimbia kila siku utanipa majibu hata kama hakijaisha unakuwa mwepesi balaa.

5)nilikuwa siwezi kuongopa hii mpaka Leo imeniathiri japo siku hizi naongopa kwa mambo yaliyokuwa na umuhim zamani hata kama kuna jambo natakiwa niongope ili mambo yangu yaende mimi nasema kweli, hii ilisababisha baadhi ya ndugu na marafiki kunichukia na kuniita mnafiki mgombanishi kwasabu jambo ambalo mimi nilikuwepo basi siwezi kudanganya hii ilisababisha ndoa ya dada yangu kuvunjika kwasabu ya kutokuwa mwaminifu na mimi ndo siwezi kuongopa,hii story nyingine ntawachosha.

6)kuchukulia poa mambo ya umuhim,yani naweza kupewa mchongo lakin mimi nakuwa nachukilia poa naweza kusema ntaenda kesho hiyo kesho ikifika nikikakaa maskani nikila kitu basi naishia hapohapo hata kama nilishajiandaa siendi na baki kuvuta bangi tuu mpaka jion, na kesho yake hivyo hivyo labda nisile kitu nitoke moja kwa moja stand,hii ilisababisha kuchelewa kujitegemea manake fursa zilikuwa zinanipita.

6)nilikuwa naamini katika jambo moja mfano nilikuwa napenda kuimba kwahiyo juhud zangu nyingi niliziweka katika mziki tofaut na sasa naweza kufatilia mambo hata ma 4 kwa wakati mmoja litakalotiki ndo hilohilo lakin ndum ni jambo moja ukimaliza ndo nianze lingine hii ndoto ilikufa na kukatishwa tamaa na producer alochukua beat yangu pamoja na melody akawapa wasanii wakubwa tip top mimi akawa ananizungusha mpaka ikafika miezi 6 ananiambia bado anafanya remix ila simlaum sana nakumbuka aliniambia tufanye ngoma nyingine mi na bangi zangu nikamwambia nataka nyimbo yangu ileile na matusi juu,

jamaa akavurunda kisha akanipa nakumbuka siku ya kwanza alinipa empty cd, akakaa tena kama week mbili ndo aknipa lakin hakufanya remix,ngoma ya hao jamaa mpaka leo inapigwa .

nikaachana na mziki nikaacha na bangi na sasa nina family maisha yanasonga sikuweka yote mengime nimeacha kama kuna cha kujifunza chukua kama hakuna acha.

ila bangi sio mbaya kama tumavyoaminishwa kila mtu inampeleksha jinsi yeye anvyovikiria au kichwa chake mfano watu ambao nilokuwa nakula nao kaya hawana sababu nilozitaja hapo kuna mwamnangu mmoja yeye akila kaya anatongoza sana na anawagonga madem.na mchangamfu kwa kila mtu .mwingine anawaza sana biashara yake mpaka sasa ana duka kubwa sana....... na bado yupo kwenye chama.

Lete za kwako tujifunze na mimi nikumbuke vituko vingine ili vijana ambao hawatumii hii kitu wakiingia basi wajue wanaingia kwa sababu zipi au wasiingie kabisa.

Ushauri kama hujawahi kuvuta bangi achana nayo, kuna wengine wanavuta ili waonekane wahuni hawa ni wapumbavu usiingie huko.
Screenshot_20200422-192805.jpg
 
Kuna mtu alishawahi kula ugoro halafu yupo kwenye shamba la mihogo akaanza kutambaa sasa akiwa anatambaa anvyoipita mihogo anajiona yupo kasi kishenzi yani ni kama yupo kwenye gari lenye kasi kumbe anatambaa[emoji23][emoji23]
[emoji2] [emoji2] kuna vituko siku moja moja ila ukiwa understand unajua hii ndumu unaacha.
 
Ndumu ni balaa......
Jamaa mmoja alitoka na ndoo yake kavaa bukta tu mchana wa saa 7, kaenda kwenye tifutifu kachota mchanga wake kindoo kimejaa, akaulizwa wapeleka wapi huo mchanga akajibu naenda kuoga joto kali sana.
Bila shaka ndumu ilimwambia lile tifu pale ni bwawa.
 
Ndumu ni balaa......
Jamaa mmoja alitoka na ndoo yake kavaa bukta tu mchana wa saa 7, kaenda kwenye tifutifu kachota mchanga wake kindoo kimejaa, akaulizwa wapeleka wapi huo mchanga akajibu naenda kuoga joto kali sana.
Bila shaka ndumu ilimwambia lile tifu pale ni bwawa.
[emoji2] [emoji2] ila zingine watu wanatunga tu,mi nakumbuka kuna moja ilimtokea mshkaji tulikuwa tunakula vitu ilikuwa ndani sema mlango wa gheto ulikuwa mfupi ukitoka lazima uiname jamaa alivyoinama hakuinuka mpaka barabarani tunamuuliza vp mbona unatembea huku umeinama ndo akastuka.
 
Ila pombe mbaya kuliko bangi nimefanya mambo mengi ya kishezi na kikatili baada ya kuanza kunywa pombe? ambayo wakati nakula kitu nilikuwa mtu wa amani tu.sijui nani alokataza bangi akaruhusu pombe katika huu ulimwengu yaani ni kama vise versa .
 
[emoji2] [emoji2] ila zingine watu wanatunga tu,mi nakumbuka kuna moja ilimtokea mshkaji tulikuwa tunakula vitu ilikuwa ndani sema mlango wa gheto ulikuwa mfupi ukitoka lazima uiname jamaa alivyoinama hakuinuka mpaka barabarani tunamuuliza vp mbona unatembea huku umeinama ndo akastuka.
Hahahaaa hii kitu ni noma, inaweza kukuumbua hadharani aisee. Kwahiyo msingemshtua angeendelea kuinama njia nzima dah.
 
The same as applies to me kasoro number 3 kwangu ilikuwa kinyume chako.

I stopped marijuana cause ilikuwa inanifanya nakuwa paranoid most of the time
 
Mimi bado naendelea kuvuta bangi since 2001, niko kwenye ndoa huu mwaka wa tatu na tumebarikiwa mtoto mmoja, mke wangu hapendi nivute bangi tunagombana ila anaamini ganja inanifanya nitulie nyumbani, so huwa najifungia navuta na mara chache akiwa amefurahi huwa anakuja anakaa pembeni nikivuta, bangi sio mbaya tatizo ni wavuta bangi wenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
The same as applies to me kasoro number 3 kwangu ilikuwa kinyume chako.

I stopped marijuana cause ilikuwa inanifanya nakuwa paranoid most of the time
Umenikumbusha sababu nyingine mwishoni mwishon nilikuwa mtu wa hofu yani nikivuta mapigo ya moyo yanakuwa yanenda kasi halafu nakuwa na hofu hii ilisababishwa na sehem tulokuwa tuna vuta kuvamiwa na polisi mara kwa mara.kwaiyo ikawa nikilipua au nikisikia harufu mapigo ya moyo yanabadilika.
 
Mimi bado naendelea kuvuta bangi since 2001, niko kwenye ndoa huu mwaka wa tatu na tumebarikiwa mtoto mmoja, mke wangu hapendi nivute bangi tunagombana ila anaamini ganja inanifanya nitulie nyumbani, so huwa najifungia navuta na mara chache akiwa amefurahi huwa anakuja anakaa pembeni nikivuta, bangi sio mbaya tatizo ni wavuta bangi wenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kweli mkuu hata katika mahusiano mvuta bangi achepuki tofauti na mlevi wa pombe,kwanza ganja mapema tu upo home ila pombe nishwahi kulala nje siku 3
 
Back
Top Bottom