Nini kilisababisha urafiki na Besti/ Mshkaji wako kufa?

Kaka hiko sio kisasi sasa hio ni dhambi mpya
 
una nyongo kama yangu asee,kulipa kisasi mi ni kula adi bibi yake,familia yote..hahahah hapo roho kwatu.
 
Kwema team MMU?

Marafiki ni watu muhimu na wenye manufaa makubwa kwetu, japokuwa wakati mwingine anaweza kuwa kichomi akavuruga maisha yako?...
Dah mm nna bahati mbaya na marafiki waongo waongo wanapenda kujisifia wanapenda ushindani washari washamba sijui nna mkosi gani 🥹🥹

Huwa sidumu na rafiki hata miezi sita najikuta nampotezea nafanya yangu.

Hivyo sina rafiki am alone na siwataki pia naona maisha ni ya amani ikiwa hivi👋
 
Kwa upande wako nini kilisababisha urafiki wako na besti yako/mshkaji wako kufa?
Ni hiyo hiyo tu deni na sio deni mizinga tu.
Alafu mtu apige simu mara 100.
Na bahati mbaya anapiga mida mibovu ya kazi.
Mi hapo nashindwa kiukweli
 
Sijawahi kuwa na rafiki....
Maana urafiki mtego
Yonathani mwana wa sauli alimpa daudi ufalme kisa urafiki ...mwishowe akafa katika vita za daudi badaye daudi akaangamiza uzao wake
MUSIJISAHAULISHE YUDA ALIKUWA MWEKA HAZINA WA YESU
 
Aliniomba afungue mradi wa kufuga mbuzi huku nlipo kwan malisho na maji uhakika kuliko huko aliko, akaniomba kuusimamia na tukakubaliana kunlipa kila mwezi, kweli alinunua eneo, ujenz ukafanyka akaweka mbuz nikamtafutia mchungaji kaz ikaanza sasa gharama za kuendeshea mradi kama madawa, pumba, mahtaji ya mchungaji nikawa natoa mimi kwa makubaliano ikfka mwsho wa mwez atarudsha wee nlikoma na nlianza kuyumba sn kiuchumi kwan nlijikuta nahudumia mradi, nahudumia family yng nk halafu kunlipa akawa ananisumbua sn mpk tukawa tunagombana kbs mbaya zaid akawa n muongo muongo mtu anakwambia hela yako takutumia leo jion then kmy hatumi na kilichokuwa knaniuma zaid uchumi wng na wake n mbingu na ardhi yan anajiweza na nduguze wanajiweza sn ila wema wng ulinponza kbs. Nilijfunza uktaka udugu, urafk udumu msjaribu kukopeshana hela kbs.
 
Kama wewe ndo ulikua msimamizi ulishindwa nini Kuuza hao Mbuzi Kufidia pesa yako
 
Mlimalizana vipi? Ningekua mimi ndio ningepiga bei hao mbuzi.
 
Kama wewe ndo ulikua msimamizi ulishindwa nini Kuuza hao Mbuzi Kufidia pesa yako
jamaa nlikuwa namuheshmu sn sn na tulikuwa tunaaminiana sn mpk analeta mradi huku nlipo nadhan unaweza ona huo uaminifu kwng na wakati ananunua mbuz alikuwa ananitumia hela nimununulie.
 
mimi inshu zote zinahusu pesa, kudai kudaiwa. kuna mwingine mmoja sikumchangiaga pesa ya harusi huku akiamini nipo vizuri kiuchumi akati sina kitu kabisa, mwisho wa siku akaua urafiki
 
mimi inshu zote zinahusu pesa, kudai kudaiwa. kuna mwingine mmoja sikumchangiaga pesa ya harusi huku akiamini nipo vizuri kiuchumi akati sina kitu kabisa, mwisho wa siku akaua urafiki
Noma sana, hivi kwanini watu wasiww wanaoana kimya kimya tu... kama ni kufanya sherehe ziwe ni pesa zao na siyo kusumbua watu wengine
 
Tulikua marafiki sana kipindi hajapata ajira.

mwaka wa 4 sasa yuko busy hatuchekiani tena

nimekausha tu nifanye yangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…