Kwa upande wangu, mshikaji wangu tulikuwa tunaishi maeneo yanayokaribiana. Tulikuwa na utaratibu wa kuambiana kuwa nakuja maeneo ya kwenu utanikuta baa fulani. Sasa siku moja nikamwambia hivyo kuwa nipo mitaa yake hivyo atanikuta baa fulani. Mwenzangu alikuwa anajenga mahala pengine ili baada ya kumaliza ujenzi ahamie huko (sikuwa nalijua hili). Kumbe siku namwambia nipo mitaa yake, mwenzangu amehama kama wiki imepita. Ila akaniambia nimsubiri anakuja. Nilikaa hapo mpaka usiku mkubwa. Nikaondoka. Siku za baadaye nikaja sikia kuwa alihama na siku ile aliyoniweka mitaa aliyohama hakuwa mitaa hiyo. Umbali ulitusaidia kuuvunja ushikaji.