MsaeAbood, dar express, ngorika ndiyo mabasi ninayoyakumbuka yamedumu kwenye game 30+ yrs. Hood naona kama anapotea, kampuni nyingine zilibadilishwa majina na watoto baada ya wazazi kufariki au kuchoka, mfano BM kulikuwa na basi linaitwa makundi(early 90s) dar Moro.
(Mswahili pekee enzi hizo), Kilimanjaro express ni mtoto wa sawaya express enzi hizo. Akina Osaka ni watoto wa ngorika. Kusini sina kumbukumbu kama kina matema beach, kiswele, nk waliacha legacy.
Msae hayupo sasa hiviMsae
Sumry alikuja kuacha biashara ya mabasi na kulingana na maelezo yake, anasema biashara ilifika mwisho japokuwa alikuwa na mabasi 81 wakati anaifunga na akaamua kubadilisha biashara.
Hitimisho la biashara yake amelielezea katika madereva ambao amesema hawako committed na kazi wanazopewa na ni chanzo cha gari nyingi kupaki mapema.
Pili ameongelea ushindani ambao walikuwa wengi na amedai walikuwa wanashindana na mtu ambae hapigi gharama halisi za kazi, mathalan anapiga mahesabu ya diesel pekee na kufanya kazi hivyo kuumiza kwani nao itawabidi kushusha bei na amedai mpaka sasa nauli inayotumika Mbeya-Dar miaka ya 2000 takribani ni ileile.
Amesema wakati huo magari yalikuwa kidogo nafuu na ushindani haukuwa mkubwa ila sasa ni mkubwa sana na kazi ni ngumu hivyo hata mtu akichukua gari kupitia benki ni kazi sana na kiufupi hatoweza kwani basi haliwezi kuleta zaidi ya milioni 10 kwa mwezi ilhali basi la kichina kwa sasa ni milioni 360 hivyo angalau itahitajika miaka mitatu basi kulipa bila kuleta faida na hapo bado riba ya benki. Amesema kampuni zinabadilishana, inakuja mpya na wakiona changamoto wanatoka na nyingine inakuja. Amemaliza kwa kusema fursa bado ipo mtu akijipanga kwa kuleta mabasi mazuri, menejimenti nzuri na madereva wanaojielewa.
Maelezo haya aliyatoa Salum Sumry kwenye mahojiano Oktoba 2017 baada ya kuhamia kwenye kilimo kutoka kwenye biashara ya mabasi.