Nini kimejificha kwenye Uteuzi wa Dotto Biteko kuwa Naibu Waziri Mkuu? Nini maana yake kihistoria na upi mwelekeo wa Nchi baada ya Uteuzi huu?

Kweli lazima umuulize dareva why unaendesha gari uku umelewa
 
Nasubiri wakati wa kuwaapisha hao wateule mama atasema nini...tutasoma body language yake na tutajua tu...
 
Yaani niwe mkweli kuanzia kwa dr salim,Mrema hadi Biteko sijaona kitisho ulichoandika,yani nilichoona ni maoni yako wewe ambayo yanajulikana tu,zaidi nimeona neno why why,ule uhatari uliosema unauona binafsi sijauona,Sijui DIPIII WELDIII IMEINGIAJE,Yaani kwa ufupi haya ni mawazo yako na sio lazima mawazo yako yawe ndio uhalisia,endelea kupiga tu ramli
 
Hatari iliyowahi kuikumba hii nchi tangu uhuru ni ya Idd Amin TU. Tuache mbwembwe.
 
Nashukuru Kwa mchango Wako mkuu pia Hata mchangu wako nitauchukua....
 
Ulianza kwa kuponda vijana wa sasa hawajui historia na wanashinda mitandaoni tu nikajua utakuja na hizo sababu za kuteuliwa kwa Dotto Biteko sasa kumbe we mwenyewe hujui na bado unajiuliza maswali tu. Ungeweza kutoa findings zako na maoni yako bila kuwasema vijana wa sasa
 
Mkuu nimeeelza historia kuwa Mara Nyingi inapoonekana nafasi hii Ujue kuna mambo Hayako Sawa Ndani ya serikali...sijataka kusema wala kuzungumzia Mh.Doto Biteko kwa sababu Napenda sana Bado kula kwangu nikiwa na uhuru Wangu chief Sitaki kupotea kusikojulikana 🤣🤣🤣

ila ingekuwa ni enzi za Kikwete ningemwaga mchele tu
 
Katiba nyingi za nchi za Afrika, mambo mengi huwa hayawekwi wazi. Kwa hiyo kiongozi akienda kinyume ni vigumu sana kumhoji.
 
Dr Salim A. Salim alikuwa waziri wa ulinzi, na naibu waziri mkuu, wakati wa awamu ya kwanza ya mzee Mwinyi,Na sio nyerere kama watu wanavyosema

Nyerere aliwahi kuulizwa kuhusu hiki cheo Mwaka 1986 , aliulizwa, kwa nini kumeanzishwa cheo ambacho hakipo kwenye Katiba, akajibu, "Katiba haijasema awepo, wala haijakataza asiwepo..."
Kwanini jambo alifanye Mwinyi na maswali aulizwe Nyerere? Je Mwinyi alikuwa hawezi kujibu maswali? Hakuwepo? Kulitokea nini?
 
Kwanini jambo alifanye Mwinyi na maswali aulizwe Nyerere? Je Mwinyi alikuwa hawezi kujibu maswali? Hakuwepo? Kulitokea nini?
Kipindi hicho Nyerere Alikuwa Ndo Mwenyekiti wa Chama (Ukumbuke hilo) na ukumbuke Pia Nyerere ndo Alimweka Mwinyi Awe Rais Baada ya yeye Kung'atuka na mwinyi alikuwa Rais wa zanzibar kipindi hicho na makamu wa Rais Tanzania...

Na pia kipindi hicho kumbuka Chama kilikuwa Kikubwa kuliko serkali kwa sababu Ilikuwa ni mfumo wa Chama kimoja sio Sasa...So chchte atakachosema Mwenyekiti ndo hufuatwa.....

Na nakuongezea kuwa nyerere alikuwa na power sana kwa enzi ya chama kimoja ila nguvu ilipungua kiasi pale Tulipoingia kwenye Vyama vingi...
 
Kipindi hicho Nyerere Alikuwa Ndo Mwenyekiti wa Chama (Ukumbuke hilo) na ukumbuke Pia Nyerere ndo Alimweka Mwinyi Awe Rais Baada ya yeye Kung'atuka na mwinyi alikuwa Rais wa zanzibar kipindi hicho na makamu wa Rais Tanzania...
Fafanua vizuri huo mstari mimi unanichanganya
 

Hamna lolote boss, huku unaongea kwa fake I'd kisha unaonyesha tena uoga. Sasa kama una uoga wote huo, kwanini kuja kuleta uzi ambao huwezi kuweka kile unachataka tuamini unakijua?
 
Siasa za Kanda ya Ziwa zimekaa vibaya.Dotto anafahamu sana kujenga hoja!
 
Hamna lolote boss, huku unaongea kwa fake I'd kisha unaonyesha tena uoga. Sasa kama una uoga wote huo, kwanini kuja kuleta uzi ambao huwezi kuweka kile unachataka tuamini unakijua?
Mkuu sijawahi kutumia Fake ID mahali popote Hilo ni Jina langu halisi la kwenye kitambulisho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…