King Kong III
JF-Expert Member
- Oct 15, 2010
- 56,205
- 79,515
Pole sana Ommy Dimpoz kwa kuumwa.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ishukuriwe google translateWie geht es dir mein Land Mann! Ich habe in Deutschland gelebt, aber meine Sprache ist weg! grüße deine Freundinnen und genieße Sex mit deutschen Mädchen
HakikaIshukuriwe google translate
anasumbuliwa na upungufu wa kinga mwilini.Anaumwa nn??
Kweli??Anasumbuliwa na kansa ya koo
Mungu amuwekee wepesi
DaaahAumwacho sijui ila nasikia yupo huko.
Huwenda mtaro
Mhhhh,,,,,hatari sanaanasumbuliwa na upungufu wa kinga mwilini.
Anasumbuliwa na kansa ya koo
Mungu amuwekee wepesi
Ni kansa ya koo au Dysphagia.Dysphagia
Ni muda sasa hatumuoni sijui anasumbuliwa na nini?
Nasikia ni mgonjwa ila hatujui anaumwa nini
Mnaojua mtujuze
Kwan nae ni msanii ?Hata wewe hakuon
Aiseeh Mungu amponye harakaNini Kilimsibu? Mara ya mwisho Dimpoz alionekana katika harusi ya Ali Kiba akiwa katika afya njema kabisa.
Hata hivyo, ndani yake kulikuwa na kitu kilichokuwa kinamsumbua kwa muda mrefu. Hakuna aliyefahamu sana zaidi ya rafiki yake Ali Kiba.
“Katika harusi ya Kiba pale Dar es Salaam ilinitokea asubuhi wakati nimeandaliwa chai. Tulikuwa mimi, Kiba na Gavana Joho (Hassan Joho, Gavana wa Jiji la Mombasa ambaye ni rafiki mkubwa wa Dimpoz na Kiba).
“Baada ya uchunguzi madaktari waligundua kwamba, tatizo langu ni kubwa na nilipaswa kwenda Afrika Kusini kwa wataalamu zaidi. Iligundulilka kuwa ndani ya koo langu mishipa imetanuka kiasi kwamba, haiwezi kupitisha kitu chochote kwa urahisi.”
“Hicho ndio kilikuwa chanzo cha kuja hapa Afrika Kusini. Nilikuja hapa nikionekana kama nina afya njema brother, lakini badaye kilichonitokea nilichungulia kifo. Namshukuru sana Mungu aisee.
“Nilipitia vipimo mbalimbali kabla ya operesheni, lakini madaktari walinishtua zaidi baada ya kuniambia kwamba operesheni yangu ilikuwa ngumu na nusu ilikuwa uhai huku nusu nyingine ikiwa ni kifo,” anasimulia Dimpoz.
Kwanini ilikuwa ngumu? Namuuliza Dimpoz ambaye amekuwa Afrika Kusini kwa mwezi mzima sasa na hajawahi kutoka nje zaidi ya kushinda ndani kutazama runinga na kunywa lundo la dawa alizoweka mezani karibu na kochi analokaa.
“Kilichotakikiwa katika operesheni ile madaktari waliniambia kwamba, kulikuwa na njia mbili za kunifanya nirudi katika hali ya kawaida. Kwanza ni kurekebisha mishipa ileile ya koo, lakini wakanionya kwamba baadaye hali ile ingeweza kujirudia.”
“Pili, wakaniambia njia nyingine ilikuwa ni kuhamisha njia ambayo ninaitumia katika kupitisha chakula. Hii ilionekana kuwa salama zaidi. Hata hivyo, ilikuwa operesheni ndefu sana. Awali, madaktari waliniambia ingechukua saa saba, lakini ikaja kuchukua saa 10.”
“Licha ya kunichana shingoni, pia walichana sehemu kubwa ya tumbo kwa ajili ya kurekebisha. Kilichokuwa kinatakiwa kwanza ni kuhakikisha inapatikana njia ya muda ya kupitisha chakula wakati njia halisi inaondolewa. Pia kuhakikisha njia mpya ya chakula inafanya kazi vema.”
“Sikujitambua kwa zaidi ya siku saba. Nilikuwa nimewekewa nyaya katika kila kiungo changu. Nilikuwa napumulia mashine kusaidia mapafu yangu. Kila kitu kilitibuka na nilikuwa katika hali ya hatari,” anasimulia Dimpoz kwa sauti ya chini.
“Nilipozinduka sikujua nilikuwa wapi. Kwa jinsi ambavyo nilikuwa dhaifu sana, nilihisi kifo aisee. Jinsi ambavyo madaktari walivyonishughulikia nilikuwa naona kabisa maisha yangu yapo hatarini sana,” anasema Dimpoz.
Matibabu yake
Operesheni ya Dimpoz ilikuwa kubwa. Ilifanywa chini ya wataalamu wakubwa wakiongozwa na daktari wa kike, Selvie kutoka nchi ya Romania ambaye kwa mujibu wa Dimpoz walimsaka kwa kutumia mtandao wa Internet kujua ni daktari bingwa wa maradhi gani.
“Wakati tupo Mombasa tulianza kumsaka daktari kupitia mitandao ambaye atakuwa Afrika Kusini na atakuwa ni bingwa wa maradhi haya. Hapo ndipo tulipompata daktari huyu. Ameokoa maisha yangu kwa sababu ilikuwa ni operesheni ngumu lakini alikuwa anajua anachokifanya,” anasema Dimpoz.
Shukrani kwa Gavana Joho na timu yake ya menejimenti ya Rock Star inayoongozwa na Christina Moshi maarufu kama Seven, ambaye pia anamsimamia Ali Kiba. Dimpoz anataja dau kubwa ambalo limetumika kufanikiwa operesheni na makazi yake Johannesburg katika apartments za kifahari za Woems zilizopo Sandton. Inashangaza kwelikweli.
“Brother kila ukipiga hesabu ya pesa iliyotumika nadhani inafika dola za Marekani 60,000 (Sh.132 milioni). Kujuana na watu inasaidia sana brother. Hii operesheni imegharimu kiasi kikubwa cha pesa. Kitu cha muhimu ni afya tu,” anasema Dimpoz. Wakati tukiendelea na mazungumzo inaingia meseji katika simu yake kutoka kwa Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ambaye anaonyeshwa kushtushwa na afya ya Dimpoz baada ya kupata habari kutoka kwa watu wa karibu.
“Sasa hivi ndio nimejua umuhimu wa sekta ya afya. Serikali ina kazi kubwa ya kufanya aisee. Hawa jamaa wametuacha mbali sana. Nadhani kuna watu wengi wanakufa nchini kwetu kwa kukosa aina ya matibabu ambayo nimepewa hapa Afrika Kusini.
Nini kinafuata baada ya hapa? Dimpoz amepewa ofa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ambaye ni rafiki yake wa karibu kuwa atampatia mtu wa kumtazama kwa karibu zaidi akiwa Dar es salaam. Mtu ambaye ni bingwa wa masuala ya misuli. Kwa sasa damu yake haitembei vema kutokana na mwili wake kushtuka kwa kuwa, hakuzoea sana kulala kitandani kwa muda mrefu.
“Pamoja na ofa ya Makonda lakini nimefikiria kurudi kwanza Mombasa na kujiweka sawa kwa sababu kule hakutakuwa na bugudha kama Dar es salam. Baada ya hapo nikiwa fiti natarajia kutoa nyimbo tena. Unajua nilipania mwaka huu nitoe ngoma nyingi na kurudia kwa kasi baada ya Yanje kwenda vizuri. Tayari kuna nyimbo nimerekodi bado video tu. Tatizo ni hii operesheni lakini Mungu ndio ambaye anajua kila kitu,” anasema.
Ni kweli kuna watu wengi wanakufa kutokana na Huduma mbovu na umasikini we imagine hiyo milioni 132 za kitz nani atamudu?Nini Kilimsibu? Mara ya mwisho Dimpoz alionekana katika harusi ya Ali Kiba akiwa katika afya njema kabisa.

[emoji16][emoji16][emoji16]mwanaume kujisifu dimpoz ni Kama mwanaume kujisifu ana makalio makubwa, all in all pole yake apone haraka