Nini kimempata Aslay, Nyimbo zake kwa sasa zina shida gani?

Leak

JF-Expert Member
Joined
Feb 22, 2012
Posts
52,916
Reaction score
43,505
Wasalaam

Kati ya watu au wasanii wenye vipaji hapa nchini vya kuimba ni Aslay....
Aslay anao uwezo mkubwa sana tena sana...
Lakini kwa hivi karibuni muziki wake umeanza kuyumba kabisa na hata ile ladha imeanza kupotea kabisa na hata attentions ya watu kwake imepungua sana...
Bado najiuliza nini kimempata Aslay? Je ni utunzi umechokwa? Hana kipya cha kuwapa tena mashabiki?
Nani wakumsaidia Aslay na anguko hili? washauri wako hawaoni tatizo?
Wasalaam........
 
Tatizo nyimbo zake zina sound zinazofanana,melody zinafanana na hata msg zinafanana.Mimi ningemuomba ajipe likizo kidogo alafu arudi na nyimbo zinachochezeka yaani style nyingine,sio hizi kila siku kulia lia.
 
Yaelekea aliingia kwenye mziki kufuata mkumbo na sio kipaji ndicho kilichomvuta, kwa hiyo vitu vya kuiga vimekwisha ameshindwa kubuni vyake.
 
Kwa sababu habadilishi mtindo wa kuimba.Sasa masikio yamechoka.
He should spice up!
 
Waliokuwa wanambeba wamemtosa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…