changaule
JF-Expert Member
- Jan 10, 2020
- 6,039
- 10,151
Nikusahihishe kidogo. Kasema alikuwa na mpango wa kujizawadia Ferrari na rolls-Royce. Sina budi kuuweka mpango huu kapuni na kuelekeza nguvu zaidi kwenye klabu ya Simba.Kwanza niweke bayana mimi ni mshabiki (sio mpenzi) wa Simba Sports Club, mabingwa wa nchi.
Kutokana na kushabikia klabu yetu pendwa, nimejikuta nikamfuatilia (follow) Mwenyekiti wa Bodi ya Simba, Bilionea Mo Dewji.
Namfuatilia Twitter mpaka Instagram.
Baada ya mechi ya Simba na Kaiser Chief, tajiri alitupia pale Twitani kuwa Alikua ana mipango ya kujizawadia Ferrari ama Royce Rolls lakini ameamua kuachana na mipango hiyo baada ya kipigo cha mbwa mwitu pale FNB Soccer City. Akamalizia kusema Simba ni zaidi ya furaha ya binafsi.
Juzi kati akaweka video Instagram akiwa anaimba nyimbo y Tundaman.Video hiyo ilifuatiwa na video nyingine akiwa gym akijenga misuli.
Sikatai Duniani kuna matajiri wengi wenye vituko lakini sio hulka ya Mo Dewji tunayemfahamu.
Sababu ni nini? Kipigo cha Sauzi ama kuna yanayoendelea nyuma ya Pazia.
Tajiri anaonekana ana mawazo mengi. Nini Tatizo?
Hii kauli mbona inaeleweka tu kuwa kamaanisha kuwa ataweka mzigo mwingine ili kuimarisha kikosi cha Simba.
Hayo ya kufanya mazoezi na kujipost ni kwamba ukiachana na kuwa tajiri, naye ni binadamu anaishi kama wengine na pia ana feelings kama wengine walivyo. Kuna njia nyingi za kuzuia hisia. Wengine wanaamua kumsilimua mtu jambo lililo mkuta ili mradi tu kupunguza jazba. Mwingine anakunywa maji mengi mwingine pombe. Huyu kaamua kufanyia u comedy ili kupunguza panic