Nini kimempata designer wa gari za Toyota Motors Corporation?

Hivi na sisi wanunua mitumba huwa wanatusikiliza? au ndio kumpigia gitaa mbuzi?je ni wangapi huku kwetu huwa wananunua brand new zaidi ya used?
 
Wamebadilisha muundo kutokana na utafiti wa aerodynamics ili kupunguza ulaji wa mafuta wa gari na pia styling.
mfano landcruiser 200 n prado kuanzia 2008 muundo wa nyuma ulikiwa mwembamba kuliko mbele ili kuzuia resistance ya upepo. Istoshe muundo wake ulikiwa unaharibika kutokana na mataa yaliyojitokeza nje na kioo cha nyuma kuwa kidogo lakini naona hii wanaanza kurekebisha as from 2016 models.
 
Mie walicho nikera ni kuharibu sura ya rav4 ile ya zaman na kuleta hii ya sasa amabayo haina mvuto kabisaaaaaa
Yani wanaboa sana, gari inakuwa nzuri ndani nje kituko hata ukiipimp na rim kali hainogi
 
Kwani Jaguar Land Rover hawazingatii aerodynamics? Mbona Range Rover inakuwa tamu kila ikija mpya!
 
Hivi na sisi wanunua mitumba huwa wanatusikiliza? au ndio kumpigia gitaa mbuzi?je ni wangapi huku kwetu huwa wananunua brand new zaidi ya used?
sie si watumiaji wa mwisho.
 
mi kwa kweli sijaona ubaya wowote
Duh basi wewe utakuwa mpenzi wa kuendesha gari tu na si jingine.. Hivi ndio uliwahi kusema hata redio ya gari huwa huwashi maana hupendi kelele mkuu!
 
Landcruiser pana kuliko range
Hio ni kweli ila ninacho argue ni kuwa mbona gari nyengine body zinakunjwa vizuri na kuwa na muonekano wa kuvutia huku zikikidhi standards za aerodynamics? Why Toyota anafanya vibaya ku design body kwa mgongo wa aerodynamics
 
Umeona VX V8 new model lakini?
Ndio nmeiona ipo so baggy, ingawa wamejitahidi ku facelift imekuwa na muonekano mzuri zaidi ya ile ya kilimo kwanza! Ni miongoni mwa gari chache zilizobakia na mvuto kufikia sasa!
 
hizo ndio taste za leo, toyota wamechelewa sana kufika hapo, hizo ndio looks za kina lamborgini, MG, mustangs and the like, hazijaingia sokoni leo, zipo kitambo sema zilikuwa kwa class ya watu wa juu, leo hii watanzania wengi wananunua gari za mwaka 98 hadi 2007, wanaonunua gari kuanzia za 2008 ni wachache sana, wenye vipato visivyotetereka, kuagiza spare dubai kwao sio shida.
Hadi ifike 2023 ndio hizi gari zitafika tz kwa wingi, na spare zake zitakuwa mitaani kwa wingi, na ndio utakuwa unapenda sasa huo muonekano.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…