Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
Mwenyekiti wa CHADEMA na mgombea wa ubunge jimbo la Hai mhe. Freeman Aikaeli Mbowe ameonekana mara chache sana kwenye jukwaa la siasa kumnadi Mgombea wa Urais kupitia tiketi ya chama hiko.
Mpaka naandika uzi huu leo tarehe 20/09/2020 hajazindua kampeni za kutetea ubunge kwenye jimbo lake la Hai.
Wafuasi wake wamekuwa wakiamini kwamba mgombea wao yupo bega kwa bega na mgombea urais wa CHADEMA lakini jambo hilo ni gumu kuthibitisha kwani ni muda mrefu hajaonekana hadharani.
Kutokana na hulka ya CHADEMA kupenda kuzusha taharuki, inabidi sasa serikali ifuatilie alipo Mbowe ili wasije wakafanya yao kisha wakaangushia jumba bovu serikali kama kawaida yao.
Naamini wewe unaosoma uzi huu umejipanga kumpa kura yako rais Magufuli atuongoze kipindi cha pili.
Maendeleo hayana vyama