Nini kimempata Nicodemus Julius Loyore baada ya kukamatwa na watu waliojitambulisha kuwa Polisi? Yupo wapi?

Nini kimempata Nicodemus Julius Loyore baada ya kukamatwa na watu waliojitambulisha kuwa Polisi? Yupo wapi?

Salam Wakuu,

Taarifa zinasombaa ni kuwa toka Nicodemus Julius Loyore akamatwe Disemba 19 akiwa ofisini na watu waliojitambulisha kuwa polisi mpaka leo hajulikani yupo kituo gani!

Toka siku hiyo ndugu zake wanamtafuta katika vituo vya polisi bila mafanikio yoyote! Kama alikuwa na kosa alitakiwa kupelekwa mahakamani na sio kupelekwa/kufichwa kusipojulikana huku wapendwa wake wakiwa katika wakati mgumu wa kumtafuta ndugu yao.

Nicodemus siku chache zilizopita aliweka video mtandaoni akisema kuna watu wanamtisha na kumtukana pamoja na wanaharakati wengine, na kusema ikiwa atapotea/potezwa zikapita siku 40 hajapatikana basi ndugu zake wazike nguo! Je, ndio tulipofikia hapa? Halafu mnataka kurudusha mahusiano mazuri kati ya Polisi na Wananchi! Mahusiano gani?


Pia soma
~ Nicodemus amekamatwa na watu waliojitambulisha kuwa ni askari wakiwa na nguo za kiraia
~ Video ikionesha namna Nicodemus alivyokamatwa na watu waliojitambulisha kuwa ni Polisi
Dah!kashapoteza mustakabali wa maisha yake! Nchi hizi za Africa Bora ufanye tu yako maisha yaende, tofauti na hapo utaacha wanao yatima au la!
 
Huyu dogo akili hana,unajirekodi na kujipost vile!..hivi walidhani lile jambo dogo!?
Dogo alishiriki kuchoma vituo vya mwendokasi, walikuwa wanaelekea bandarini kuchoma yale matenki ya mafuta.

Alitakiwa aishi kimya kimya bila kelele, akazidiwa nguvu na uanaharakati ile video ya kuhamasisha maandamano yafanyike tarehe 19 Desemba ilimponza, alikuwa anasema bora maandamano yaanze mapema yaani tarehe 25 Desemba aliona wenzake wanachelewa sana.

Hakujua kwamba mfumo ulikuwa unamfuatilia kimya kimya.
 
Nchi haina kiongozi kwasasa, ni kuna vikundi vimegawana majukumu ya kuongoza nchi, bila kikundi kimoja kuingilia kingine, ni kama ilivyokuwa mexico kipindi cha Cartels, uyu mpaka wake ni huu, kundi hili mpaka wake ni ule. We kama waziri anazuia haya, lakini utekaji unaendelea, ukiangalia kwa umakini ni nchi ipo kwnye auto pilot yaani haina rubani, kiongozi hajulikani yuko wapi, yeye ni kujificha, wakimuulizia sana anaibukia kwenye makambi ya jeshi.
Trab na Trat ye anakwambia majogoo, madume na mabeberu wanatuonea wivu Kwa raslimali zetu. Badala ya kuliunganisha taifa yeye Yuko kwenye kuomba taarabu. Kwakweli tumepatikana.
 
Uchome miundombinu,uhamasishe uasi uachwe!?..hata ruwaichi kashindwa vumilia uasi wa malofa
Watu wanachomaanisha kama kakosea ahukumiwe kisheria sio kutekwa, na kama unatetea utekwaji ipo siku utajaa kwenye anga za kiongozi au mtu yoyote, nawewe utatekwa na hakutakuwa na wakukutetea sababu mnahalalisha kuwa jambo la kawaida, haya maisha tu ndugu. 📌
 
Watu wanachomaanisha kama kakosea ahukumiwe kisheria sio kutekwa, na kama unatetea utekwaji ipo siku utajaa kwenye anga za kiongozi au mtu yoyote, nawewe utatekwa na hakutakuwa na wakukutetea sababu mnahalalisha kuwa jambo la kawaida, haya maisha tu ndugu. 📌
Ahukumiwe kisheria na nani!?.. mhuni anashughulikiwa kihuni tu, mtatia akili
 
Salam Wakuu,

Taarifa zilizombaa ni kuwa toka Nicodemus Julius Loyore akamatwe Disemba 19 akiwa ofisini na watu waliojitambulisha kuwa Polisi, mpaka leo hajulikani yupo kituo gani!

Toka siku hiyo ndugu zake wanamtafuta katika vituo vya polisi bila mafanikio yoyote! Kama alikuwa na kosa alitakiwa kupelekwa mahakamani na sio kufichwa kusipojulikana huku ndugu zake wakiwa katika wakati mgumu wa kumtafuta.

Siku chache kabla, Nicodemus alisema kuna watu walikuwa wanamtisha na kumtukana pamoja na wanaharakati wengine, na kusema ikiwa atapotea zikapita siku 40 hajapatikana basi ndugu zake wazike nguo!

Je, ndio tulipofikia hapa? Halafu mnataka kurudusha mahusiano mazuri kati ya Polisi na Wananchi! Mahusiano gani?


Pia soma
~ Nicodemus amekamatwa na watu waliojitambulisha kuwa ni askari wakiwa na nguo za kiraia
~ Video ikionesha namna Nicodemus alivyokamatwa na watu waliojitambulisha kuwa ni Polisi
Yeye ni nani huyu? Isije ikawa ni mbinu yao wenyewe
 
Kwa shujaa huenda kilio,

Nyooote mnaomsapoti pigeni video kama yeye muweke hapa watu waone ndio tujue nanyi ni mashujaa, vinginevyo kwa mwoga huenda kicheko

Keyboard warrios wamemchuuza mwenzao sasa wanamdai humu
 
Back
Top Bottom