Nini kimemsibu Mulamula?

Nini kimemsibu Mulamula?

Sexless

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2017
Posts
23,683
Reaction score
55,898
Mulamula ametumbuliwa. Maswali ni Mengi lkn yapo mawili makubwa yaliyoaibisha nchi yetu kimataifa, yamkini yamesabishwa na makosa ya balozi zetu (zilikuwa chini ya Mulamula) kushindwa kuratibu mambo vizuri?

1. Je, ni ile kadhia ya mama kupandishwa school bus kwenye mazishi ya malkia?

2. Je, ni ile clip iliyoaibisha nchi kwa kumuonesha mama akigonga glasi na Rais Nyusi kisha akamnywesha Rais Nyusi na kunywa mwenyewe kwa glasi ileile?

Au tuhuma hizi zina ukweli?

E11362E4-9D3C-4C99-8015-AED5C3B906CE.jpeg

6C9A807E-8EA6-4C4D-B9FF-47E955D0437F.jpeg

Tuna haki ya kuuliza na kujua maana wanakula kodi na tozo zetu.
 
Kwenye glass sidhani maana pale inatakiwa wazee wa kazi waoneshe kuwa darasani hawakwenda kukariri midifinisheni.

Unakumbuka scenario ya raisi wa North korea alivyobadilishiwa kalamu chap na dada yake wakati wa kusaini mikataba fulani? Dada aliona hapa kunaweza kuwa na assassination attempt na hivyo akatumia akili za ziada ku switch kalamu
 
Duh!

Umeamua maksudi mazima kuifanya mada yako muhimu sana ikaonekana 'cheap' kwa visababu ulivyoweka kama ushahidi.

Bila shaka kuna mambo muhimu zaidi ambayo yatakuwa yanasababisha waziri kuwa kama hayupo.

Mbona hata kabla ya hayo matukio alishaonesha kama hayupo?

Hebu piga bongo zaidi.
 
Kwenye glass sidhani maana pale inatakiwa wazee wa kazi waoneshe kuwa darasani hawakwenda kukariri midifinisheni.

Unakumbuka scenario ya raisi wa North korea alivyobadilishiwa kalamu chap na dada yake wakati wa kusaini mikataba fulani? Dada aliona hapa kunaweza kuwa na assassination attempt na hivyo akatumia akili za ziada ku switch kalamu
Hayo mambo hayanihusu kabisa, pamoja na kwamba umenitaja taja mara kadhaa!
 
Kuondolewa serikalini na Kisha kurejeshwa au kutorejeshwa ni maamzi ya mwenye rungu.

Tusianze kutafuta sababu hapa, kesho anaweza pata nafasi zaidi ya hiyo tukaumbuka hapa jamvini kwa maneno ya leo.

Uzuri mama huwa anaeleza sababu za mabadiliko wakati wa uapisho, ebu tusibiri. Waweza kukuta ameenda kuungana ikulu na akina Kabudi kumshauri mkuu wa kaya.
 
Back
Top Bottom