Kingsmann
JF-Expert Member
- Oct 4, 2018
- 4,805
- 17,850
Kwanza nianze kwa kusema RIP mfalme wa Crank Music Tanzania.
Leo ni siku ya huzuni kweli kweli wapenda bongofleva hasa ile ya zamani. Ni wazi ladha ya bongofleva ya enzi za akina CPwaa ilikuwa na ladha yake tofauti kabisa na sasa ambapo kuna copy and paste nyingi sana za nje ya nchi.
Turudi kwenye msingi wa hii thread, kama taarifa za kidaktari zilivyosema kwamba CPwaa kafariki kwa Pneumonia (Nimonia), hivyo hilo libaki kama lilivyo. Japo kuna wanaozusha kwamba ni deportivo la coruna lkn hizo ni habari zisizo na uthibitisho.
Lakini ukijaribu kufuatilia maisha yake ya miezi kadhaa iliyopita utagundua kuna kitu hakiko sawa. Kwa miezi kadhaa CPwaa hakuwa active kwenye mitandao ya kijamii kama ilivyozoeleka. Mathalani kwenye mtandao wa Instagram ambapo ndio alikuwa anaupenda sana, mara ya mwisho kupost ilikuwa November 1, ina maana mpaka mauti yanamfika leo ilikuwa imeshapita miezi 2 na nusu bila kupost chochote kitu ambacho sio kawaida yake toka ajiunge na mtandao huo mwaka 2013.
Hii inaonesha kuna kitu nyuma ya pazia ambacho kilikuwa hakiko sawa kwa mfalme huyu. Ni nini kilimsibu?
PIA SOMA> TANZIA - Msanii Ilunga Khalifa maarufu 'C Pwaa' afariki dunia Hospitali ya Taifa Muhimbili
CPwaa akiwa na D-Banj mwaka 2010
CPwaa akiwa na Mesen Selekta mwaka2013