Nini kimemuua CPwaa? Kuna kitu hakijakaa sawa

Kingsmann

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2018
Posts
4,805
Reaction score
17,850
Kwanza nianze kwa kusema RIP mfalme wa Crank Music Tanzania.

Leo ni siku ya huzuni kweli kweli wapenda bongofleva hasa ile ya zamani. Ni wazi ladha ya bongofleva ya enzi za akina CPwaa ilikuwa na ladha yake tofauti kabisa na sasa ambapo kuna copy and paste nyingi sana za nje ya nchi.

Turudi kwenye msingi wa hii thread, kama taarifa za kidaktari zilivyosema kwamba CPwaa kafariki kwa Pneumonia (Nimonia), hivyo hilo libaki kama lilivyo. Japo kuna wanaozusha kwamba ni deportivo la coruna lkn hizo ni habari zisizo na uthibitisho.

Lakini ukijaribu kufuatilia maisha yake ya miezi kadhaa iliyopita utagundua kuna kitu hakiko sawa. Kwa miezi kadhaa CPwaa hakuwa active kwenye mitandao ya kijamii kama ilivyozoeleka. Mathalani kwenye mtandao wa Instagram ambapo ndio alikuwa anaupenda sana, mara ya mwisho kupost ilikuwa November 1, ina maana mpaka mauti yanamfika leo ilikuwa imeshapita miezi 2 na nusu bila kupost chochote kitu ambacho sio kawaida yake toka ajiunge na mtandao huo mwaka 2013.

Hii inaonesha kuna kitu nyuma ya pazia ambacho kilikuwa hakiko sawa kwa mfalme huyu. Ni nini kilimsibu?

PIA SOMA> TANZIA - Msanii Ilunga Khalifa maarufu 'C Pwaa' afariki dunia Hospitali ya Taifa Muhimbili


CPwaa akiwa na D-Banj mwaka 2010


CPwaa akiwa na Mesen Selekta mwaka2013


 

Aliugua wiki2 akawa anatumia dawa huku anaendelea na shughuli zake ilipofika jumatano akazidiwa wakamkimbiza muhimbili kumbe mapafu yalishaathirika sana na Pneumonia
 
Aliugua wiki2 akawa anatumia dawa huku anaendelea na shughuli zake ilipofika jumatano akazidiwa wakamkimbiza muhimbili kumbe mapafu yalishaathirika sana na Pneumonia
Pneumonia ni medical condition ya hatari sana, ilimwua pia James Brown kabla hata Covid haijaingia duniani. C-Pwaa alikuwa na historia ya pneumonia tangu utotoni kadri ndugu zake wanavvyofahamu. Sasa nini kiko nyuma ya pazia? Kwa nini kila mara watu wanataka kuhusisha kifo chochote na Covid? Tumuache apumuzike kwa amani!
 

Huyu profesa naye hajui maana ya matumizi ya mask (barakoa). Ukweli ni kuwa virusi vya Covid-19 huambukiza kwa kutumia njia tatu: pua, mdomo na macho. Kwa hiyo ukivaa barakoa kukinga mdomo na pua tu haitoshi kujikinga na virus hivyo kwani vinaweza kupitia machoni. Matumizi ya barakoa ni kumzuia aliyezivaa kuambuiza wengine, haimzuii yeye kuambukizwa! Wote tukivaa barakoa, tutapunguza sana maambukizi, lakini akivaa mtu mmoja tu katika jamii, wote tunakuwa na hatari ile ile ikiwa ni pamoja na aliyevaa barakoa hiyo!
 
Sars cov ikidevelop hupelekea nimonia pia.
 
Akili za wapinza ni kulazimisha kila kibaya kimesababishwa na rais John Pombe Magufuli
Hapa ndio wanapofeli na ikaonekana watu wenye chuki na waliokosa uzalendo.
 
Aliugua wiki2 akawa anatumia dawa huku anaendelea na shughuli zake ilipofika jumatano akazidiwa wakamkimbiza muhimbili kumbe mapafu yalishaathirika sana na Pneumonia
Huko nje ya tz ugonjwa huo unaitwa covid 19
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…